Inapokuja kwenye mipango yako ya maisha, tegemea mambo makubwa sana. Tegemea kufanya mambo makubwa ambayo yatabadili kabisa maisha yako. Tegemea kazi yako kuwa bora sana kiasi kwamba itaongeza thamani na kipato chako kitaongezeka pia. Tegemea kuwa na biashara kubwa ambayo itawasaidia watu wengi kutatua matatizo yao.

Vitu hivi viko ndani ya uwezo wako hivyo tegemea makubwa na jitoe kuweka juhudi kuhakikisha ya kwamba unavifikia vitu hivi.
Inapokuja kwenye mipango ambayo inawahusisha watu wengine, usitegemee chochote. Usiweke matumaini makubwa kutokana na ahadi ambazo amekupa mtu, usitegemee kwamba kwa kusema kitu basi atakitekeleza na maisha yako yatakuwa bora sana. Usitegemee chochote na hivyo chochote kitakachotokea kitakuwa ni bora kwako.
SOMA; Ni Ruhusa Kwako Kubadili Mawazo.
Unapoweka mategemeo yako makubwa kwa mtu utaishia kukatishwa tamaa na kuumizwa pia. Kwa sababu watu watakuambia kitu kingine na kufanya kitu kingine.
Kutokutegemea chochote kutoka kwa mtu haimaanishi utamwacha kila mtu afanye anavyojisikia. Utaendelea kumbana mtu atimize kile ambacho alikuahidi kufanya, ila tu wewe usiweke mipango yako mikubwa ya maisha kwa mategemeo ya kitu ambacho mtu amesema atafanya.
Watu wanabadilika, watu wanasahau, watu wanachelewa na mengine mengi ambayo yatakukwaza sana pale ambapo utakuwa umeweka mategemeo yako makubwa kwa mtu.
TAMKO LA LEO;
Katika mipango yangu binafsi, nitaweka mategemeo makubwa sana. Nitategemea makubwa kutoka kwenye kile ambacho ninafanya na nitatumia mategemeo haya kunisukuma ili niweze kupata kile ambacho ninakitaka kwenye maisha yangu. Katika mipango ambayo watu wengine wameniahidi, sitategemea chochote. Hii ni kwa sababu najua watu wanabadili mawazo, watu wanasahau na watu wanashindwa kuweka vipaumbele. Japo nitawabana wafanye kile walichoniahidi, lakini sitokubali mipango yangu ikwamishwe na mipango ya watu wengine.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.