Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,
Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya CHUO CHA MAUZO.
Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.
Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.
Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.
Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.
Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 61 na 62
Kwenye mbinu namba 61 tulijifunza ukamilishaji wa kujipongeza.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 61 tulijifunza kwamba
Pale mteja anapoona analipa gharama kubwa, mkumbushe kwamba anapaswa kuyafurahia maisha, hivyo ajipongeze.
Kwa mfano, mteja anakuambia gharama ni kubwa, unamjibu hivi;
“Ni kweli gharama ni kubwa, lakini siyo kitu unachofanya kila siku. Jipongeze leo.
Na kwenye ukamilishaji wa kufanya kazi kwa juhudi, mbinu namba 62 tulijifunza kwamba
Watu wengi wanafanya kazi kwa juhudi, lakini bado hawathamini hilo. Wakumbushe kwamba sababu ya wao kufanya kazi kwa juhudi ni kupata vitu vizuri kama unachomuuzia na atakuwa tayari kuwa nacho
Kwa mfano, mteja anakuambia gharama ni kubwa,
Unamjibu hivi;
“Najua ni gharama kubwa. Na ndiyo maana watu kama wewe mnafanya kazi kwa juhudi, ili kuweza kumudu vitu vizuri kwenye maisha. Na baada ya hapo unamwambia akamilishe malipo.
SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 61-62
Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 63 na 64
Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

- Ukamilishaji wa unastahili.
Ukamilishaji huu unatumia hitaji la watu kutaka kuona wanastahili kuwa na vitu vizuri. Waonyeshe kwamba wanastahili kuwa na hicho unachowauzia na watasukumwa kuwa nacho
Kwa mfano mteja anakuambia gharama ni kubwa, wewe mwambie hivi;
“Najua ni gharama kubwa, na unastahili kuwa nacho. Kama wewe hustahili kuwa na hiki, sijui nani atakayestahili.
Weka sahihi yako hapa, tukamilishe hili, kamilisha malipo, ipi njia nzuri kwako kukamilisha malipo?
Kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo ili uende ukafurahie uwekezaji wako au matunda ya kazi yako.
- Ukamilishaji bei ni kubwa.
Ukamilishaji huu, unatumia pingamizi analotoa mteja kama sababu kwa nini wanatakiwa kununua. Hupingani na pingamizi hilo wala kulitatua, badala yake unamwonyesha hilo pingamizi analotoa ndiyo sababu ya yeye kufanya maamuzi sasa.
Kwa mfano, pale mteja anaposema bei ni kubwa sana.
Wewe mjibu hivi;
“Hiyo ndiyo sababu unapaswa kufanya manunuzi sasa ili uwe na kitu hiki na kuanza kuyafurahia maisha yako sasa. Weka sahihi yako hapa(hii inatumika kwa biashara ambazo zinahitaji mteja aweke ili akamilishe malipo, ipi njia nzuri kwako kukamilisha malipo? Kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo.
Mwisho, Ukamilishaji ni hatua muhimu kwa kila mtu kupata kila anachotaka kwenye maisha yake.
Kwenye mazungumzo yoyote yale na mteja, hakikisha kuna kitu unakamalisha. Usikubali kutoka mikono mitupu, pambana kuhakikisha juhudi ulizoweka haziendi bure.
Kama umekosa mauzo, basi upate hata miadi, namba ya simu ya kuendelea kumfuatilia na mteja wa rufaa.
Kauli yetu inasema ABC-always be closing mara zote unapaswa kukamilisha wateja.
Nenda kakamilishe mauzo makubwa kadiri ya malengo yako uliyojiwekea leo.
Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi kupitia mbinu ulizojifunza leo na mbinu nyingine za nyuma ulizojifunza.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii; Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo
Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki kukujali katika mauzo,
Rafiki na mwalimu wako anayekupenda na kukujali katika mauzo,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504