Kitu Kimoja Ambacho Wapenda Mafanikio Wote Wanacho Kwa Pamoja.

Habari za leo msomaji wangu wa AMKA MTANZANIA na wa makala hii, nikukumbushe kwamba kama hujui umuhimu wa wewe kupewa pumzi ya uhai na Mungu, ila unajua tu shida zako na maumivu unayopitia, utakuwa hujitendei haki kabisa na utakuwa unajinyima fursa nyingi za kuona vitu vizuri mbele yako. Nikushauri kwamba changamoto unayoipitia sasa ni moja ya safari yako, isikupe shida bali tazama uelekeo wako wa kufika kituo chako cha safari, hii itakupa nguvu na ujasiri wa kujua hilo jambo ni la muda tu utalipita.
Siku zote za maisha yetu ya kila siku watu wengi hupenda kuwa katika hali fulani hivi kama mtu fulani wanaomwona yupo vizuri kimafanikio ya kimwili ama kiroho. Kuna watu wasipomsikia fulani kasema nini juu ya jambo fulani linalozushwa sana wataona hilo jambo halina uzito wowote, tofauti na wanavyolichukulia wengine.

PENDA MABADILIKO, HATA KAMA UPO MWENYEWE.


Binadamu yeyote duniani kabla ya kufanikiwa jambo lolote lile kubwa na lenye kuwavuta wengi na kuwafanya wajiulize kwa nini huyu kafanikiwa kiasi hiki, mbona yupo tofauti na sisi, mbona tukijaribu kumwiga anabadilika haraka, mbona ana wateja wengi, mbona dunia/jamii inamzungumza sana, mbona hana tofauti kubwa na mimi, kwa nini yeye yupo hivi na vile? Ukijaribu kujiuliza sana haya maswali ni ngumu kuyapatia majibu sahihi kama hutojijua wewe ni nani na kwa nini ulizaliwa na kwa nini mpaka sasa unaishi japo hata kwenye ukoo wako kuna watu hawakufahamu kabisa sababu huna kitu cha kuwafanya ukujue kwa mema.

SOMA; Mambo 10 Ambayo Watu Wenye Mafanikio Huyafanya Sana Katika Maisha Yao.
Mtu yeyote akijitambua huanza kutamani mabadiliko, mabadiliko haya ndio yanayomfanya aendelee kuwa bora zaidi ya jana, huwezi kumkuta mtu anayejitambua anafanya vitu vya kipuuzi puuzi pasipo maana yeyote labda ukute karukwa na akili, lakini kila jambo analolifanya mtu mwenye kujielewa yeye ni nani muda huo na anatakiwa afanye nini na hatakiwi kufanya nini kwenye maisha yake, mtu wa namna hii huwezi kukaa naye zaidi ya nusu saa mkiwa mnaendana kauli zenu maana wakati wewe una mtazamo hasi yeye anakuwa na mtazamo chanya, wakati wewe unawaza makosa tu ya mtu fulani na kutafuta kosa moja tu katika yale yote aliyofanya mtu, yeye atakuwa anatazama yapi mazuri aliyofanya na yapi mabaya aliyokosea ili kupitia huyo mtu yeye asipate kufanya hilo kosa kwa kujipanga vizuri hapo mbeleni, ndivyo ilivyo kwenye makampuni/mashirika makubwa yaliyoendelea na kubaki sokoni pasipo kushuka chini kiuchumi.
Mpenda mabadiliko yeyote huwezi kumkuta akiwa palepale alipokuwa jana, yeye anapoimaliza siku yake anawaza leo nimefanya nini? je katika yote niliyofanya lipi nimekosea, na lipi nimefanya kama jana na wakati nilipaswa kufanya kama leo na sio jana, katika yote niliyofanya yapi ya kurekebisha na yapi yakuondoa, na yapi ya kuongeza, ukifika hatua hii katika maisha yako ya kila siku iwe wewe ni mjasiriamali/mwimbaji/mfanyabiashara/mwanafunzi na vingine vingi unavyovifahamu na kuvifanya katika maisha yako utakuwa tofauti sana na wenzako wote wanaokuzunguka. Hili halihitaji miujiza mikubwa sana, linahitaji ujitambue tu, ukishajitambua na kuanza kutafuta kusudi lako na kuanza kutafuta vile vitu unavyoona ukifanya unajisikia vizuri, na usipofanya unajisikia vibaya, ama ukifanya unajisikia vibaya na hatia ndani kwako ila kwa watu vinaonekana vizuri lakini kwako unaona si sahihi maana unaujua ukweli, tambua kwamba ndani kwako kuna hitaji mabadiliko ndio maana unasikia vitu vikitofautiana.
SOMA; Tabia Hizi Nne(4) Ulizonazo Zinakuzuia Wewe Kufikia Mafanikio Makubwa.
Unachotakiwa kujua kitu kingine tena kwa wapenda mabadiliko, ni watu ambao hata njia anayopitia kila siku kuelekea sehemu yaweza kuwa kazini au shuleni… huwezi kumwona akipita njia hiyohiyo kila siku, huwezi kumwona akivaa nguo moja siku tatu mfululizo bila kubadili hata kama hana nguo za kutosha utamwona akibadili hata shati ili mradi aonekana tofauti tu, huwezi kukuta kwake upangaji wa vitu upo vilevile kama ulivyoona miezi sita iliyopita ama mwako uliopita lazima utakuta mabadiliko ndani kwake, huwezi kumwona akinunua nguo za rangi moja kila akiingia dukani, huwezi kumwona akiandika kwa mtindo uleule kila siku lazima utamwona akibadilibadili uandishi kutokana na uhitaji wa wasomaji wake yaani yeye kila siku anawaza ubunifu mpya.
Ukitaka haya mabadiliko yote yaanze kutokea kwako lazima ujitambue, mengine yatakuja yenyewe kwenye juhudi zako za kila siku, cha kufanya kama wewe tayari unajielewa lakini huoni mafanikio yeyote kwa kile unachofanya, jifunze kujishusha, jifunze kuwa msikilizaji kwa yule unayempa huduma, jifunze kujiuliza hiki ninachotoa kwa mteja wangu ingekuwa mimi ningekifurahia?, jifunze yale ambayo hupendi yaondoe haraka sana na yale unayoyapenda yaweke na uyaboreshe haraka sana na kabla hayajachoka yaondoe na badilika kutokana na uhitaji unaoupenda wewe utokee, usisubiri malalamiko kwa wateja wako kama wewe ni mtoa huduma bali mteja akutane na utofauti wa hali ya juu kwenye huduma yako.
Ukishindwa sana kuelewa haya ninayoyasema, jifunze kwa mtoto mdogo anayekua, mtoto hupenda kuweka akilini kile mkubwa wake anafanya, yupo makini kila hatua ya ukuaji wake, akifika wakati wa kutambaa huwezi kumkuka ulipomkalisha, akifika wakati wa kuota meno huwezi kumzuia kung’ata wakati ananyonya maana ule mwasho wa fizi zake ni mkali sana yeye anafikiri kung’ata kwake kutapunguza kuwasha kumbe anamuumiza mama yake. Penda mabadiliko yeyote yale kwenye maisha yako yawe kwenye ndoa/biashara/ofisini kwako ulipoajiriwa, usipende kuwa kama jana penda kuwa kama leo.
Makala hii imeandikwa na Samson Ernest ambaye anapatikana kwa jina hilohilo facebook, waweza wasiliana naye kwa njia ya kupiga simu/whatsApp 0759808081 au samsonaron0@gmail.com
Nikutakie mabadiliko mema katika huduma/kazi yako.
Pata makala nzuri moja kwa moja kwneye email yako kutoka AMKA MTANZANIA, bonyeza maandishi haya na uweke email yako na utakuwa unatumiwa makala.
Pata ujumbe mzuri wa hamasa kila siku asubuhi kwenye simu yako. Bonyeza maandishi haya na uweke namba yako ya simu na utaanza kupokea ujumbe wa hamasa kila siku.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: