
Rafiki Yangu,
Kuna kitu hatuambiwi mapema.
Kuna ukweli ambao wengi hawaujui…
Mpaka siku wanapopewa barua ya kustaafu.
Na huo ndio mchezo unaoua wastaafu wengi kimya kimya.
Tunaishi tukitegemea mshahara.
Tunafanya kazi miaka 20, 30, 40… bila kujenga kitu nje ya kazi.
Halafu tunategemea mafao yatusaidie mpaka uzee?
Haiwezekani.
Hakuna pesa ya mafao inayoweza kubeba mahitaji ya miaka 20–30 ya baada ya kazi.
Hilo ndilo somo ambalo hatufundishwi shuleni.
Na tatizo halipo tu kwenye pesa… lipo pia kwenye tabia.
Unapopata mafao, ghafla unahisi wewe ni tajiri.
Unaanza kugawa, kusaidia kila mtu, kununua vitu ambavyo hukuwahi kumiliki.
Unataka kufidia miaka yote ya kunyimwa na mfumo.
Na hapo ndipo mzizi wa kufilisika unaanza.
Lakini subiri…
Ushasikia hii kauli?
Maisha ya uzeeni ni matokeo ya maamuzi ya ujana.
Hii si methali tu.
Ni ukweli mchungu.
Fikiria hivi…
Umezoea kupokea pesa kila mwezi.
Ghafla, hakuna tena.
Lakini gharama zinaendelea.
Watoto bado wanasoma.
Afya inaanza kuzingua.
Umeme, maji, kodi, chakula… hakuna anayekuonea huruma.
Kila wiki kuna msiba, harusi, michango.
Kila mmoja anakutazama kama “mzee aliyejenga maisha vizuri”.
Lakini moyoni?
Unapiga hesabu.
Unatetemeka.
Pesa inaisha.
Muda unakwenda.
Na hakuna chanzo kingine cha kuingiza kipato.
Hapo ndipo wengi wanachoka.
Wengi wanauza viwanja.
Wengine wanauza nyumba.
Wengine wanahamia kijijini kulikokuwa kwa bei ndogo.
Wengi wanaanza kuishi kama mzigo kwa watoto wao.
Si kwamba hawakufanya kazi.
Walifanya.
Walijituma.
Lakini hawakupanga mapema.
Walikosa msingi wa uwekezaji.
Kustaafu si tatizo.
Kutokuwa na mpango wa uwekezaji ndio tatizo.
Hakuna pesa itakayodumu bila mfumo.
Hakuna mafao yatakayotosha bila mpango.
Na hakuna mpango utakaa bila maarifa.
Uwekezaji si juu ya pesa nyingi.
Ni juu ya uelewa.
Ni juu ya kujua wapi uweke, lini uweke, na jinsi ya kukua.
Na hii ndiyo sehemu wengi wanakosea.
Wanataka kuanza na milioni 10.
Wanataka fursa kubwa.
Wanangoja mpaka maisha yachanganye.
Wanangoja mpaka wanazeeka.
Na mchezo unaishia hapo…
Na suluhisho ni mojawapo ya vitu rahisi kuliko unavyofikiri:
Jenga mfumo wa uwekezaji mapema.
Mfumo unaokuwezesha:
Kuongeza kipato.
Kuanzisha chanzo cha ziada.
Kuzalisha pesa ukiwa bado una nguvu.
Kufika uzee ukiwa na uhuru, sio mzigo.
Na sio lazima kuanza na pesa nyingi.
Kilicho muhimu ni maarifa.
Unachohitaji ni kuelewa misingi ya uwekezaji…
Misingi ambayo shule hazifundishi.
Waajiri hawasemi.
Na wastaafu wengi wanaigundua pale ambapo wamechelewa.
Hii ndiyo sababu kitabu cha*ELIMU YA MSINGI YA UWEKEZAJI * kimetengenezwa.
Kinafundisha kwa lugha rahisi.
Kwa mifano halisi.
Kwa hatua unazoweza kuanza nazo leo.
Kabla hujachelewa.
Kabla maisha hayajakubana.
Kuna mzee mmoja jirani yangu…
Alifanya kazi serikalini karibu miaka 33.
Kila mtu aliamini mzee yuko vizuri.
Siku alipostaafu, alilipwa mafao mazuri tu.
Mji mzima ulijaa shangwe.
Mzee alifanya sherehe, akagawana, akasaidia ndugu, akaboresha nyumba.
Lakini baada ya mwaka mmoja…
Kilianza kimya kimya.
Mfuko ukaanza kubanuka.
Gharama za afya zikaongezeka.
Watoto bado wanahitaji msaada.
Na hakuna chanzo kingine cha kipato.
Alinong’oneza siku moja:
Kama ningejua… ningejenga mpango wangu mapema. Sasa nimechelewa.
Maneno yake yalinikata kama kisu.
Na sikutaka mtu mwingine ayapitie hayo machungu.
Ndiyo maana najituma kukupa haya maarifa leo.
MWISHO… KAMA UNA HURUMA NA KESHO YAKO, HII NDIO NAFASI YAKO
Kesho haiji kwa bahati.
Kesho inajengwa.
Leo.
Kwa hatua ndogo.
Kwa maarifa sahihi.
Na kitabu kimoja kinaweza kubadili mustakabali wako mzima.
Na kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA UWEKEZAJI ndicho ramani ya kujitoa kwenye hatari ya kufilisika baada ya kustaafu.
Usisubiri mpaka uchelewe kama wengine.
Anza leo.
Jiokoe leo.
Kama bado hujakipata unaweza kuanzia hapa 👇
https://wa.link/kj1hrl
Karibu.
0756694090.
Kutoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhan Amir.