
Rafiki Yangu,
Kuna kipindi unajikuta unaumia sana…
Si mwili, bali moyo.
Umeamini mtu, akakusaliti.
Umejitahidi, ukaanguka.
Umeweka juhudi, matokeo hayaji.
Na hapo ndipo wengi hukosea, wanaruhusu maumivu yawatawale.
Wanakuwa wagumu, wanajifungia, wanakata tamaa.
Wanajidanganya kwamba sina tena bahati, au labda si mimi.
Lakini ukweli ni huu maumivu si adui wako, ni mwalimu wako.
Yanakuja kukuonyesha sehemu unayopaswa kukua.
Kila maumivu yana ujumbe.
Yanakuambia, hapo ulikuwa hujajua,
Yanakuambia, hapo unahitaji kubadilika.
Lakini wengi wanayakimbia badala ya kuyasikiliza.
Unapokimbia maumivu, unajinyima maarifa.
Unapokubali kukaa nayo, unaanza kujijua.
Unagundua nguvu zako halisi zipo ndani sio nje.
Sasa ngoja nikuambie kitu cha kweli kabisa…
Hakuna mtu aliyefanikiwa bila kuumia.
Kila mtu aliyejenga mafanikio makubwa, aliwahi kulia usiku mmoja.
Lakini hawakulia bure. Walilia, kisha wakajifunza.
Na wakatoka wakiwa wamesoma somo ambalo vitabu havifundishi, somo la maisha.
Nilimkuta kijana mmoja Arusha, alikuwa na duka dogo la nguo.
Akaibiwa mzigo wake wote usiku mmoja.
Wiki nzima alikuwa amepotea, hana raha.
Nilipokutana naye, nikamwambia, Usiruhusu maumivu haya yakutawale yafanye yakufundishe.
Akanitazama akaniambia, Lakini nimeumia sana.
Nikajibu, “Ndiyo, ila ndani ya maumivu hayo kuna siri ya mwelekeo mpya.*
Baada ya miezi mitatu, akafungua duka jipya, safari hii akaweka mfumo wa usalama, akaanza kuuza online.
Leo, ananiambia, Kama nisingeibiwa, nisingejua kuwa nilikuwa najibana.
Hapo ndipo nilielewa kabisa, maumivu ni zawadi iliyofungwa kwa karatasi ya mateso.
Ni somo linalokuandaa kuwa toleo jipya la wewe bora zaidi.
Kama kuna kitu kimekukwaza leo, usikimbie.
Kaa nacho, uliza somo lake ni lipi.
Maisha hayakupi adhabu, yanakupa mafunzo.
Tatizo ni sisi, tunatazama maumivu kwa macho ya huzuni badala ya macho ya uelewa.
Wacha maumivu yakufundishe nidhamu, ujasiri, na upendo wa kweli.
Lakini kamwe usiyape ruhusa yakutawale, maana yakikutawala yanafunga milango ya fursa zako.
Unapojifunza kuvumilia, unaanza kuelewa falsafa ya ndani ya ustoa.
Ustoa ni kujitawala.
Ni kuamua kwamba mimi si rahisi kuvunjika.
Ni kuelewa kwamba dunia haina huruma, lakini wewe unaweza kujitawala ili uishi kwa amani ndani ya machungu.
Watu wengi leo wanaishi wakiwa mateka wa yaliyopita.
Wamefungwa na majeraha ya zamani.
Wanabeba hasira, chuki, na majuto.
Lakini mtu mwenye hekima anajua: kupona ni uamuzi, si bahati.
Uamuzi wa kusema, Sitanung’unika tena, nitajifunza.
Kila wakati unapojikuta umepigwa chini, kumbuka sio mwisho wako, ni mwanzo wa somo jipya.
Maumivu yanakutaka utoke pale ulipo.
Yanataka uamke.
Yanataka ukubali kuwa safari ya ukuaji haianzi na furaha, huanza na maumivu.
Wacha yakufundishe uvumilivu, nidhamu, na ustahimilivu.
Lakini usiyape nguvu ya kukuongoza, maana yakikupata, yanakufanya uwe mwepesi kukata tamaa, kulalamika, na kulaumu.
Wewe sio mwathirika, wewe ni mwanafunzi wa maisha.
Na kama unataka kujifunza zaidi namna ya kujitawala, kuishi kwa amani hata katikati ya maumivu, basi soma kitabu FALSAFA YA USTOA.
Ndani yake utajifunza namna ya kutawala hisia zako, kupunguza machungu, na kuendelea mbele ukiwa na utulivu wa ndani.
Kama unataka kuishi maisha ambayo maumivu yanakuwa walimu wako, sio mabwana wako,
… basi kitabu hiki ni cha lazima kwako.
Wacha maumivu yakufundishe, usiyape ruhusa yakutawale.
Soma FALSAFA YA USTOA leo, na jifunze sanaa ya kujitawala ili uitawale dunia.
Hiki hapa 👇
https://wa.link/524kl0
Karibu.
0756694090.