‎Hapo Zamani,

Samson alikuwa kijana wa kawaida aliyeamua kuanzisha biashara ya kuuza vitenge Kariakoo, Dar es Salaam.
‎
‎Hakuwa na mtaji mkubwa, lakini alikuwa na ndoto kubwa ndoto ya kuinua familia yake,
‎
‎Kutoka kwenye maisha ya kukopa hadi maisha ya kutajwa kwenye semina kubwa kama ‘mfanyabiashara aliyefanikiwa.’
‎
‎Lakini kuna kitu kilimkosesha usingizi ni kwamba biashara yake ilikuwa haikui.
‎
‎Kila siku alifungua duka, aliketi akisubiri wateja, lakini pesa haikufuata jasho lake.
‎
‎Siku moja akiwa kwenye daladala, alisikia vijana wawili wakizungumza kwa furaha kuhusu jinsi walivyoongeza mauzo kwenye biashara zao kwa msaada wa kitabu kimoja kinachoitwa CHUO CHA MAUZO.
‎
‎Mmoja alisema:
‎
‎“Bila hiki kitabu, nisingejua kuwa neno dogo tu kama ‘Habari Njema’ linaweza kuvutia mteja kuliko punguzo.”
‎
‎Samson alishtuka. Kitabu? Mauzo? Hayo siyo mambo aliyowahi kuyapa uzito.
‎
‎Alikuwa akiamini kwamba mauzo yanakuja tu kama bahati au kwa kupumguza bei.
‎
‎“Nani ana muda wa kusoma vitabu?”
‎
‎ Alijiambia. “Mbona mimi nataka pesa sasa hivi, siyo masomo.”
‎
‎Lakini wiki hiyo hiyo alipoteza mteja mkubwa aliyekuwa tayari kununua mzigo wa laki mbili.
‎
‎Mteja alimwambia:
‎
‎“Samahani kaka, sikuhisi kama unajua unachouza.”
‎
‎Maneno hayo yalimchoma kama msumari wa moto.
‎
‎Samson alimkumbuka kijana mmoja anayeitwa Musa, aliyekuwa na duka jirani.
‎
‎Musa alikuwa na foleni ya wateja kila asubuhi.
‎
‎Akamwendea na kumuuliza:
‎
‎“Kaka, unatumia uchawi gani?”
‎
‎Musa alicheka na kumpa nakala ya kitabu cha CHUO CHA MAUZO.
‎
‎“Soma hiki. Hiki ndicho kilichonigeuza kutoka kuwa muuzaji hadi kuwa mshauri wa wateja.”
‎
‎Samson alianza kusoma. Kurasa ya kwanza akisema:
‎
‎“Wateja hawataki tu bidhaa, wanatafuta suluhisho.
‎
‎Ukiweza kuzungumza na hisia zao, utauza zaidi ya bidhaa utauza matumaini.”
‎
‎Alijifunza mbinu za kuuliza maswali sahihi, kutumia lugha ya kuhamasisha, kuandaa ofa za kuvutia, na kutengeneza uhusiano wa kudumu na wateja.
‎
‎Hakuona mabadiliko ya haraka.
‎
‎Ilibidi apambane na woga wa kuzungumza, kukumbana na wateja wagumu, na kuacha tabia ya kusema “Karibu kaka” bila maana.
‎
‎Lakini siku moja, mteja mpya alikuja na Samson alitumia mojawapo ya mbinu kutoka kitabu kile.
‎
‎Badala ya kuuliza “Unataka kitenge gani?”
‎Aliuliza:
‎
‎“Unatafuta kitenge kwa ajili ya kukivaa kwenye hafla ya aina gani?”
‎
‎Mteja alitabasamu.
‎
‎“Kwa harusi ya mdogo wangu. Wewe ni tofauti.”
‎
‎Akanunua vitambaa vitatu bila kuomba punguzo.
‎
‎Miezi mitatu baadaye, Samson alikuwa tayari kuongeza duka la pili. Lakini janga lilitokea:
‎
‎Ghafla washindani walitoa bei za chini sana sokoni.
‎
‎Wateja wengi walienda kwao. Samson akakaribia kukata tamaa.
‎
‎Lakini alifungua tena kurasa za mwisho za CHUO CHA MAUZO na kukumbushwa:
‎
‎“Unaposhindwa kuuza kwa bei, uza kwa thamani.”
‎
‎Akaanza kuongeza huduma ya kufungasha zawadi, kutoa ushauri wa mitindo kwa wateja, na kutuma ujumbe wa shukrani kwa kila mteja aliyenunua.
‎
‎Sasa Samson hakuwa tu muuzaji wa vitenge alikuwa mshauri wa mavazi ya hafla.
‎
‎Biashara yake ilikua kwa kasi ya ajabu.
‎
‎Mapato yake yakaongezeka MARA MBILI ndani ya miezi sita.
‎
‎Samson alianza kushiriki mafunzo kwa wafanyabiashara wengine wadogo.
‎
‎Akawaambia:
‎
‎“Siri haipo kwenye bidhaa, ipo kwenye akili yako na akili inachochewa na maarifa.
‎
‎Na maarifa haya niliyapata kwenye kitabu cha CHUO CHA MAUZO.”
‎
‎Leo hii, Samson ni mfanyabiashara mkubwa, ana wafanyakazi, duka la mtandaoni, na anaandaliwa kuhudhuria semina ya kimataifa.
‎
‎Yote yalianza pale alipoamua kuchukua kitabu na kukisoma.
‎
‎Kama wewe ni mfanyabiashara na unajiuliza “Nifanye nini ili niuze zaidi?”
‎
‎Jibu linaweza kuwa si bidhaa mpya, si duka kubwa zaidi bali ni maarifa mapya.
‎
‎👉 Chukua kitabu cha CHUO CHA MAUZO leo.
‎
‎👉 Geuza biashara yako kuwa shujaa wa sokoni.
‎
‎Anyway, kama bado hujapata kitabu hiki, unaweza kuweka oda yako hapa 👇
‎
‎https://wa.link/6pruxn
‎
‎Karibu.
‎0756694090.
‎
‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
‎
‎Ramadhani Amir
‎
‎