
Rafiki yangu mpendwa,
Leo nina taarifa njema sana kwako, taarifa za tukio kubwa ambalo huwa linatokea mara moja tu kila mwaka.
Tukio hilo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jukwaa la kukutana watu wenye kiu ya mafanikio makubwa na wanaoyapambania bila kukata tamaa.
Mwaka huu 2025, tunakwenda kuwa na semina hii kwa mwaka wa 10 mfululizo, na pia ndiyo itakuwa semina ya mwisho kabisa.
Sababu za kwa nini ni ya mwisho na nini kitakachofuata, utazipata utakaposhiriki semina.
Hii siyo fursa ya kukosa, kama umewahi kushiriki semina hizi huko nyuma, unajua thamani yake.
Karibu mwaka huu 2025 upate thamani kubwa zaidi, lakini pia ukutane na wengine ambao wamekuwa wakishiriki.
Kama hujawahi kushiriki SEMINA ZA KISIMA CHA MAARIFA, hii ndiyo nafasi yako ya kipekee ya kutimiza hilo.
Kwani ukiikosa nafasi hii, hutaweza kuipata tena.
Karibu ushiriki na utayabadili kabisa maisha yako.
Kitu kimoja zaidi ni kwamba SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2025 itafanyika Zanzibar,
…hii ikiwa ndiyo mara ya kwanza na pekee ya semina hii kufanyika nje ya Tanzania Bara.
Tumeifanya semina hii Dar, Dodoma, Arusha na Mbeya.
Kwa awamu hii ya mwisho, tunayavuka maji na kwenda Zanzibar, tena semina itafanyika pembeni ya ufukwe wa bahari.
Hivyo siyo tu tutapata mafunzo, bali pia tutapata mapunziko mazuri sana. Usikubali kukosa semina hii ya kumi na ya mwisho kabisa.
Nichukue nafasi hii kukukaribisha sana wewe rafiki yangu kwenye semina hii, karibu uungane na wanamafanikio wenye kiu kubwa.
Karibu pia ujue ngwe inayofuata baada ya kuhitimisha semina hii.
Kwani safari ya Ubilionea ni lazima ifikiwe, na kila aliyedhamiria.
Taarifa kamili za SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2025 zipo hapo chini, zisome kwa kina na chukua hatua mara moja.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2025
Kauli mbiu:
“Jifunze, Jipange, Tekeleza: Jenga Maisha na Biashara Yenye Thamani na Uhuru wa Kifedha”
📍 Mahali: Zanzibar Ocean View Hotel
📅 Tarehe: Ijumaa 10 Oktoba – Jumatatu 13 Oktoba 2025
💎 LENGO LA SEMINA
✅ Kukuwezesha kuboresha biashara yako ili ikue haraka na kuwa endelevu, na kufikia thamani ya dola bilioni 1.
✅ Kukupa mfumo wa usimamizi wa fedha binafsi ili ujenge utajiri na kufikia uhuru wa kifedha.
✅ Kukupa mpango wa utekelezaji wa hatua kwa hatua utakaoanza kuufanyia kazi mara moja.
✅ Kukuunganisha na watu wanaofanana na wewe kwa mitandao ya ukuaji.
✅ Kupata mapumziko pamoja na utalii wa Zanzibar huku ukijifunza.
📅 RATIBA KAMILI YA SEMINA
🗓️ Ijumaa 10 Oktoba 2025
✅ Check-in Zanzibar Ocean View Hotel kuanzia saa 8:00 mchana.
✅ Mapokezi na utambulisho wa washiriki jioni.
✅ Chakula cha usiku na mijadala ya kujenga mtandao.
🗓️ Jumamosi 11 Oktoba 2025: Mafunzo ya BILIONEA MAFUNZONI
Mada:
“Jinsi ya Kujenga Biashara Yenye Kukua Haraka na kufikia thamani ya Zaidi ya dola bilioni 1.”
1️⃣ Kipindi 1: Kujenga Bidhaa/Huduma Inayokabiliana na ushindani Sokoni
• Tambua tatizo la mteja na utengeneze bidhaa bora.
• Unda mfumo rahisi wa masoko unaovutia wateja bila gharama kubwa.
• Mpango wa utekelezaji wa kuboresha au kuunda bidhaa yako.
2️⃣ Kipindi 2: Mauzo na Huduma kwa Wateja kwa Ukuaji wa Haraka
• Mfumo wa mauzo unaofanya kazi na maneno sahihi ya kuuza.
• Huduma bora inayowafanya wateja warudi mara kwa mara.
• Mpango wa mfumo wa mauzo na huduma.
3️⃣ Kipindi 3: Fedha na Timu Imara
• Usimamizi wa fedha kwa ukuaji na kuandaa bajeti rahisi.
• Kuajiri na kukuza timu bila kuongeza gharama kubwa.
• Mpango wa fedha na mpango wa timu.
4️⃣ Kipindi 4: Uongozi, Teknolojia, Mitandao na Urithi
• Nidhamu na mindset ya ushindi ya uongozi.
• Kutumia teknolojia kuongeza ufanisi.
• Kujenga mtandao na kuandaa urithi wa biashara yako.
• Mpango wa kila kipengele kwenda kufanyia kazi.
🗓️ Jumapili 12 Oktoba 2025: Mafunzo ya NGUVU YA BUKU
Mada:
“Vunja Laana Ya Umasikini, Jenga Utajiri Wa Vizazi.”
1️⃣ Kipindi 1: Kuongeza Mapato
• Njia za kuongeza kipato na kujenga vyanzo vingi vya mapato.
• Mpango wa kuongeza kipato ndani ya siku 30.
2️⃣ Kipindi 2: Bajeti, Akiba na Matumizi Bora
• Kuandaa bajeti rahisi na kuishi ndani ya kipato.
• Mbinu za kuweka akiba bila kujisikia kubana.
• Kupunguza matumizi yasiyo lazima bila kuharibu maisha.
• Mpango wa bajeti na akiba.
3️⃣ Kipindi 3: Usimamizi wa Madeni na Kutoa
• Kutoka kwenye madeni hatua kwa hatua.
• Udhibiti wa mikopo na kutoa kwa jamii huku unakua kifedha.
• Mpango wa kulipa madeni na kutoa.
4️⃣ Kipindi 4: Uwekezaji na Ulinzi wa Utajiri
• Utangulizi wa kuwekeza kwa uelewa na kidogo ulichonacho.
• Jinsi ya kulinda mali zako kwa bima na mfumo wa kisheria.
• Mpango wa uwekezaji na ulinzi wa utajiri.
🗓️ Jumatatu 13 Oktoba 2025: Ziara ya Utalii
Ziara ya Pamoja: City Tour, Prison Island & Nakupenda Sandbank
✅ Ziara ya Prison Island (kuona kasa wakubwa, historia ya gereza na kisiwa).
✅ Ziara ya Nakupenda Sandbank kwa kupumzika na kuogelea kwenye mchanga wa bahari ya bluu.
✅ City Tour ya Zanzibar (Stone Town, Forodhani, masoko ya spice na maeneo muhimu ya kihistoria).
✅ Transfer, Guide, Soft drinks, Chakula cha mchana (seafood), Boat na entrance fees zote.
💰 GHARAMA ZA KUSHIRIKI
✅ Mtu mmoja: Tsh 880,000/=
✅ Wawili (chumba kimoja): Tsh 1,550,000 (Tsh 775,000 kwa kila mmoja)
🎯 OFA YA MALIPO YA MAPEMA
✅ Mpaka 01/09/2025:
• Mtu mmoja: Tsh 780,000
• Wawili: Tsh 1,350,000 (Tsh 675,000 kwa kila mmoja)
🔖 JINSI YA KUJISAJILI
✅ Thibitisha nafasi yako kwa kulipa Tsh 100,000 kabla ya tarehe 31/07/2025.
✅ Malipo yote yakamilike kabla ya tarehe 06/10/2025.
ADA INAJUMUISHA:
✅ Malazi na chakula kamili (breakfast, lunch na dinner) ndani ya Zanzibar Ocean View Hotel (siku 3).
✅ Vipindi vyote vya mafunzo ya semina kwa siku 2, Jumamosi na Jumapili.
✅ Ziara ya utalii Zanzibar siku ya Jumatatu.
✅ Mwongozo (Guide) na viingilio kwenye maeneo ya utalii.
KWA NINI USIKOSE?
✅ Utatoka na mpango kamili wa biashara na fedha binafsi wa kwenda kufanyia kazi mara moja.
✅ Utapumzika na kupata nguvu mpya Zanzibar.
✅ Utajenga mtandao wa watu wenye malengo kama yako.
✅ Utapata uelewa wa kina na hatua za utekelezaji kutoka kwa wakufunzi wenye matokeo.
Kuwahi kuthibitisha nafasi yako, ingia hapa 👇
https://wa.link/a5u2kf
🌟 Usikubali nafasi hii ya mwisho ikupite chukua hatua sasa, jiandikishe leo, na anza safari ya kubadilisha biashara na maisha yako milele!