Mara nyingi watu huwa hawapendi kuujua ukweli kwa sababu ukweli unauma. Hasa pale ambapo ukweli huo unakuwa unahusu mapungufu ya mtu moja kwa moja.

Haijalishi hutaki kuusikia ukweli kwa kiasi gani, lakini hili halitabadili ukweli. Ni bora ukabadili mtazamo wako kuhusu kupokea ukweli na hili litakusaidia sana.

SIKILIZA NA FANYIA KAZI
SIKILIZA NA FANYIA KAZI

Njia moja muhimu ya kupokea na kujua ukweli ni kuomba mrejesho. Kwa jambo lolote ambalo unafanya, omba watu wakupe mrejesho, omba kujua ni wapi unafanya vizuri na wapi unakosea. Kama unafanya biashara uliza wateja wako au wasaidizi wako. Kama umeajiriwa uliza mwajiri wako au wasaidizi wako. Kama ni kwenye familia mwulize mwenza wako.

SOMA; Huu Ndio Ukweli Kuhusu Wewe.

Waulize watu hawa muhimu ni kipi wanaona hakiendi sawa, au ni kitu gani wangetaka kiwe bora zaidi. Najua utaogopa kufanya hivi kwa sababu hutaki kusikia ukweli kwamba kuna maeneo unakosea, ukweli unauma.

Lakini kama unakwepa ukweli nataka nikuambie kitu kimoja kwamba ni wewe pekee ndio utakuwa hujui kinachoendelea. Kwa mfano kama unafanya biashara na mteja haridhiki, mteja huyo atamwambia kila mtu kasoro wewe. Kwa sababu labda alishawahi kukua mbia na wewe hukusikiliza au ulimkatisha tamaa.

Ni muhimu sana kusikiliza na kuchambua maoni au mrejesho wowote ambao unapewa na watu ambao ni muhimu kwako. Unaweza kuwa na ukweli ambao utakusaidia wewe kuwa bora zaidi.

TAMKO LA LEO;

Ukweli ni mzuri ila ni mchungu kusikia, hasa pale ambapo unahusisha maoni au mrejesho kwa kile ambacho ninakifanya. Kuanzia sasa nitaacha kuogopa ukweli na kukaribisha maoni haya. Kwa sababu najua kama nikiuogopa hakuna kinachobadilika bali mimi ndio ninakuwa nje ya ukweli. Lakini kama nitaupokea na kuufanyia kazi kuna kitu naweza kubadili na hivyo nikawa bora zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.