3346; Hakikisha upo tayari.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Kila mtu anataka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yake.
Japokuwa mafanikio yana maana tofauti kwa watu tofauti.
Wengi kati ya hao wanaoyataka mafanikio, huwa wanaianza safari ya kuyaendea mafanikio wanayoyataka.
Wanaanza safari yao wakiwa na shauku kubwa, wakiwa wanaona wazi kabisa kwamba wanaenda kuyafikia mafanikio wanayoyataka.
Lakini kwa bahati mbaya sana, wengi huwa hawadumu kwenye safari hiyo ya mafanikio kwa muda mrefu.
Kwani huwa haiwachukui muda mrefu kabla hawajakutana na uhalisia wa safari hiyo, ambao unaumiza.
Kwanza wanakutana na vikwazo, matatizo na changamoto mbalimbali ambazo zinakuwa kikwazo kwao kuendelea. Wanaangushwa na watu waliokuwa wanawategemea, kwa kudanganywa, kuibiwa na hata kushitakiwa.
Watu waliodhani wako nao upande mmoja, wanagundua siyo kama hivyo walivyodhani.
Pili wanafanya makosa mbalimbali ambayo yanaifanya safari kuwa ngumu zaidi. Makosa hayo yanatokana na kutokujua kipi sahihi kufanya au kuchelewa kufanya yaliyo sahihi. Makosa yao yanazidisha ugumu wa safari na mtu kuona kama mafanikio makubwa hayawezekani.
Hali hizo ambazo kila anayeingia kwenye safari ya mafanikio anakutana nazo, ndizo zimekuwa zinawatenganisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Wanaofanikiwa wanaendelea na safari licha ya hayo magumu wanayokuwa wamekutana nayo. Kwa kuendelea na safari hiyo, wanayavuka hayo na kuweza kupata mafanikio makubwa wanayoyataka.
Wanaoshindwa huwa wanakata tamaa na safari hao kuishia kwenye yale magumu wanayokuwa wamekutana nayo. Wanakuwa wameiona safari haiwezekani tena, huku wakiona mengine yakiwa rahisi zaidi na hivyo kwenda kwenye hayo rahisi.
Hakuna watu ambao wamezaliwa kuyaweza mafanikio na wengine kuyashindwa.
Tofauti pekee ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa ni utayari wao kwenye safari.
Wanaofanikiwa wanakuwa wapo tayari kukabiliana na chochote bila kukwama. Wao wanachotaka ni mafanikio makubwa na hakuna chochote kinachokuwa na nguvu ya kuwasumbua kwenye hilo.
Wanaoshindwa wanakuwa hawapo tayari kukabiliana na magumu wanayokutana nayo.
Wanataka kila kitu kiwe rahisi kadiri ya wanavyotaka wao. Wanapokutana na magumu, wanaachana na hicho wanachofanya na kwenda kwenye kingine wanachoona ni rahisi zaidi kwao.
Je wewe umechagua upande upi? Na una ushahidi gani kwamba upo kwenye huo upande ambao umechagua?
Ni rahisi kujiambia upo upande wa mafanikio, lakini kama umekuwa unahangaika na njia nyingi za mafanikio, unajidanganya na hutafanikiwa.
Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti tunayoijenga, tupo kwenye safari ya kujenga mafanikio makubwa kwa kila mmoja huku tukiwa na maandalizi sahihi.
Tumejiandaa kukabiliana na chochote tunachokutana nacho kwenye hiyo safari bila ya kuishia njiani.
Tunajua kabisa kwamba kupata mafanikio kuna gharama kubwa ya kulipa na tupo tayari kulipa gharama hiyo.
Magumu na changamoto tunazokutana nazo tunajua kabisa kwamba ni sehemu ya hiyo safari na hivyo hatukwami kwa namna yoyote ile.
Jamii hii ya wanamafanikio inatuwajibisha kubaki kwenye mchakato wa kuyaendea mafanikio bila kukata tamaa wala kuishia njiani.
Kwa kuwa na wengine ambao tunaambatana nao na ambao wanatuwajibisha, tunalazimika kuwa tayari kwa ajili ya safari ya kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe