Habari za leo rafiki?

Hongera sana kwa kuuanza mwaka huu mpya wa mafanikio. Leo ni siku ya kwanza kabisa ya mwaka wetu huu mpya.

Kama bado huelewi ni nini kinaendelea hapa basi huenda hukusoma makala inayoelezea kuhusu mwaka huu mpya. Lakini sio kesi, kwanza isome hapa halafu ndio urudi hapa tuendelee na mipango yetu ya mwaka huu mpya.

Isome makala yenyewe hapa; Jambo Muhimu Sana Kwako Kuzingatia Kabla Mwaka 2015 Haujaisha Na Kuanza Kwa Mwaka 2016.

Kama tayari umeshaisoma makala na ukaielewa vizuri basi nikukaribishe tena kwenye mwaka wetu huu mpya ambao una miezi 13. Ndio huu ni mwaka wa tofauti na wa kipekee sana kwetu sisi wana mafanikio. Na kama umejitoa kweli kwamba mwaka huu 2016 unataka kufanya makubwa, basi siku ya kuanza hivyo ni leo.

Hivyo basi pamoja na maelekezo niliyotoa kwenye makala ya wewe kutuma email, bado naendelea kutengeneza mpango bora sana wa kuhakikisha 2016 inakuwa ya tofauti kwa kila mmoja wetu.

Mwaka huu 2016 utakuwa mwaka wa kipekee sana, lakini hautakuwa wa kipekee kama wengine wanavyosema tu, bali utakuwa wa kipekee kwa sababu utakwenda kufanya kwa kipekee.

Hivyo kwa siku ya leo fanya lile zoezi ambalo nimekushirikisha kwenye makala hiyo hapo juu, andika vizuri sana, na tuma mawasiliano yako pia.

Kwa upande wangu naandaa mfumo mzuri ambao nitakushirikisha wa kuweza kupanga malengo ya mwaka huu 2016, na tunaanza kuyafanyia kazi mara moja wakati kila mtu anajiandaa na sikukuu na mengine mengi. Ili wakati wao wanazinduka na kuanza kujipanga, sisi tunakuwa tumeshashika kasi ya ajabu.

Tuendelee kuwa pamoja kupitia KISIMA CHA MAARIFA, AMKA MTANZANIA na hata kupitia email yako na tutaendelea kushirikishana mbinu hizi muhimu za kuhakikisha kila siku yetu inahesabika kuwa siku ya kipekee. Na kwa mwaka wetu huu mpya, ni lazima uwe wa kipekee zaidi.

Najua kama tumekuwa pamoja kwa muda, mwaka wako 2015 haukuwa kama miaka mingine, ulikuwa wa tofauti na nina hakika kuna mengi ulianza kufanya, huenda kuna mengi hukuwez akukamilisha kama ulivyotaka, usiogope wala kukata tamaa, wenzako wengi hawajaanza hata hiyo hatua. Na mwaka huu 2016 utakwenda mbali zaidi ya pale ulipokwenda 2015.

Je upo tayari twende pamoja kwa miezi hii 13, tufanye makubwa pamoja, tuwe na maisha bora na tunayoyafurahia, basi hakuna nafasi nyingine zaidi ya hii moja muhimu sana.

Fanyia kazi yaliyopo kwenye makala iliyopita na endelea kufuatilia hapa kwa makini, wiki hii nitakushirikisha mpango mzuri sana kwa mwaka wetu huu mpya.

Nakuahidi kwamba nimeshajitoa kuwa na wewe katika safari hii ya kuboresha maisha yetu, swali ni je wewe umejitoa kuendelea kuwa pamoja na sisi? Kama ndio basi hongera sana.

Kwa sasa nikuache ukitafakari vyema mwaka wako 2016 unataka uweje, ninakuandalia njia nzuri ya kuyaandika malengo yako kwa 2016 na nitakushirikisha pamoja na taarifa nyingine muhimu.

Rafiki na Kocha wako.

Makirita Amani.