Usiogope Kushirikisha Wengine Kile Unajua Kwa Hofu Ya Kuibiwa Ujuzi Wako.

Watu wengi wamekuwa wakipatwa na hofu ya kuwashirikisha wengine namna wanafanya mambo yao au kazi zao kwa kuhofia kuwa labda wakishafanya hivyo basi maana yao haitakuwepo tena, au labda wale watu hawataona umuhimu wao na wengine huhofia hata kupoteza kazi zao au labda bidhaa nyingi kuingia sokoni hivyo kupunguza au kupoteza baadhi ya wateja.

 
Ndugu yangu katika maisha hakuna jambo jema kama kuwashirikisha wengine kile unajua, au kuwaambia namna unafanya shughuli zako, kwanza naona inakusaidia hata wewe mwenyewe kujifunza zaidi wakati unapoelekeza wengine, inakupa nafasi ya kuweza kujifunza zaidi na hata kugundua vitu vipya au inakuwa ni nafasi yako wewe kuweza hata kuona vitu vile vile kwa upya au kwa mtazamo mwingine na ikaongeza maana kwenye utekelezaji wa manufaa yako, lakini ukitambua kuwa una wajibu wa kuelekeza wengine pia nawe utahakikisha unajifunza zaidi, kuona unapata vitu vipya na kuzidi kujiimarisha zaidi ili uzidi kubobea kwenye kile unafanya.
SOMA; Tengeneza Kipato Cha Ziada Huku Ukiendelea Kufanya Unachofanya Sasa.
Inawezekana wapo watu waliopoteza kazi zao kwa kuwa walishakuwa wametoa ujuzi wao kwa wengine na pengine wao wakaonekana si wa maana tena mahali pale. Kuna mwingine alipoteza wateja na pengine kufikia kufunga biashara yake kwa kuwa tu aliwaelekeza namna anavyofanya biashara yake na wao wakaweza kumuiga. Ndugu yangu mimi naamini kwamba sisi wote tumeumbwa tofauti, kila mtu ana namna yake ya kufanya mambo yanayoonekana kuwa sawa kabisa, hivyo katika lolote usilipe wazo la kwamba nikimfundisha nitapoteza nafasi yangu au nikimfundisha mimi nitapoteza wateja wangu n.k, furahia kuona kwamba angalau umepata nafasi ya kushirikisha wengine ujuzi wako, umepata nafasi ya kuongeza kitu kwa wengine, maana hapo ni unakuwa unagusa maisha ya mtu moja kwa moja kwa kupanda kitu cha maana ndani mwake. Ndugu yangu tambua kuwa hata kama ataanza fanya kitu hicho hawezi kukifanya kama wewe, maana wewe ni wewe na yeye ni yeye, nyie ni watu wawili tofauti, mnatofautiana hata namna ya kufanya mambo yenu, mnaweza kufanya jambo hilo hilo lakini kwa namna tofauti, kila mtu ana namna ya kufanya yake. Usiipe hofu nafasi na kukufanya ukose nafasi adimu hiyo ya kufundisha wengine kile unaelewa vyema, hofu ni adui wa wewe kufikia malengo yako, usiisikilize hofu, hofu haina habari njema ya kukupa wewe, maana hofu itakuambia usifanye hiki, usifanye kile na tambua kuwa hofu huwa inakuwa na sababu zinazoonekana za maana na za ukweli kabisa hivyo kukufanya wewe ujifariji na kujiona umefanya maamuzi sahihi. Ndugu yangu zinduka huko usingizini, huu sio wakati wa kuogopa kushirikishana maarifa uliyo nayo na wengine, unaweza kukataa kumshirikisha hayo mawazo au ujuzi lakini mwenzio anaweza kupata kila kitu mtandaoni, anaweza asiyapate kama ambavyo wewe ungempatia lakini waweza shangaa anafanya hata zaidi yako, hivyo acha uchoyo na hofu . Tambua kwenye kufundisha , unafundishwa pia. Hakuna namna utafundisha nawe usipate cha kujifunza, ndugu yangu vipo vingi sana vya kujifunza hapa duniani na ili mradi tunaishi hapa chini duniani basi kila siku kipo kitu cha kujifunza, hakuna ajuaye vyote mpaka wakati huu, wote bado tunategemeana kwa namna moja au nyingine.
SOMA; Mambo Saba(7) Yanayowafanya Wafanyakazi Wengi Kuwa Na Ufanisi Mdogo Kwenye Kazi Zao.
Kuna mwingine anakaa na kujiona kama hana kitu cha kushirikisha wengine, anajiona yeye hafai hana kitu cha maana , ndugu yangu tambua kuwa kila mtu ni wa muhimu sana na ana kusudi lake kuwepo hapa duniani, hivyo hakuna mwanadamu asiye na jambo la kumfaidia mwenzie, unacho kitu cha maana pia, unaweza kuwa unaona ni kidogo au ni cha kawaida lakini tambua kuwa kinaweza fanya badiliko ndani ya mtu mwingine, usisite wala kuogopa kushirikishana na wengine kile unacho, usiwaze kwamba kitapokelewaje n.k, wewe fanya wajibu wako wa kushiriki na wengine kile umepewa na muumba basi hayo mengine muachie aliyekiweka ndani mwako ndiye anajua yule alimkusudia afaidike na ujumbe wako au kile unacho, si lazima ukubalike na watu wengi sana.
Amka, shiriki na wengine kile umepewa ndugu yangu.
Makala imeandikwa na Beatrice Mwaijengo
+255 755 350 772

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: