
Hapo Zamani,
Samson alikuwa kijana wa kawaida aliyeamua kuanzisha biashara ya kuuza vitenge Kariakoo, Dar es Salaam.
Hakuwa na mtaji mkubwa, lakini alikuwa na ndoto kubwa ndoto ya kuinua familia yake,
Kutoka kwenye maisha ya kukopa hadi maisha ya kutajwa kwenye semina kubwa kama ‘mfanyabiashara aliyefanikiwa.’
Lakini kuna kitu kilimkosesha usingizi ni kwamba biashara yake ilikuwa haikui.
Kila siku alifungua duka, aliketi akisubiri wateja, lakini pesa haikufuata jasho lake.
Siku moja akiwa kwenye daladala, alisikia vijana wawili wakizungumza kwa furaha kuhusu jinsi walivyoongeza mauzo kwenye biashara zao kwa msaada wa kitabu kimoja kinachoitwa CHUO CHA MAUZO.
Mmoja alisema:
“Bila hiki kitabu, nisingejua kuwa neno dogo tu kama ‘Habari Njema’ linaweza kuvutia mteja kuliko punguzo.”
Samson alishtuka. Kitabu? Mauzo? Hayo siyo mambo aliyowahi kuyapa uzito.
Alikuwa akiamini kwamba mauzo yanakuja tu kama bahati au kwa kupumguza bei.
“Nani ana muda wa kusoma vitabu?”
Alijiambia. “Mbona mimi nataka pesa sasa hivi, siyo masomo.”
Lakini wiki hiyo hiyo alipoteza mteja mkubwa aliyekuwa tayari kununua mzigo wa laki mbili.
Mteja alimwambia:
“Samahani kaka, sikuhisi kama unajua unachouza.”
Maneno hayo yalimchoma kama msumari wa moto.
Samson alimkumbuka kijana mmoja anayeitwa Musa, aliyekuwa na duka jirani.
Musa alikuwa na foleni ya wateja kila asubuhi.
Akamwendea na kumuuliza:
“Kaka, unatumia uchawi gani?”
Musa alicheka na kumpa nakala ya kitabu cha CHUO CHA MAUZO.
“Soma hiki. Hiki ndicho kilichonigeuza kutoka kuwa muuzaji hadi kuwa mshauri wa wateja.”
Samson alianza kusoma. Kurasa ya kwanza akisema:
“Wateja hawataki tu bidhaa, wanatafuta suluhisho.
Ukiweza kuzungumza na hisia zao, utauza zaidi ya bidhaa utauza matumaini.”
Alijifunza mbinu za kuuliza maswali sahihi, kutumia lugha ya kuhamasisha, kuandaa ofa za kuvutia, na kutengeneza uhusiano wa kudumu na wateja.
Hakuona mabadiliko ya haraka.
Ilibidi apambane na woga wa kuzungumza, kukumbana na wateja wagumu, na kuacha tabia ya kusema “Karibu kaka” bila maana.
Lakini siku moja, mteja mpya alikuja na Samson alitumia mojawapo ya mbinu kutoka kitabu kile.
Badala ya kuuliza “Unataka kitenge gani?”
Aliuliza:
“Unatafuta kitenge kwa ajili ya kukivaa kwenye hafla ya aina gani?”
Mteja alitabasamu.
“Kwa harusi ya mdogo wangu. Wewe ni tofauti.”
Akanunua vitambaa vitatu bila kuomba punguzo.
Miezi mitatu baadaye, Samson alikuwa tayari kuongeza duka la pili. Lakini janga lilitokea:
Ghafla washindani walitoa bei za chini sana sokoni.
Wateja wengi walienda kwao. Samson akakaribia kukata tamaa.
Lakini alifungua tena kurasa za mwisho za CHUO CHA MAUZO na kukumbushwa:
“Unaposhindwa kuuza kwa bei, uza kwa thamani.”
Akaanza kuongeza huduma ya kufungasha zawadi, kutoa ushauri wa mitindo kwa wateja, na kutuma ujumbe wa shukrani kwa kila mteja aliyenunua.
Sasa Samson hakuwa tu muuzaji wa vitenge alikuwa mshauri wa mavazi ya hafla.
Biashara yake ilikua kwa kasi ya ajabu.
Mapato yake yakaongezeka MARA MBILI ndani ya miezi sita.
Samson alianza kushiriki mafunzo kwa wafanyabiashara wengine wadogo.
Akawaambia:
“Siri haipo kwenye bidhaa, ipo kwenye akili yako na akili inachochewa na maarifa.
Na maarifa haya niliyapata kwenye kitabu cha CHUO CHA MAUZO.”
Leo hii, Samson ni mfanyabiashara mkubwa, ana wafanyakazi, duka la mtandaoni, na anaandaliwa kuhudhuria semina ya kimataifa.
Yote yalianza pale alipoamua kuchukua kitabu na kukisoma.
Kama wewe ni mfanyabiashara na unajiuliza “Nifanye nini ili niuze zaidi?”
Jibu linaweza kuwa si bidhaa mpya, si duka kubwa zaidi bali ni maarifa mapya.
👉 Chukua kitabu cha CHUO CHA MAUZO leo.
👉 Geuza biashara yako kuwa shujaa wa sokoni.
Anyway, kama bado hujapata kitabu hiki, unaweza kuweka oda yako hapa 👇
https://wa.link/6pruxn
Karibu.
0756694090.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir