Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,
Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya CHUO CHA MAUZO.
Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.
Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.
Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.
Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.
Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 63 na 64
SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 63-64
Kwenye mbinu namba 63 tulijifunza ukamilishaji wa unastahili.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 63 tulijifunza kwamba ukamilishaji huu unatumia hitaji la watu kutaka kuona wanastahili kuwa na vitu vizuri. Waonyeshe kwamba wanastahili kuwa na hicho unachowauzia na watasukumwa kuwa nacho
Kwa mfano mteja anakuambia gharama ni kubwa, wewe mwambie hivi;
“Najua ni gharama kubwa, na unastahili kuwa nacho. Kama wewe hustahili kuwa na hiki, sijui nani atakayestahili.
Weka sahihi yako hapa, tukamilishe hili, kamilisha malipo, ipi njia nzuri kwako kukamilisha malipo?
Kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo ili uende ukafurahie uwekezaji wako au matunda ya kazi yako
Na kwenye ukamilishaji wa bei kubwa mbinu namba 64 tulijifunza kwamba ;Ukamilishaji huu, unatumia pingamizi analotoa mteja kama sababu kwa nini wanatakiwa kununua. Hupingani na pingamizi hilo wala kulitatua, badala yake unamwonyesha hilo pingamizi analotoa ndiyo sababu ya yeye kufanya maamuzi sasa.
Kwa mfano, pale mteja anaposema bei ni kubwa sana.
Wewe mjibu hivi;
“Hiyo ndiyo sababu unapaswa kufanya manunuzi sasa ili uwe na kitu hiki na kuanza kuyafurahia maisha yako sasa. Weka sahihi yako hapa(hii inatumika kwa biashara ambazo zinahitaji mteja aweke ili akamilishe malipo, ipi njia nzuri kwako kukamilisha malipo? Kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo.
Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 65 na 66
Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;
65. Ukamilishaji wa muhtasari.
Huu ukamilishaji huu unatumika mara baada ya kufanya mazungumzo na mteja na kumueleza kile unachouza.
Sasa unakuja kuhitimisha yale ambayo mmkubaliana kwa kumpa muhtasari
Kwa mfano,
“Henry, wacha nikukumbushe nini unakwenda kupata hapa; 1) unapata maktaba nzima ya zana za mafunzo 2) mafunzo ya sauti 3) mafunzo ya video 4) vitabu vyote 5) namba ya mawasiliano ya msaada bure. Hivyo basi, weka sahihi yako hapa.”
Chukua muda na andika muhtasari wa yale yote mteja anakwenda kupata anaponunua kisha wasilisha muhtasari huo wakati wa kukamilisha mauzo, inaonyesha thamani kubwa mteja anayokwenda kupata na kumsukuma kuchukua hatua.
Kwa mfano, Muhtasari wa kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI, ukinunua kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI unapata manufaa yafuatayo, moja unaingia kwenye program ya NGUVU YA BUKU, mbili, unapata masomo ya uwekezaji na fedha 3, unakaa kwenye program kwa miaka 10, 4, unapata usimamizi wa karibu kwa miaka 10 na 5 unaidiwa kufungua akaunti na kukutanishwa na watu wa UTT AMIS endapo una maswali ya kuwauliza.
Hapo mteja anaona thamani anayokwenda kupata na hivyo inakuwa rahisi kwake kukamilisha manunuzi.

66. Ukamilishaji wa sina fedha.
Pale mteja anaposema sina fedha kwa sasa.
Mwambie hivi mteja ;
“Kama nikikusaidia njia ya kuweza kupata fedha, je utakuwa tayari kukamilisha manunuzi sasa? Kama ndiyo, weka sahihi hapa,( kuweka sahihi ni kwa biashara ambazo zinahusisha mtu kuweka sahihi kama vile mauzo ya viwanja, mikataba ya sheria juu ya kitu fulani.
Kama ndiyo, lipia kiasi ulichokuwa nacho sasa.
Ukamilishaji huu unakufanya ujihakikishie kwamba kikwazo pekee kwao ni fedha. Na hivyo ukiweza kuwaonyesha njia za kupata fedha, wananunua. Ila kama fedha siyo kikwazo pekee, hawatakubali, hivyo utapaswa kujua kikwazo halisi.
Mwisho, Ukamilishaji ni hatua muhimu kwa kila mtu kupata kila anachotaka kwenye maisha yake.
Kwenye mazungumzo yoyote yale na mteja, hakikisha kuna kitu unakamalisha. Usikubali kutoka mikono mitupu, pambana kuhakikisha juhudi ulizoweka haziendi bure.
Kama umekosa mauzo, basi upate hata miadi, namba ya simu ya kuendelea kumfuatilia na mteja wa rufaa.
Kauli yetu inasema ABC-always be closing mara zote unapaswa kukamilisha wateja.
Nenda kakamilishe mauzo makubwa kadiri ya malengo yako uliyojiwekea leo.
Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi kupitia mbinu ulizojifunza leo na mbinu nyingine za nyuma ulizojifunza.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii; Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo
Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,
Rafiki na mwalimu wako anayekupenda na kukujali katika mauzo,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504