‎
‎Rafiki yangu mpendwa,
‎
‎Leo nina taarifa njema sana kwako, taarifa za tukio kubwa ambalo huwa linatokea mara moja tu kila mwaka.
‎
‎Tukio hilo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jukwaa la kukutana watu wenye kiu ya mafanikio makubwa na wanaoyapambania bila kukata tamaa.
‎
‎Mwaka huu 2025, tunakwenda kuwa na semina hii kwa mwaka wa 10 mfululizo, na pia ndiyo itakuwa semina ya mwisho kabisa.
‎
‎Sababu za kwa nini ni ya mwisho na nini kitakachofuata, utazipata utakaposhiriki semina.
‎
‎Hii siyo fursa ya kukosa, kama umewahi kushiriki semina hizi huko nyuma, unajua thamani yake.
‎
‎Karibu mwaka huu 2025 upate thamani kubwa zaidi, lakini pia ukutane na wengine ambao wamekuwa wakishiriki.
‎
‎Kama hujawahi kushiriki SEMINA ZA KISIMA CHA MAARIFA, hii ndiyo nafasi yako ya kipekee ya kutimiza hilo.
‎
‎Kwani ukiikosa nafasi hii, hutaweza kuipata tena.
‎
‎Karibu ushiriki na utayabadili kabisa maisha yako.
‎
‎Kitu kimoja zaidi ni kwamba SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2025 itafanyika Zanzibar,
‎
‎…hii ikiwa ndiyo mara ya kwanza na pekee ya semina hii kufanyika nje ya Tanzania Bara.
‎
‎Tumeifanya semina hii Dar, Dodoma, Arusha na Mbeya.
‎
‎Kwa awamu hii ya mwisho, tunayavuka maji na kwenda Zanzibar, tena semina itafanyika pembeni ya ufukwe wa bahari.
‎
‎Hivyo siyo tu tutapata mafunzo, bali pia tutapata mapunziko mazuri sana. Usikubali kukosa semina hii ya kumi na ya mwisho kabisa.
‎
‎Nichukue nafasi hii kukukaribisha sana wewe rafiki yangu kwenye semina hii, karibu uungane na wanamafanikio wenye kiu kubwa.
‎
‎Karibu pia ujue ngwe inayofuata baada ya kuhitimisha semina hii.
‎
‎Kwani safari ya Ubilionea ni lazima ifikiwe, na kila aliyedhamiria.
‎
‎Taarifa kamili za SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2025 zipo hapo chini, zisome kwa kina na chukua hatua mara moja.
‎
‎Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
‎Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
‎
‎SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2025
‎
‎Kauli mbiu:
‎“Jifunze, Jipange, Tekeleza: Jenga Maisha na Biashara Yenye Thamani na Uhuru wa Kifedha”
‎
‎📍 Mahali: Zanzibar Ocean View Hotel
‎📅 Tarehe: Ijumaa 10 Oktoba – Jumatatu 13 Oktoba 2025
‎
‎💎 LENGO LA SEMINA
‎
‎✅ Kukuwezesha kuboresha biashara yako ili ikue haraka na kuwa endelevu, na kufikia thamani ya dola bilioni 1.
‎
‎✅ Kukupa mfumo wa usimamizi wa fedha binafsi ili ujenge utajiri na kufikia uhuru wa kifedha.
‎
‎✅ Kukupa mpango wa utekelezaji wa hatua kwa hatua utakaoanza kuufanyia kazi mara moja.
‎
‎✅ Kukuunganisha na watu wanaofanana na wewe kwa mitandao ya ukuaji.
‎
‎✅ Kupata mapumziko pamoja na utalii wa Zanzibar huku ukijifunza.
‎
‎ 📅 RATIBA KAMILI YA SEMINA
‎
‎🗓️ Ijumaa 10 Oktoba 2025
‎
‎✅ Check-in Zanzibar Ocean View Hotel kuanzia saa 8:00 mchana.
‎
‎✅ Mapokezi na utambulisho wa washiriki jioni.
‎
‎✅ Chakula cha usiku na mijadala ya kujenga mtandao.
‎
‎🗓️ Jumamosi 11 Oktoba 2025: Mafunzo ya BILIONEA MAFUNZONI
‎
‎Mada:
‎“Jinsi ya Kujenga Biashara Yenye Kukua Haraka na kufikia thamani ya Zaidi ya dola bilioni 1.”
‎
‎1️⃣ Kipindi 1: Kujenga Bidhaa/Huduma Inayokabiliana na ushindani Sokoni
‎
‎• Tambua tatizo la mteja na utengeneze bidhaa bora.
‎
‎• Unda mfumo rahisi wa masoko unaovutia wateja bila gharama kubwa.
‎
‎• Mpango wa utekelezaji wa kuboresha au kuunda bidhaa yako.
‎
‎2️⃣ Kipindi 2: Mauzo na Huduma kwa Wateja kwa Ukuaji wa Haraka
‎
‎• Mfumo wa mauzo unaofanya kazi na maneno sahihi ya kuuza.
‎
‎• Huduma bora inayowafanya wateja warudi mara kwa mara.
‎
‎• Mpango wa mfumo wa mauzo na huduma.
‎
‎3️⃣ Kipindi 3: Fedha na Timu Imara
‎
‎• Usimamizi wa fedha kwa ukuaji na kuandaa bajeti rahisi.
‎
‎• Kuajiri na kukuza timu bila kuongeza gharama kubwa.
‎
‎• Mpango wa fedha na mpango wa timu.
‎
‎4️⃣ Kipindi 4: Uongozi, Teknolojia, Mitandao na Urithi
‎
‎• Nidhamu na mindset ya ushindi ya uongozi.
‎
‎• Kutumia teknolojia kuongeza ufanisi.
‎
‎• Kujenga mtandao na kuandaa urithi wa biashara yako.
‎
‎• Mpango wa kila kipengele kwenda kufanyia kazi.
‎
‎ 🗓️ Jumapili 12 Oktoba 2025: Mafunzo ya NGUVU YA BUKU
‎
‎Mada:
‎“Vunja Laana Ya Umasikini, Jenga Utajiri Wa Vizazi.”
‎
‎1️⃣ Kipindi 1: Kuongeza Mapato
‎• Njia za kuongeza kipato na kujenga vyanzo vingi vya mapato.
‎
‎• Mpango wa kuongeza kipato ndani ya siku 30.
‎
‎2️⃣ Kipindi 2: Bajeti, Akiba na Matumizi Bora
‎
‎• Kuandaa bajeti rahisi na kuishi ndani ya kipato.
‎
‎• Mbinu za kuweka akiba bila kujisikia kubana.
‎
‎• Kupunguza matumizi yasiyo lazima bila kuharibu maisha.
‎
‎• Mpango wa bajeti na akiba.
‎
‎3️⃣ Kipindi 3: Usimamizi wa Madeni na Kutoa
‎
‎• Kutoka kwenye madeni hatua kwa hatua.
‎
‎• Udhibiti wa mikopo na kutoa kwa jamii huku unakua kifedha.
‎
‎• Mpango wa kulipa madeni na kutoa.
‎
‎4️⃣ Kipindi 4: Uwekezaji na Ulinzi wa Utajiri
‎• Utangulizi wa kuwekeza kwa uelewa na kidogo ulichonacho.
‎• Jinsi ya kulinda mali zako kwa bima na mfumo wa kisheria.
‎• Mpango wa uwekezaji na ulinzi wa utajiri.
‎
‎🗓️ Jumatatu 13 Oktoba 2025: Ziara ya Utalii
‎
‎Ziara ya Pamoja: City Tour, Prison Island & Nakupenda Sandbank
‎
‎✅ Ziara ya Prison Island (kuona kasa wakubwa, historia ya gereza na kisiwa).
‎
‎✅ Ziara ya Nakupenda Sandbank kwa kupumzika na kuogelea kwenye mchanga wa bahari ya bluu.
‎
‎✅ City Tour ya Zanzibar (Stone Town, Forodhani, masoko ya spice na maeneo muhimu ya kihistoria).
‎
‎✅ Transfer, Guide, Soft drinks, Chakula cha mchana (seafood), Boat na entrance fees zote.
‎
‎💰 GHARAMA ZA KUSHIRIKI
‎
‎✅ Mtu mmoja: Tsh 880,000/=
‎
‎✅ Wawili (chumba kimoja): Tsh 1,550,000 (Tsh 775,000 kwa kila mmoja)
‎
‎🎯 OFA YA MALIPO YA MAPEMA
‎
‎✅ Mpaka 01/09/2025:
‎• Mtu mmoja: Tsh 780,000
‎• Wawili: Tsh 1,350,000 (Tsh 675,000 kwa kila mmoja)
‎
‎🔖 JINSI YA KUJISAJILI
‎
‎✅ Thibitisha nafasi yako kwa kulipa Tsh 100,000 kabla ya tarehe 31/07/2025.
‎✅ Malipo yote yakamilike kabla ya tarehe 06/10/2025.
‎
‎ADA INAJUMUISHA:
‎
‎✅ Malazi na chakula kamili (breakfast, lunch na dinner) ndani ya Zanzibar Ocean View Hotel (siku 3).
‎
‎✅ Vipindi vyote vya mafunzo ya semina kwa siku 2, Jumamosi na Jumapili.
‎
‎✅ Ziara ya utalii Zanzibar siku ya Jumatatu.
‎
‎✅ Mwongozo (Guide) na viingilio kwenye maeneo ya utalii.
‎
‎KWA NINI USIKOSE?
‎
‎✅ Utatoka na mpango kamili wa biashara na fedha binafsi wa kwenda kufanyia kazi mara moja.
‎
‎✅ Utapumzika na kupata nguvu mpya Zanzibar.
‎
‎✅ Utajenga mtandao wa watu wenye malengo kama yako.
‎
‎✅ Utapata uelewa wa kina na hatua za utekelezaji kutoka kwa wakufunzi wenye matokeo.
‎
‎Kuwahi kuthibitisha nafasi yako, ingia hapa 👇
‎
‎https://wa.link/a5u2kf
‎
‎🌟 Usikubali nafasi hii ya mwisho ikupite chukua hatua sasa, jiandikishe leo, na anza safari ya kubadilisha biashara na maisha yako milele!