3285; Siyo kwa ajili yako.
Rafiki yangu mpendwa,
Pata picha umepewa nguvu ya uumbaji wa mnyama ambaye atakuwa na manufaa makubwa kwa watu.
Sharti ni unaweza kuumba mnyama mmoja tu, lakini unaweza kuweka chochote unachotaka kwa mnyama huyo.
Kutokana na mahitaji ambayo yapo, wewe unaona ukiumba paka ambaye anaweza kukamata vizuri panya lakini pia akawa na mwonekano mzuri kwa watu itakuwa vizuri zaidi.
Unaumba huyo paka na watu wanamkubali kwa sifa nzuri ulizomwekea.
Lakini wanakuja baadhi ya watu na kusema kama paka huyo angekuwa mkubwa zaidi na kuwa anabweka, angesaidia na kwenye ulinzi pia.
Unawaambia sawa na kuweka sifa hizo kwa huyo paka.
Sasa amekuwa paka ambaye pia ana sifa za mbwa.
Wanakuja wengine nao wanasema kama angefaa kutoa maziwa, angerahisisha mengi zaidi.
Unaona ni wazo zuri na hapo unaongeza sifa kwa paka huyo ambaye ameshakuwa na sifa za mbwa, anakuwa na sifa za mbuzi pia.
Wanaendelea kuja wengine na mapendekezo yao, ya jinsi mnyama huyo anapaswa kuwa.
Kwa sababu ya uwezo wako wa kuweka sifa yoyote na kwa sababu watu wanahitaji, unaendelea kuongeza sifa hizo.
Mwisho unaishia kuwa na mnyama ambaye haeleweki hata ni mnyama gani na ana sifa gani.
Badala ya watu kumkubali zaidi mnyama huyo, wanaanza kumkwepa.
Kwa sababu japo anaweza kufanya mengi, hakuna kimoja au vichache anaweza kufanya kwa ubora.
Hivyo ndivyo watu wanavyoharibu biashara zao wenyewe kwa kutaka kumridhisha kila aina ya mteja.
Wengi wanaona kwa kuwa wateja wanataka kitu cha aina fulani na wanaweza kukiweka basi wanakiweka.
Mwisho wanaishia kuwa na biashara ambayo haieleweki ni ya aina gani au iko bora zaidi kwenye kitu gani.
Unapojaribu kufanya kitu kimoja kimfae kila mtu, unaishia kuwa na kitu ambacho hakimfai yeyote.
Hivyo njia bora ya kuboresha na kulinda kile unachojenga ni kuwaambia baadhi ya watu siyo kwa ajili yao.
Hapo ni pale watu wanapokuja na mapendekezo mazuri lakini yanayoharibu maana ya kitu hicho.
Wakumbushe kitu hicho kina ubora zaidi kwenye eneo gani na kama kikitawanya ili kuongeza ubora mwingine itakuwa na athari kiasi gani kwenye kupunguza ubora wake.
Usikubali kutawanya kitu kiwe na ubora kwenye maeneo mengi.
Hilo linapunguza ukali wa huo ubora.
Zingatia ubora wa kitu kwenye eneo moja kuu ambalo ndiyo litakitofautisha na vitu vingine vyote.
Hilo litajenga ufanisi mkubwa sana kwenye kitu.
Hii haimaanishi kufanya kitu kile kile kwa mazoea bila kubadilika.
Ni lazima uendelee kubadilika na kuwa bora zaidi.
Lakini ubora huo uendelee kuwa kwenye lile eneo moja kuu ambalo umechagua.
Hiyo inajengea kitu sifa mahususi na ambayo inazidi kukifanya kuwa cha thamani zaidi.
Kwa sababu unaweza kufanya kitu, haimaanishi ufanye.
Wakatalie baadhi ya watu mapendekezo yao ili kulinda sifa mahususi ya kile ambacho unakijenga.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Unapojqribu kufanya kitu kimoja kimfae kila mtu unaishia kuwa na kitu ambacho hakimfai mtu.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Sitakubali kutawanya kitu kiwe na ubora kwenye maeneo mengi, kwa sababu hilo linapunguza ukali wa huo ubora
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni kweli kabisa tumepotea sana ajili ya kutaka kuwaridhisha watu wengi na tukapoteza ile maana ya biashara zetu kwa upande qangu mimi nilipanua sana wigo hadi nikapotelea huko na baada ya kushtuliwandiyo nimerudi na sasa mambo mengine hapana najulikana kwa jina la duka la jumla la vifaa vya bomba hadi niwe bilionea na duka lijiendeshe lenyewe na sintatoka nje ya ujenzi
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Kwa sababu unaweza kufanya kitu, haimaanishi ufanye.
Wakatalie baadhi ya watu mapendekezo yao ili kulinda sifa mahususi ya kile ambacho unakijenga.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Njia nzuri ya kuwajibu wale wanaokuja na mapendekezo yao kwako kuhusu kitu fulani, ni kuwajibu si kwa ajili yako.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Fanya cheneye manufaa,sio kinachomfaa kila mtu.
🙏🙏🙏
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Upekee na Ubora kwenye biashara ni silaha ya kufanikiwa. Achana na Mambo mengi Bali bakia kwenye kitu kimoja
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kuna watu biashara yangu siyo kwaajili yao
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
kupokea maoni ya kila mteja kwenye biashara yako,mwisho wake unaishia kuwa na mnyama ambaye haeleweki hata ni mnyama gani na ana sifa gani.✍️
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Wakatalie watu baadhi ya mapendekezo yao ili kulinda sifa mahususi
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hakika hapa tunaona msimamo na ubora,fanya vichache kwa ukumbwa na ubora kuliko kuhangaika na mengi
LikeLike
Ndiyo
LikeLike