Mbinu 4 Zitakazo Kuwezesha Kumudu Kufanya Mabadiliko Katika Tabia Mbaya Zinazokukwamisha Kufikia Mafanikio Makubwa.

Kuna wakati katika maisha suala la kubadili  tabia na hatimaye kuwa na tabia za mafanikio ni la muhimu sana. Tunapokuwa tunajijiengea tabia za mafanikio kwa wingi katika maisha yetu inakuwa rahisi kufikia mafanikio makubwa. Kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa ya kujifunza tabia za mafanikio ili kujihakikishia mafanikio ya kudumu.
Lakini pamoja na umuhimu huo wa kuwa na tabia za mafanikio, kuna changamoto nyingi kubwa ambazo zinakuwa zinatukuta wakati tunapotaka kubadili tabia hizi. Moja kati ya changamoto kubwa ni kujikuta baada ya muda tunaanza kurudia tabia zile za awali ambazo ulikuwa umepania kuziacha. Kwa mfano unaweza ukaanza tabia ya kufanya mazoezi kila siku, lakini baada ya muda unajikuta unaanza kutegea au kuaacha kabisa.
Hiyo haitoshi unaweza ukawa umejipangia ratiba yako vizuri kabisa ya kuhakikisha ni lazima kila siku utaamka asubuhi na mapema na kuanza kujisomea. Kwa siku mbili za kwanza kwa hamasa kubwa unafanya hivyo, ila unashagaa baada ya muda tena kupita unajisahau na kurudia maisha yako ya awali. Zipo tabia nyingi mbaya kwetu ambazo kuna wakati tunajaribu sana kuzibadili na zinakuwa kama zinakataa.
Ni kitu ambacho kimekuwa kikiwatokea watu wengi kiasi kwamba kupelekea wengine kukata tamaa na kuamini kwamba tabia walizonazo haziwezi kubadilika kwa namna yoyote. Watu hawa wamekuwa wakisahau kuwa kila kitu kinauwezo wa  kubadilika ikiwa kuna mikakati au mbinu za kufuata. Ni mbinu hizihizi ambazo nataka nikushirikishe hapa ili kufanya mabadiliko katika tabia mbaya zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa.
1. Anza kufanya mabadiliko kidogo kidogo.
Ikiwa unataka kubadili  tabia mbaya mojawapo uliyonayo, anza kwa kubadili kidogo kidogo. Kama umeamua kutaka kujenga tabia ya kujisomea anza kwa kusoma kurasa chache kwanza, kisha siku kadri zinavyozidi kwenda unakuwa unaongeza kidogo kidogo. Chochote unachotaka kubadili, anza nacho kidogo kidogo hiyo itakuwa ni mbinu sahihi ya kukufikisha kwenye mafanikio.
2. Fanya mabadiliko hayo yawe endelevu.
Kama umeamua kujenga tabia ya kujisomea, jisomee kila siku bila kuacha. Kama umeamua kujenga tabia ya kuamka asubuhi na mapema fanya hivyo pia bila kuacha. Kwa kila tabia ambayo umeamua kuifuata ifanye iwe endelevu kwako. Lakini ikiwa utafanya leo na kesho ukaacha hiyo itakuwa ni sawa na kupoteza muda kwako kwani hakuna ambacho utakuwa unafanya. Na ili kufanikiwa katika hili anza kwa kidogo kama nilivyotangulia kusema.
3. Ongeza majukumu kila siku.
Ikiwa lengo lako kubwa ni kujisomea kama nilivyosema kwa kadri siku zinavyosonga mbele, ongeza idadi ya kurasa unazojisomea. Kwa chochote kile unachofanya ongeza mzigo zaidi kwa kadri siku zinavyokwenda ili kukua. Kwa kufanya hivyo utajikuta unazidi kuleta mabadiliko na unakuwa unamudu kujijengea uwezo mkubwa wa kubadili tabia zako na kuwa na tabia za mafanikio zaidi.
4. Jiwekee Tathmini.
Kwa kuwa upo kwenye mchakato mzima wa kuweza kubadili zako zinazokukwamisha na kujenga tabia za mafanikio ni vizuri ukawa mtu wa kujiwekea tathimini. Kila mara na kila wakati uwe makini kuangalia mabadiliko. Je, ni kweli unayapata au upo palepale? Kama kuna sehemu unakwama unaweza ukawa ndiyo wakati wa kurekebisha na kusonga mbele.
Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio iwe ya ushindi daima.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: