Unajua kwa nini watu wengi hawafurahii maisha?
Unajua kwa nini watu wengi wanaonekana kuweka juhudi sana kwenye kazi au biashara lakini bado wanaonekana kabisa hawayapendi maisha yao?
Ni kwa sababu hawapati muda wa kuishi maisha yao. Hawapati muda wa kuwa pale walipo. Kila mara wanafikiria kitakachotokea baada ya hapa.

Unakuwa na hamu ya chakula kitamu, labda hata unaenda hoteli nzuri ili kupata mapumziko na chakula, lakini wakati unakula, akili yako haipo pale kwenye kula. Akili yako unawaza kitakachotokea baada ya kula.
Unasubiria sherehe kwa shauku kubwa sana, labda ni mahafali, au labda ni harusi. Lakini hiyo siku ya sherehe yenyewe akili yako haipo pale, inafikiria kitakachotokea baada ya hiyo sherehe. Kama ni mahafali unafikiria je utapata kazi itakayokuridhisha, je maisha yatakwenda kama ulivyopanga? Kama ni harusi basi unafikiri je maisha yatakwenda vizuri kama mlivyopanga? Na mengine mengi.
SOMA; FAIDA ZA KUISHI LEO
Umekuwa hupati nafasi ya kufurahia chochote unachofanya kwa sababu unaruhusu akili yako ianze kuzurura huku na huko. Na ndio inakufikisha kwenye fikra ya nini kitatokea baada ya tukio hili la sasa kuishi.
Cha kushangaza hata unavyosoma hapa, unafikiria utafanya nini baada ya kumaliza kusoma, hivyo hufurahii wala kujifunz akwa undani na hivyo kuweza kubadili maisha yako.
Acha kujidhulumu maisha yako. Pale ulipo weka mawazo yako yote. Chochote unachofanya, weka mawazo yako yote pale. Hayo ndio maisha yako na ukiweza kufanya hivi utafurahia kila sekunde ya maisha yako.
Ila kama utaruhusu akili yako iruke ruke utajikuta hupati muda wa kufurahia maisha yako.
TAMKO LA LEO;
Najua nimekuwa nakosa nafasi ya kufurahia maisha yangu kwa sababu nimekuwa naruhusu akili yangu iruke huku na huko. Chochote ambacho nimekuwa nafanya, akili yangu imekuwa inafikiria ni nini kitatokea baadae badala ya kuwa pale na kufurahia kila sehemu ya kile ninachofanya. Kuanzia sasa, popote nitakapokuwa, chochote nitakachokuwa nafanya, akili yangu na mawazo yangu yote yatakuwa pale. Maisha ni yangu, nina kila haki ya kuyafurahia, kila sekunde ya maisha haya.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.