Jumapili ya kesho tarehe 13/04/2014 nitakuwepo kwenye kipindi cha AMKA NA BADILIKA kinachoendeshwa na kampuni ya COSNET. Kipindi hiki kinarushwa kupitia televisheni ya taifa TBC1 kila jumapili saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Katika kipindi cha kesho mimi ndiye nitakuwa mgeni ambapo nitaelezea historia fupi ya wapi ninapotoka na wapi ninapokwenda. Nitaelezea baadhi ya malengo makubwa niliyowahi kujiwekea na nikayatimiza na pia nitaelezea changamoto kubwa nilizokutana nazo kwenye maisha yangu.
Nitaeleza njia ambazo kijana yeyote wa kitanzania anaweza kuzitumia kuyapanga maisha yake na kufikia malengo aliyojiwekea. Pia nitazungumzia njia ya kuweza kukuza mitaji kwa watu ambao wanatamani kufanya biashara ila mtaji ni tatizo kwao.
Angalia kipindi hiki uweze kujifunza na kuhamasika kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kumbuka wewe ndiye dereva wa maisha yako. Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote unalofanya ni lazima uchukue jukumu la kuendesha maisha yako. Ufanye kazi kwa bidii, ujifunze kila siku na uache kutegemea misaada au kulalamika.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako nzuri ya maisha.
Kumbuka tuko pamoja katika safari hii, na nina hakika tutafika kule tunalikopanga kufika.
Ni jambo jema&zuri pia inaleta hamasa kuona vijana kama wewe kutumia muda vizuri kwa ajili ya maendeleo!!
Tunahamasika, endelea kuwa na moyo huo!
LikeLike
Very good motivation Dr to be Mr Aman Makirita
I've watched tha amka na badilika hosted by Mtsimbe..keep it up!
LikeLike
Amani, nimekusikiliza Sana na nimekuelewa. Or good.
LikeLike
Great thinker.
LikeLike
Keep it up aman! Good work.
LikeLike
nimekipenda kipindi. all the best to your plan bro
LikeLike
show nzuri amani! nimeipenda na confidence uliyoonyesha
LikeLike
Hongera sana Amani Mungu akubariki sana
LikeLike
Hongera sana Amani Mungu akubariki sana.
LikeLike
all the best bro
LikeLike
kk naomba km una video ya hiyo interview unitumie nilimiss hicho kipindi
LikeLike
Asante sana Franco.
TUKO PAMOJA.
LikeLike
Asante sana Brock.
TUKO PAMOJA.
LikeLike
Habari Innocent,
Samahani video haipo kwenye hali ambayo inafaa kutumwa.
Karibu sana.
LikeLike