
Watu Wachache Wanaielewa, Lakini Inawapa Maisha Yenye Amani na Mwelekeo
Rafiki Yangu,
Kuna watu wanapitia changamoto kila siku…
Lakini bado wako cool.
Wana utulivu.
Wanafanya maamuzi kwa akili, si kwa hofu.
Wakati wengine wanapotea kwa presha,
wao wanatulia, wanapumua, na kufikiri.
Unashangaa, Wanafanyaje?
Kwa sababu kila kukicha dunia inawapigia kelele,
mambo yanagoma, presha zinapanda,
lakini bado hawaonekani kuchanganyikiwa.
Siri yao ni moja wanafahamu sayansi ya akili tulivu.
Wamejifunza namna ya kuishi bila kuruhusu kila kitu kuvuruga ndani yao.
Lakini ukweli ni kwamba wengi wetu hatujui siri hiyo.
Tunachanganyikiwa haraka.
Tunapoteza mwelekeo kwa jambo dogo.
Simu ikilia vibaya, moyo unadunda.
Ujumbe mmoja tu unaharibu siku nzima.
Unajikuta unaamka na amani,
lakini jioni unakosa hata pumzi.
Kila kitu kinakuuma.
Kila mtu anakukasirisha.
Kila tukio linakupeleka mbali na utulivu wako.
Unalalamika, unaumia, unachoka.
Unahisi dunia inakukaba.
Lakini ukweli ni huu dunia haitakoma kuwa na misukosuko.
Ila wewe unaweza kujifunza kuishi bila kuchanganyikiwa hata katikati ya kelele hizo.
Usiweke imani kubwa sana kwenye wazo la nitakuwa na amani nikishafanikiwa.
Hapana.
Amani ya kweli haianzii nje.
Inaaanzia ndani.
Watu wengi wanadhani utulivu ni matokeo ya maisha mazuri,
lakini kiukweli maisha mazuri ni matokeo ya utulivu.
Kama akili yako haijatulia,
hata ukipata pesa, utaumia.
Hata ukipata mafanikio, hutayaona.
Hata ukipata mapenzi, utakosa furaha.
Hii ndio sababu wengine wana kila kitu,
lakini bado wanaishi kama wamechanganyikiwa.
Sayansi ya kuishi bila kuchanganyikiwa inajengwa hatua kwa hatua.
Kwanza:
Jifunze kujisikiliza ndani yako.
Usikimbilie kujibu tafuta utulivu.
Wakati mambo yanaenda mrama, kaa kimya kidogo.
Acha akili yako ipumue.
Pili:
Jifunze kutenganisha tatizo na hisia zako.
Siyo kila unachohisi ndicho ukweli.
Wakati mwingine akili yako inahitaji muda wa kufikiri kabla ya kuchukua hatua.
Tatu:
Kumbuka si kila kitu kinahitaji majibu yako mara moja.
Wakati mwingine, kimya chako ndicho jibu bora zaidi.
Ukijua haya,
unaacha kuchanganyikiwa kwa vitu vidogo.
Unaanza kuona mambo kwa uwazi.
Na unajifunza kwamba nguvu yako kubwa ipo kwenye utulivu wako wa ndani.
Namkumbuka jamaa mmoja anaitwa Kelvin.
Kila siku alikuwa na stress kazini.
Wafanyakazi wanamkwaza, boss anamlaumu, mteja analalamika.
Kila siku ni kelele kichwani.
Siku moja akaenda likizo ya wiki moja.
Akiwa huko, alikaa kimya.
Hakujibu simu.
Hakutuma meseji.
Akaanza kuandika hisia zake kila asubuhi.
Alipoendelea, akagundua kitu kimoja kikubwa:
Nilikuwa naumia si kwa sababu ya kazi, bali kwa sababu ya namna nilivyokuwa naifikiria.
Aliporudi, hakubadilisha kazi.
Lakini alibadilika yeye.
Akaanza kupanga siku zake vizuri,
akajifunza kusema hapana pale inapobidi,
na akaanza kuishi kwa utulivu.
Leo Kelvin ni mtu tofauti.
Wale waliokuwa wakimcheka kwa upole wake,
sasa wanamuuliza, Bro, unawezaje kubaki mtulivu hivi?
Rafiki yangu,
Kuishi bila kuchanganyikiwa si uchawi.
Ni sayansi.
Ni maamuzi.
Ni nidhamu ya akili.
Dunia haitapunguza kelele,
lakini unaweza kujifunza kusikia kimya chako ndani yake.
Na hapo ndipo nguvu ya kweli inapoanzia.
Usiruhusu mambo ya nje yakuvuruge.
Tawala akili yako, utatawala maisha yako.
Soma kitabu kipya cha
FALSAFA YA USTOA
Ujitawale Mwenyewe Kisha Uitawale Dunia.
Kitabu hiki kinakufundisha sayansi ya utulivu.
Namna ya kutumia akili yako kuishi bila kuchanganyikiwa,
…bila presha, na bila kupoteza amani yako ya ndani.
Anza leo kujenga akili isiyotikisika maisha yako yatabadilika milele.
Kukipata kitabu hiki, unaweza kubonyeza hapa 👇
https://wa.link/524kl0
Karibu.
0756694090.