Kuna vitu vitatu muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kufikia mafanikio makubwa.

Vitu hivyo ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kuwa mwaminifu na kuwa muadilifu. Ukikosa kimoja kati ya vitu hivi vitatu ni sawa na jiko la mafiga matatu ambalo limekosa figa moja, haliwezi kupika. Ukikosa vyote vitatu ni sawa na kwamba huna maisha kabisa. Kama ilivyo kwenye jiko kama hakuna mafiga yote matatu hakuna jiko kabisa.

Tabia hizi tatu ndio zitakazokuwezesha kutoka popote ulipo, hata pangekuwa chini kiasi gani na kuweze kufikia mafanikio makubwa. Bila ya tabia hizi tatu utajaribu sana kufikia mafanikio lakini utashindwa. Unaweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ila kama umekosa uaminifu, hakuna mtu atakayetaka kufanya kazi na wewe. Unaweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na ukawa na uaminifu, ila kama umekosa uadilifu utajikuta kila siku unaingia kwenye matatizo.

Kutokana na umuhimu wa tabia hizi tatu katika kufikia mafanikio, tutazijadili moja baada ya nyingine hapa kwenye kipengele cha TABIA ZA MAFANIKIO kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Mwezi huu wa pili tutaanza kujijengea tabia ya UAMINIFU. Kwa mwezi mzima kila siku ya jumanne utapata makala itakayokuwezesha wewe kujijengea tabia hii muhimu ambayo itakuwezesha kufikia malengo yako na mafanikio makubwa.

Je inawezekana kujijengea tabia hii?

Swali muhimu ambalo watu wengi wanaweza kujiuliza ni je inawezekana kujijengea tabia hii? Watu wengi wanafikiri ukishakosa uaminifu na hasa unapokuwa mtu mzima ndio basi tena, ni vigumu kubadilika kwa sababu ndivyo maisha yako yalivyozoea.

Ukweli ni kwamba kitu chochote ambacho unakifanya sasa umejifunza hapa hapa duniani. Ni tabia chache sana ambazo mtu umezaliwa nazo, ila nyingine nyingi umejifunza kw akuchagua mwenyewe au kuiga wengine wanavyofanya kwenye jamii inayokuzunguka.

Haijalishi umekosa uaminifu kwa muda mrefu kiasi gani, unaweza kuanza kujifunza leo na ukaboresha maisha yako. Katika makala hizi za kujijengea tabia ya uaminifu tutakwenda hatua kwa hatua za jinsi ya kujijengea tabia hii. Kama utafuata maelekezo yote vizuri utakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kufikia mafanikio.

Kukosa uaminifu ni tatizo la kitaifa.

Kwa nchi yetu Tanzania, kukosa uaminifu ni tatizo la kitaifa. Wizi, ufisadi na hata mambo mengine mabaya yanayoendelea kwenye nchi hii yanatokana na kukosekana kwa uaminifu. Sasa hivi kila mtu anayepata nafasi yoyote anaangalia ni jinsi gani anaweza kupata zaidi ya alichopangiwa kupata. Ndio maana rushwa imekithiri, watu wanaiba fedha na mali za umma na tunaendelea kuwa masikini.

Kama tusipoweza kutatua tatizo hili la uaminifu, tutaendele akuwa masikini kama taifa. Hii ni kwa sababu asiye mwaminifu anaendelea kuwa masikini na anawasababisha wengine nao kuwa masikini.

Ni muhimu sana kila mtu kujijengea uaminifu.

Kwa nchi yetu Tanzania, kila mtu, namaanisha kila mtu anatakiw akujifunza jinsi ya kujijengea tabia ya uaminifu. Sisemi kwamba nchi nzima woote sio waaminifu, ila tuna watu wengi sana ambao sio waaminifu hivyo ni rahisi kuwaharibu wale ambao ni waaminifu. Kwa mfano kwenye eneo ambalo watu wamezoea kutoa rushwa, ukienda mtu ambaye hutoi rushwa unaonekana ni wa ajabu. Hii inaweza kumfanya mtu mwaminifu kutoa rushwa kwa sababu kila mtu anafanya hivyo.

Ni muhimu kila mtu kujifunza jinsi ya kujijengea tabia ya uaminifu, ili kama sio mwaminifu uwe mwaminifu na kama tayari ni muaminifu uimarishe uaminifu wako na kuwashawishi wanaokuzunguka nao wawe waaminifu.

Watu waliofanikiwa sio waaminifu, sio kweli.

Kitu cha mwisho ambacho nafikiri wengi watakuwa wanajiuliza kuhusu tabia hii ya uaminifu ni kwamba mbona watu waliofanikiwa sio waaminifu? Kuna habari nyingi ambazo huwa tunazipata kuhusu watu matajiri, utasikia huyu alifanya mambo fulani ambayo sio ya uaminifu ndio akapata utajiri. Utasikia mwingine amenyonya wafanyakazi, anaibia serikali, anakwepa kodi ndio maana amekuwa tajiri.

Kwanzia leo, kama kweli unataka kufikia mafanikio, futa mawazo haya hasi kwenye kichwa chako. Hakuna mtu aliyefanikiwa na akaendelea kukaa kwenye mafanikio hayo kwa muda mrefu kama sio mwaminifu. Mifano iko wazi, angalia viongozi wote wa kiserikali ambao wameiba mafedha mengi na wengine kwenda kuyaficha nje ya nchi kabisa. Mwisho wa siku mambo yamelipuka na ukweli umejulikana. Angalia majambazi ambao wamekuwa wakiiba fedha nyingi bila hata ya kukamatwa, unawez akujiuliza kwa nini watu hawa wasiache wizi baada ya kupata fedha nyingi na kufanya mambo mengine? Jibu ni rahisi, hawan atabia ya uaminifu, hivyo  hata akiacha wizi baada ya kupata fedha nyingi na kuingia kwenye biashara anaishia kupata hasara.

Leo nakupa siri moja kwa nini watu wengi wenye mafanikio wanajengewa picha kwamba ni watu ambao sio waaminifu. Mwandishi mmoja wa kimarekani aliwahi kuulizwa swali hilo, kwa nini nyie waandishi mmekuwa mkiwaandika watu wenye mafanikio kama watu ambao sio waaminifu. Kwa nini hata kwenye maigizo, watu matajiri wanaonekana kuwa na roho mbaya? Yeye alijibu; hivyo ndivyo jamii inavyopenda kuona, na sisi tunawapatia hicho hicho, pia watu matajiri ni rahisi kuwaandika vyovyote unavyotaka na usipate pingamizi. Ukianza kuwaandika watu masikini, wataleta malalamiko makubwa sana. Ila kwa kuwa matajiri hawana muda wa kufuatilia mambo madogo kama haya basi inakuwa rahisi kwetu.

Katika makala hizi za kujijengea tabia ya uaminifu tutajifunz amambo yafuatayo;

1. Maana ya uaminifu.

2. Jinsi ya kujijengea tabia ya uaminifu.

3. Jinsi ya kuepuka mazingira yanayokuondolea tabia ya uaminifu.

4. Uhusiano kati ya tabia ya uaminifu na mafanikio.

Kupata nafasi ya kujifunza jinsi ya kujijengea tabia hii ya uaminifu jiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga bonyeza haya maandishi ya neno KISIMA CHA MAARIFA kisha fuata maelekezo. Jaza fomu na kisha utume fedha ya uanachama kwenda namba 0717396253 au 0755953887 na utume jina au email uliyojiunga nayo. Kupata nafasi ya kujifunza kuhusu tabia za mafanikio na kujifunza ujasiriamali na biashara ada ni tsh elfu kumi kwa mwaka. Jiunge leo ili uweze kupata mafunzo bora yatakayokuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri kwenye kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani,

makirita@kisimacha maarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322