
Hii Ndio Siri Ya Watu Wenye Utulivu Wa Ajabu!
Watu Wachache Wanaijua, Lakini Inawafanya Waishi Maisha Yasiyotikisika
Rafiki Yangu,
Kuna watu wanapitia changamoto kubwa…
Lakini bado wanatabasamu.
Hawakimbii.
Hawapigi kelele.
Wanakaa kimya, wanatulia, wanatafakari.
Unashangaa, Anawezaje kuwa mtulivu wakati mambo yameharibika hivi?
Wakati wengine wanapoteza mwelekeo,
wengine wanabaki imara kama mwamba.
Siri yao ni moja tu..
Wamejifunza kutawala akili zao.
Si kwa sababu maisha yao ni rahisi
bali wameamua kuwa watulivu hata wakati dunia inawapigia kelele.
Utulivu hauji kwa bahati.
Ni maamuzi ya ndani.
Ni nidhamu ya akili.
Ni ujuzi wa kujitawala.
Lakini wengi wanashindwa hilo.
Wanakasirika haraka.
Wanachoka mapema.
Wanavunjika moyo kwa jambo dogo.
Wanakuwa watumwa wa hisia zao.
Kuna watu wanaamka na furaha asubuhi,
lakini saa tatu tu wanakuwa wameshajaa hasira.
Kila kitu kinawakasirisha.
Kila mtu anawaudhi.
Na mwisho wa siku,
wanajiona wamechoka, wamepotea, wamevunjika ndani.
Maisha yao ni kama redio yenye kelele.
Hawatulii.
Hawana amani.
Hiyo ndiyo sababu watu wengi hawafiki walikopanga.
Sio kwa sababu hawana maarifa,
bali kwa sababu hawajui utulivu wa ndani unavyofanya akili ifanye kazi vizuri.
Usidanganywe na mawazo ya mitaani.
Eti mtu mtulivu ni dhaifu.
Eti kukaa kimya ni kuogopa.
Hapana!
Utulivu ni nguvu.
Kimya ni silaha.
Mtu mwenye utulivu anaona mbali kuliko wenye kelele.
Watu wengi wanadhani nguvu ni kupiga kelele,
kuonesha hasira, au kushindana na kila mtu.
Lakini ukweli ni kwamba…
nguvu ya kweli ni kujua lini usiseme kitu.
Ni kujua namna ya kufikiri kabla ya kutenda.
Mtu mwenye utulivu hajali nani anamchokoza.
Anajua thamani ya amani yake ya ndani.
Sasa hebu jiulize,
unawezaje kuwa na utulivu huo wa ajabu?
Kwanza, anza kujijua.
Tambua kinachokukasirisha, kinachokuvunja moyo, kinachokukengeusha.
Ukishakijua, unakimilikisha.
Pili, jifunze kukaa kimya.
Wakati unahisi unataka kujibu haraka kaa kimya.
Wakati unahisi unataka kulipiza kisasi tulia.
Hapo ndipo nguvu inaanza kukua.
Tatu, fanya maamuzi ukiwa umetulia.
Hasira, huzuni, au hofu hazina uwezo wa kuona mbali.
Lakini akili iliyotulia inaona fursa hata katikati ya giza.
Utulivu ni kama macho ya ndani.
Unapoona wazi, unaishi vizuri.
Namkumbuka rafiki yangu mmoja, Said,
alikuwa anapoteza mteja mkubwa kila alipokasirika.
Kila mara akihisi kudharauliwa, anajibu kwa ukali.
Na mwisho wa siku, anajikuta ameharibu dili.
Siku moja aliniambia,
Bro Rama, nimechoka kuharibu kila kitu kwa hasira zangu.
Tukakaa, nikamfundisha kitu kimoja…
Tulia kwanza. Hasira zikipita, ndipo utajua cha kusema.
Akanisikiliza.
Miezi michache baadaye, akanipigia simu.
“Bro, kile ulichoniambia kimeniokoa.
Nilipotulia, niliweza kusaini mkataba ambao nilikuwa nakaribia kuharibu.
Sasa najua, utulivu ni nguvu kuliko maneno.
Leo, Said ni mmoja wa watu wanaoheshimika kazini kwake.
Watu wanamwambia, Bro, una utulivu wa ajabu!
Anacheka tu, anajua siri yake ni moja alijifunza kujitawala.
Rafiki yangu,
usitafute utulivu kwa kutoroka matatizo.
Tafuta utulivu kwa kujijua.
Kwa kuutawala moyo wako.
Kwa kuamua kuwa imara hata wakati mambo ni magumu.
Hiyo ndio siri ya watu wenye utulivu wa ajabu.
Wamejifunza kwamba nguvu ya kweli haiko kwenye misuli,
bali iko kwenye akili tulivu.
Kwa sababu mtu mwenye utulivu wa ndani,
anaweza kushinda vita yoyote ya nje.
Anyway kujifunza zaidi,
Soma kitabu hiki kipya cha
FALSAFA YA USTOA
Kitabu hiki kinakufundisha siri ya kutawala akili yako,
kutuliza moyo wako,
na kuishi maisha yenye amani hata katikati ya kelele za dunia.
Kupata kitabu hiki bonyeza hapa 👇
https://wa.link/524kl0
Karibu.
0756694090.
PS: Utulivu Ni Nguvu. Jifunze Kuimiliki Leo.