Kuna mtu ambaye ni mrefu kuliko wewe, au mfupi kuliko wewe au mzuri kuliko wewe.
Kuna mtu ambaye kazi yake au biashara yake ni bora kuliko yako.
Kuna mtu ambaye kipato chake ni kikubwa kuliko chako.
Au kama unatumia mitandao ya kijamii, kuna mtu ambaye ana marafiki wengi kwenye mitandao hii kuliko wewe.
Hatuna haja ya kuangalia mbali kuona watu hawa ambao wamekuzidi kwa kile ambacho unafanya.

Swali ni je, ulinganisho huu unaofanya ni sahihi kwako? Ni muhimu kwako kuweza kufanya kazi iliyo bora, kuishi maisha yaliyo bora?
Kuliko kupoteza muda wako kwa kujilinganisha na vitu ambavyo sio muhimu, ni bora ukajiuliza ni kipi muhimu kwako, kipi kinahitaji kubadilika, ni kipi kina thamani ya kufanyia kazi.
Achana na ulinganisho usio muhimu kwako. Ulinganisho muhimu kwako ni kujilinganisha kile unachofanya sasa na uwezo ulionao. Nyingine zote ni kelele.
Je unaweza kuachana na kelele hizi ili ufanye kile kilicho bora?
TAMKO LA LEO;
Najua nimekuwa napoteza muda wangu kujilinganisha na watu kwa vitu ambavyo sio muhimu kwangu. Kuanzia sasa nitaacha kupoteza muda wangu kujilinganisha kwa vitu ambavyo sio sahihi na nitawekeza nguvu zangu kwenye kuboresha kile ambacho ninafanya, kwa kuleta mabadiliko, kwa kukamilisha vilivyo muhimu.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.