Jumapili ya kesho tarehe 13/04/2014 nitakuwepo kwenye kipindi cha AMKA NA BADILIKA kinachoendeshwa na kampuni ya COSNET. Kipindi hiki kinarushwa kupitia televisheni ya taifa TBC1 kila jumapili saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Amka na badilika

  Katika kipindi cha kesho mimi ndiye nitakuwa mgeni ambapo nitaelezea historia fupi ya wapi ninapotoka na wapi ninapokwenda. Nitaelezea baadhi ya malengo makubwa niliyowahi kujiwekea na nikayatimiza na pia nitaelezea changamoto kubwa nilizokutana nazo kwenye maisha yangu.

  Nitaeleza njia ambazo kijana yeyote wa kitanzania anaweza kuzitumia kuyapanga maisha yake na kufikia malengo aliyojiwekea. Pia nitazungumzia njia ya kuweza kukuza mitaji kwa watu ambao wanatamani kufanya biashara ila mtaji ni tatizo kwao.

  Angalia kipindi hiki uweze kujifunza na kuhamasika kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kumbuka wewe ndiye dereva wa maisha yako. Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote unalofanya ni lazima uchukue jukumu la kuendesha maisha yako. Ufanye kazi kwa bidii, ujifunze kila siku na uache kutegemea misaada au kulalamika.

  Nakutakia kila la kheri katika safari yako nzuri ya maisha.

Kumbuka tuko pamoja katika safari hii, na nina hakika tutafika kule tunalikopanga kufika.