Usifanye Kosa Hili Kubwa Ambalo Litaondoa Imani Kwa Wale Wanaokuamini Na Kukutegemea.

Habari za leo ndugu msomaji wangu wa makala hii, nina imani umeamka salama na unapenda kujifunza jambo jipya kuhusu maisha yako, hata kama kuna changamoto unayoipitia ya kukuumiza moyo wako/maisha yako bado nitasema umeamka salama ndio maana umepata nafasi/neema ya kufungua hapa na kusoma, tena unaenda kujifunza vitu vipya ama kuviboresha zaidi kama ulikuwa unavijua hapo kabla.
Mara nyingi mafanikio yetu ya hapa duniani husababishwa na jamii zetu zinazotuzunguka, kama wewe ni mfanyabiashara/mjasiriamali, asilimia kubwa ya biashara yako inategemea utoe huduma bora kwa jamii ndipo mafanikio yako yawe juu zaidi, vivyohivyo kwa viongozi wa dini hutegemea uaminifu na utiifu kwa wale wanaowaongoza ndipo Mungu huwainua zaidi na zaidi, na kuonekana wa muhimu sana katika kusanyiko wanaloliongoza/wanalolitumikia.

 
Inapotokea katika maisha yako ukaanza kujiendesha wewe mwenyewe kwa kujiheshimu na kuepuka vitu vibaya vinaomkosea Mungu na jamii kwa ujumla, na ukaonekana ni mtu wa kuigwa kwa maadili mema jinsi unavyoishi na unavyoonekana mwenye mafanikio ya kimwili na kiroho, wengi hupenda kukufuatilia na kujua umewezaje kufika hapo ulipo na ilikuwaje ukafanikiwa kushinda vikwazo vingi hapo nyuma. Kwa kuwa ni maisha yako na unajua ulipoanzia na ulipo si vigumu kumwelezea mtu umefanyaje mpaka kufika hapo ulipo.
SOMA; Mambo Matano(5) Muhimu Ya Kuzingatia Kwenye Malezi Ya Watoto Ili Kuwaandaa Kufikia Mafanikio.
Unapofikia kiwango hichi cha kuheshimiwa na wanadamu, na kukupa nafasi katika maisha yao kukusikiliza ama kutoa huduma kwao, usije ukafanya kosa la kujiinua kwao na kuanza kuwatishia kuwa isingekuwa wewe wasingefika hapo walipo… ni sawa kwa mawazo ya kibinadamu unaweza fikiri hivyo na ilikuwa ni mpango wako kujitoa kwao lakini jua mawazo ya Mungu si mawazo ya mwanadamu, unapoona una vitu vya ziada vya kujifunza kwa wengine na wao hawana elewa kwamba Mungu amewekeza jambo ndani yako la kuwainua wengine ambao bado hawajajitambua kwa nini walizaliwa waje waishi hapa duniani na kwa nini hawakufa miaka mingi iliyopita ila bado wapo na wanaishi, nini inawapasa kufanya japo wanaonekana wanaumizwa/kukata tamaa na vitu vingi, muda mwingine wanalala njaa, muda mwingine wanakosa huduma mhimu kama mavazi, tiba nk lakini pamoja na hayo yote wanayoyapitia bado wanaishi.
Unapogundua kuna kundi kubwa nyuma linakutazama wewe, usije ukabweteka na kuona hakuna kama wewe na wasikusumbue, na utafanya unavyotaka wewe na si wanavyotaka wao, nasema upo sahihi kabisa ila elewa si kila jambo unaweza fanya unavyojisikia wewe lazima kuna muda utege sikio uwasikie wanaokufanya uonekane wa tofauti wanasema nini, wanataka nini, na hawataki nini, baada hapo unachukua mawazo yao na unachanganya na mawazo yako ndipo unapata wazo sahihi ambalo litawafanya wote mwendelee kuona mwenzangu ni mhimu kwangu na mimi ni mhimu kwake.
SOMA; Kama Unataka Maisha Mazuri Shindana Na Mtu Huyu Mmoja Tu, Wengine Wote Achana Nao.
Ukijiona upo juu sana mwenye hawa walioko chini atawatumia kukushusha chini maana kama wataanza kukuona huna umhimu kwao tena, je utatoaje huduma kwao ambayo inakufanya uonekane upo juu?
Shukuru kwa kuwa umejua kwa nini ulipaswa kuishi, na ona mzigo ndani yako ya kuwasaidia na wengine wajue kwa nini wana haki ya kuwepo duniani na kuishi hapa duniani, ondoa roho ya uchoyo ya kutaka wewe uwe kama wewe tu na mwingine asijue, kumbuka haya sio maisha ya shuleni ambapo mwenzako alikuwa akitaka kujua kwa nini unafaulu sana upo tayari asijue chochote na wala akiomba kitabu kwako usimpe kabisa ukijua atakupita, ulikuwa sawa kwa wakati huo kwa sababu hukupata wa kukuambia kuwa hiyo sio sahihi ila kwa kuwa umekutana nami kwa njia ya makala hii nakwambia usifanye kosa hilo tena.

Nikutakie wakati mwema, endelea kufurahia kuja kwako duniani, endelea kutafuta kusudi lako la kuumbwa(kuzaliwa), endelea kuishi maisha yanayompendeza Mungu na wengine wanaokuzunguka utawapendeza pia na utawavuta zaidi waendelee kujifunza kutoka kwako.
Makala hii imeandikwa na Samson Ernest ambaye anapatikana facebook kwa jina hilo hilo pia waweza wasiliana naye kwa njia ya whatsApp 0759808081. ama kwa email; samsonaron0@gmail.com.
Asante.

2 thoughts on “Usifanye Kosa Hili Kubwa Ambalo Litaondoa Imani Kwa Wale Wanaokuamini Na Kukutegemea.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: