
Rafiki Yangu Mpendwa,
Unajua nini kinauma?
Mtoto wako anaenda shule kila siku…
Anakazana…
Lakini hawezi hata kuweka akiba ya buku.
Sio kwa sababu hana hela.
Ni kwa sababu hajawahi kufundishwa.
Na hata wewe hujawahi kumfundisha.
Wengi wetu tunadhani watoto ni wadogo sana kufundishwa fedha.
Wengi tunasema:
Watapata tabu bure.
Wangojee wakue kwanza.
Lakini hiyo ndio sumu kubwa zaidi.
Umemwona mtoto wa jirani yenu?
Ana miaka 12 tu… lakini ana “Akaunti” yake.
Anaandika kila hela anayopata.
Anajua kutumia na kuweka akiba.
Mtoto Wako Je?
Anachukua elfu moja…
Anaimaliza yote na bado anakwambia nitumie tena.
Na unamtumia.
Kila siku.
Mwaka mzima.
Miaka kadhaa…
Mpaka kesho hajui thamani ya buku.
Hajui kusema nitahifadhi.
Na bado unamuita smart?
Kibaya zaidi ni kwamba watu wazima wengi ndo kwanza wana matatizo ya fedha.
Na wanadhani watoto wao watajifunza wakikua.
Mbona na wewe umekua lakini bado hela hazikutoshi?
Unawapenda watoto wako?
Basi wape zawadi ambayo hawataisahau maisha yao yote:
Maarifa ya fedha.
Kuanza ni rahisi kuliko unavyodhani.
Anza kwa kumfundisha kutunza buku moja.
Moja tu.
Kwa wiki.
Kwa mwezi.
Hata kwa siku.
Tengeneza kopo au boksi.
Kiite Boksi La Buku.
Mwambie:
Kila siku utaweka buku hapa ndani, mwisho wa mwezi tutajua umekomaa kiasi gani.
Mfanye ajivunie akiba yake.
Mfanye ahisi kama mjasiriamali.
Mpe changamoto za “ku-save.”
Utaona tabia yake inabadilika.
Fedha ni mchezo wa akili.
Na akili inaanza mazoezi mapema.
Nilikutana na mama mmoja Keko, Dar.
Mtoto wake wa miaka 10 alikuwa anauza keki za shilingi 500.
Anachukua faida yake, anaweka buku kila jioni kwenye kopo.
Mama alimfundisha baada ya kushindwa kulipa ada mwaka mmoja.
Baada ya miezi 6…
Yule mtoto alikuwa na Tshs 120,000.
Alijinunulia viatu.
Alichangia ada.
Akaambiwa: Wewe utakuwa mtu mkubwa sana.
Na ni kweli.
Leo yule mtoto ana ndoto za kuwa “mfanyabiashara maarufu duniani.”
Na anaiamini.
Kwa sababu anaona inavyowezekana.
Usisubiri watoto wakue.
Waanze sasa.
Buku moja kwa siku ni shule kubwa kuliko darasa.
Tengeneza “Mpango wa Kuokoa Buku” nyumbani kwako leo.
Kila mtoto aanze.
Hii siyo hadithi, ni maisha.
👉 Anza leo, kabla mtoto wako hajaanza kukulaumu kesho.
Anyway, kama bado hujaweka oda ya kitabu hiki kipya cha NGUVU YA BUKU TOTO,
Basi nafasi yako hii hapa 👇 kabla ya tarehe 9.
Ni hapa 👉https://wa.link/2x7eqq
Karibu.
Imetoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir