Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi wamekuwa wakiyaendesha maisha yao kwa kubahatisha. Kila wanachofanya ni kwa mazoea na hawana uhakika ni matokeo ya aina gani wanayokwenda kupata.
Na hilo linaanzia kwenye tabia ya watu ya kutokuwa na mipango ya muda mrefu kwenye maisha yao. Wanafanya kile kinachokuja mbele yao kwa wakati husika.
Sasa kwa sababu dunia huwa haikosi vitu vya watu kufanya, watu huishia kuchoka kwa kuhangaika na mengi na yasiyokuwa na tija.

Katika wakati wowote ule, kila mtu atakuwa anafanyia kazi malengo fulani. Kama mtu atakuwa hafanyii kazi malengo yake, basi atakuwa anafanyia kazi malengo ya mtu mwingine.
Kwa watu kukosa malengo wanayofanyia kazi, wamekuwa wanajikuta wanatumika na wengine na hivyo kuwanufaisha zaidi hao wengine kuliko wanavyonufaika wao wenyewe.
Lakini pia, kumekuwa na tabia ya watu kukimbia magumu na kutaka mambo rahisi. Wengi wanapokutana na magumu kwenye yale wanayofanya, huwa wanaona hawawezi kuendelea, hivyo wanaacha na kwenda kwenye mambo mengine.
Na kubwa zaidi, wengi ambao hawafanikiwi huwa ni rahisi sana kukatishwa tamaa na maoni ya watu wengine. Pale wengine wanapowakosoa kwa yale wanayofanya, wanakata tamaa na kuacha. Kwa sababu watu huwa hawaishiwi ukosoaji, wengi sana wamekuwa wanakwama.
Mafanikio yako kwenye maisha, yanategemea sana jinsi unavyoweza kuyavuka hayo yaliyoainishwa hapo juu, ambayo ni kutumika na wengine, kukutana na magumu na kukatishwa tamaa. Kama unaweza kuyavuka hayo na kuendelea na safari yako, basi mafanikio yatakuwa yako kwa uhakika.
Karibu uangalie kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo utajifunza kwa kina zaidi sifa unazohitaji kujijengea ili uweze kuyakabili maisha yako ya kila siku na kupata ushindi mkubwa. Fungua kipindi hapo chini, ujifunze na kwenda kuchukua hatua ili ujijengee mafanikio ya uhakika kwenye maisha yako.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.