Mambo 20 Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha The 360 Degree Leader.

Habari ndugu msomaji wa makala za uchambuzi wa mambo 20 kutoka kwenye kitabu. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri. Karibu tena katika utaratibu wetu wa kujifunza kupitia kitabu cha wiki. Wiki hii tutajifunza kutoka kwenye kitabu kinaitwa The 360 degree Leader, kitabu hiki kimeandikwa na Mwandishi nguli wa maswala ya Uongozi, si mwingine bali ni John C. Maxwell. Kitabu hiki amekiita kiongozi wa nyuzi 360 (The 360 degree leader) kwa sababu kinahusu jinsi ya kuongoza popote pale ulipo, bila kujali upo kwenye pembe ipi ya dunia, au ngazi ipi ya cheo katika kazi. 
Kitabu hiki ni kizuri sana hasa kwa watu wanaotaka kuwa viongozi, ni kizuri sana kwa viongozi wanaoanza na kinawafaa zaidi viongozi wa ngazi ya kati (middle leaders), viongozi wa kati ni wale ambao wako kwenye nyadhifa za katikati za shirika au kampuni. Kitabu hiki kinafundisha mambo mengi sana, lakini kubwa ni jinsi gani ya kutengeneza ushawishi na kuongoza watu popote ulipo bila kujali cheo chako. Kinafundisha kanuni za kuweza kuwaongoza wale waliokuzidi vyeo (mabosi zako), wale wenye vyeo sawa na wewe, na wale wa chini yako.
 
Karibu sana tujifunze.
1. Kua kiongozi haihitaji kua na cheo fulani. Wala huhitaji kua Mkurugenzi au CEO ili uweze kuongoza kwa ufanisi. Unaweza kuongoza popote pale ulipo na kuleta mabadiliko makubwa, hata kama una ripoti kwa mtu mwingine wa juu yako ambaye sio kiongozi mzuri. Siri ni kujifunza kuendeleza ushawishi wako ukiwa hapo ulipo, kwenye nafasi hiyo uliyopo. Unajifunza kuongoza walio juu yako, waliosawa na wewe, na walio chini yako.
2. Uongozi ni uchaguzi unaofanya na sio sehemu ulipo kaa (nafasi). Kila mtu ana uwezo wa kuchagua kua kiongozi popote pale alipo bila kujali cheo. You can make a difference no matter where you are.
3. Ukitaka kufanikiwa katika uongozi, jifunze sana kuhusu uongozi kwa kadri uwezavyo kabla hujapata cheo, maana itakusumbua sana kujifunza ukiwa tayari umefika pale. Kama unataka kua CEO, jifunze sana kuhusu uongozi mzuri wa CEO unapaswa uweje. Kwa maneno mengine fanya maandalizi mapema. If you want to be a successful leader, learn to lead before you have a leadership position.
4. Makosa yanayofanyika na kiongozi wa juu hua yanagharimu shirika au kampuni kwa kiasi kikubwa kuliko makosa yanayofanywa na viongozi wa chini. Kama usipojifunza ujuzi mbalimbali za uongozi na mchakato wa kufanya maamuzi wakati ukiwa bado kwenye nafasi ya chini ambapo vihatarishi (risks) ni vidogo, basi kuna uwezekano ukapata taabu sana pindi utakapofika ngazi za juu ambapo gharama ya makosa inakua ni kubwa, pia makosa yanakua na athari kwa watu wengi na pia ni rahisi sana kuonekana. Becoming a good leader is a lifelong learning process.
SOMA; Kiongozi Anazaliwa au Anatengenezwa? Jibu Hili Hapa.
5. Watu wasiokua na uzoefu wa uongozi, hua wana makadirio yaliyozidi (overestimate) kuhusu umuhimu wa cheo fulani cha uongozi. Mfano kabla mtu hajawa Meneja, anakua na matazamio makubwa sana kuhusu kua Meneja, anaweza dhani pengine akifika hapo atakua mtu wa muhimu sana, pengine akifika hapo kila mtu atamheshimu, au atakua na mamlaka makubwa sana. Unaweza kuwagundua watu wa mtindo huo hata kwa maneno yao, kwa mfano wengi husema, “yaani ningekua mimi ndio meneja wa hii kampuni, ningeongeza mishahara ya wafanyakazi wote” au Mimi ningekua ni waziri wa wizara ya Nishati na madini ningefanya hili na lile. Hii yote ni kwa sababu hawana uzoefu na uongozi huo. Pengine wakifika hapo, wakawa na mtazamo tofauti kabisa.
6. Viongozi wazuri hua wanakua na ushawishi zaidi ya cheo walicho nacho. Kama tunavyoelewa uongozi ni ushawishi, uwezo wa kushawishi watu wakufuate. Viongozi wasio na uwezo, hawawezi kushawishi watu nje ya cheo walichonacho, yaani watu wanamfuata kwa sababu ya cheo chake tu, ila siku wakivuliwa wadhifa huo hakuna anayetaka hata kumsikia. Hii ina maana cheo chake ndio kilikua kinamsaidia kulazimisha watu wamfuate anachosema. Viongozi wazuri ni wale wenye uwezo wa kushawishi watu hata zaidi ya madaraka ya cheo walichonacho. Unakuta mtu ni kiongozi wa ngazi ya chini ila ana uwezo hata wa kushawishi mabosi zake wakaufuata ushauri wake. Hata anapoachia wadhifa wake bado watu wanamfuata anachosema na kushauri.
.
7. Kufikiri kwamba maisha katika nafasi ya juu ya uongozi ni rahisi, ni sawa na kufikiri kwamba majani ya upande wa pili wa uzio ni ya kijani kizuri. Wakati hujayaona. Kua katika nafasi ya juu ya uongozi kuna matatizo yake na changamoto zake pia, lazima ujipange kwa hilo.
8. Unapopanda kwenda juu kwenye uongozi wa shirika, uzito wa majukumu yako unaongezeka. Katika mashirika mengi kwa kadri unavyopanda juu kiuongozi (cheo) wingi wa majukumu unayopewa unaongezeka haraka kuliko hata mamlaka unayopata. Kwanza unapopanda juu, vitu vingi vinatarajiwa kutoka kwako, shinikizo (pressure) inakua ni kubwa zaidi, na hata athari ya maamuzi yako yanakua na uzito. Lazima uyazingatie haya mambo. So in some ways, leaders have less freedom as they move up, not more.
9. Viongozi wazuri ni mara chache sana hufikiri kwa kuangalia vikwazo au mipaka (boundaries) inayowazuia, badala yake hufikiri kwa kuangalia fursa zinazowazunguka na zinazoweza kutokea mbeleni. Sifa ya kiongozi ni uwezo wake wa kufanya mambo yatokee, na sio kuonyesha sababu kwa nini hakijafanyika. Leadership is seeing opportunity in tough times
10. Viongozi wabovu hulazimisha heshima, yaani hua wanataka waheshimiwe hata kwa lazima, wakati mwingine hata kwa kutisha wengine ili wawaheshimu. Kwa upande mwingine viongozi wazuri na wenye uwezo heshima kwao huja moja kwa moja, maana wanapofanya wajibu wao vizuri kunawaletea sifa nzuri ambayo huwaletea heshima. Ukiona kiongozi analazimisha heshima, ujue hana uwezo, na ndani yake ni mdhaifu, sasa anajihisi kila mtu anaona udhaifu wake, hivyo anataka kuufunika.
11. Jiongoze mwenyewe vizuri. Watu hudhani uongozi huanza kwa kuongoza wengine, wakati mwingine hata hawataki kujifunza maswala ya uongozi maana wanaona wao sio viongozi, tena hawana watu wa kuwaongoza. Ukweli ni huu, uongozi unaanza na wewe, kwa kujiongoza wewe mwenyewe. Kama huwezi kujifuata mwenyewe, nani atakufuata? Hujaona watu wenye nyadhifa za juu, lakini hawawezi kujiongoza hata wao wenyewe, yaani anasema hichi, kisha yeye anafanya kingine. Anza kwa kujiongoza mwenyewe, anza kwa kujifuata mwenyewe, wengine watakufuata. Lead yourself. That’s where it all starts
SOMA; Siri Kumi za Mafanikio Kwenye Uongozi.
12. Watu waliofanikiwa wanafanya vitu ambavyo wale ambao hawajafanikiwa hawako tayari kuvifanya. Mfano wengi ambao hawafanikiwi hawapendi kufanya vitu vigumu, vitu vyenye kuhitaji kutumia akili sana. Wanataka vitu rahisi ambavyo kila mtu anaweza kufanya. Katika maisha ukiona kitu ambacho kila mtu anaweza kukifanya achana nacho.
13. Kiongozi wa wadhifa wa katikati katika shirika ili uweze kujenga ushawishi mkubwa hata kwa wakubwa zako, ni sharti kufanya mambo ya tofauti ambayo wenzako wa ngazi sawa na wewe hawataki kuyafanya. Moja wapo ni kufanya shughuli zinazoonekana ni ngumu kwa wengine. Unapoweza kufanikisha majukumu magumu utaonekana mapema sana. Ukiweza kutengeneza ujuzi wa kutatua matatizo, heshima yako itaongezeka na utahitajika sana katika shirika. Unajua kwa nini? Maana changamoto na matatizo kazini hua hayaishi, changamoto na matatizo ni sehemu ya kazi na wengi hawapendi kukabiliana nazo. Hivyo wewe ukiweza kuzikabili na kutatua utajijengea heshima tena kwa haraka. Uongozi wako utaendelea kukukua siku hadi siku.
14. Ni rahisi kutoka kwenye kushindwa (failure) kwenda kwenye mafanikio, kuliko kutoka kwenye visingizio (excuses) kwenda kwenye mafanikio. Watu wako tayari kutoa sababu 100 kwa nini hawezi, kuliko kutoa sababu hata 2 kwa nini wanaweza. Wanaotoa udhuru hua hawajaribu, na hawako tayari kushindwa. Kutokana na kushindwa unajifunza, kisha unafanya maboresho, halafu unasonga mbele. It’s easier to move from failure to success than from excuses to success.
15. Kuna tofauti kati ya uongozi (leadership) na utawala (management). Utawala unafanya kazi na michakato (processes) wakati uongozi unafanya kazi na watu. Vyote vinahitajika ili shirika au kampuni iweze kuendeshwa vizuri. Meneja kazi yake ni kuhakikisha michakato, mifumo na taratibu mbalimbali zinafuatwa kikamilifu, lakini kiongozi kazi yake ni kuwaongoza wao wanaosimamia hiyo michakato. Kwa maneo mengine uongozi ni zaidi ya utawala. Leaders lead the people who manage the processes.
16. Kiongozi mzuri hua anaweka mkazo kwenye vile visivyoonekana au visivyoshikika. Mara nyingi vitu vinavyosimamiwa (manage) ni vile vinavyoshikika na kupimika. Vitu hivyo hutoa ushahidi halisi na unaweza kuvifanyia tathimini ya kimantiki (logical evaluation) kabla ya kufanya maamuzi. Kwa upande mwingine Uongozi ni mchezo wa visivyoshikika. Tunaposema uongozi ni ushawishi, je unaweza kuushika ushawishi kwa mkono? Viongozi wanahusika na vitu kama ari, hamasa, hisia, mtazamo, n.k Hii Ndio maana ya vitu visivyoshikika.
SOMA; Makosa Makubwa Matano Yanayoweza Kukuharibu Wewe Kama Kiongozi.
17. Timu ya uongozi inakua na ufanisi zaidi ya kiongozi mmoja. Hivyo ili shirika lifanikiwe ni lazima, kama kiongozi ujikite katika kutengeneza timu ya viongozi badala ya kutegemea mtu mmoja tu. Kama wewe ni kiongozi wa nyadhifa ya kati kwenye shirika, jikite zaidi kuwatengeneza wale unaowaongoza kua viongozi. Wanapokua viongozi na kufanya kazi kama timu ya viongozi, ndivyo hivyo ufanisi utakua mkubwa katika kitengo au idara yako, na ndivyo utajiweka katika nafasi nzuri ya kwenda juu zaidi.
18. Viongozi wenye maono wako tayari kuwaajiri watu wazuri kuliko wao, hata kama itabidi kuwalipa mshahara mkubwa kuzidi wa kwao. Jambo hili sio rahisi kwa viongozi wengi, maana wengi wanaweka maslahi yao mbele kuliko ya maslahi ya shirika. Viongozi wengi wanatamani wao ndio waonekane wazuri zaidi, hata wanapoajiri watu, wanataka waajiri wenye uwezo mdogo kuliko wao au angalau wenye uwezo sawa na wao. Maana anaangalia kwamba huyu mwenye uwezo zaidi anaweza kuja kuchukua nafasi yangu. Mimi binafsi nimewahi kushiriki katika mchakato wa kumwajiri mtu ambaye alikuja kua bosi wangu, kwenye interview alifanya vizuri, lakini nilihitajika na viongozi wangu kumtolea mapendekezo/sifa za ziada maana nilikua nikimfahamu kabla na ilijulikana kwamba nilisoma naye chuo kimoja. Japo alikua anakuja kua bosi wangu, nilikua muwazi maana nilijua uwezo wake mzuri aliokua nao, nikatoa mapendekezo mazuri juu yake ili aajiriwe. Kisha aliajiriwa na akaweza kuonyesha uwezo wake mkubwa, na baada ya muda mfupi akapandishwa cheo cha juu zaidi. Visionary leaders are willing to hire people better than themselves.
19. Uongozi ni safari inayoanzia pale ulipo, na sio pale unapotaka kuwepo. Hii ina maana kwamba uongozi hauanzii kwenye nafasi ya juu, unaanzia pale ulipo. Hata kama huna aliyepo chini yako wa kumuongoza, unaanza na kujiongoza wewe, kisha utawaongoza wale wenzako mliopo sawa, halafu utawaongoza wale wa juu yako. Hivyo anza kujifunza kuongoza kuanzia hapohapo ulipo. Ukifanya vizuri katika nafasi uliyopo ni rahisi kupanda ngazi. Viongozi wa juu wanapoangalia nani wa kumpandisha ngazi ya juu, sifa ya kwanza wanaangalia ni nani anayefanya vizuri kwenye nafasi aliyopo kwanza. Mfano kama shirika lina maofisa kadhaa, na kuna nafasi ya meneja inahitajika kujazwa, ikitokea kwamba wanataka kumpandisha mmoja wa maofisa ili awe meneja, ni lazima wataangalia kwanza katika hao maofisa ni yupi anayefanya vizuri katika hiyo nafasi yake ya uofisa. Leadership is a journey that starts where you are, not where you want to be
20. Ukuaji wako kama kiongozi ndio uhai wa uongozi wako. Ili uzidi kuongeza ushawishi kama kiongozi, na kufanya wale unaowaongoza waendelee kukufuata ni lazima uendelee kukua. Ili uweze kutengeneza viongozi ni lazima uwe unakua, ufahamu wako uwe unaongezeka mara kwa mara. Uwezo wako wa kufanya mambo lazima ukue, uwezo wako wakufikiri na kuona mbali zaidi lazima ukue. Usikubali kudumaa kiuongozi, jifunze kila siku, maana hakuna kiongozi anayejua kila kitu kuhusu uongozi. Utofauti wetu unatokana na utayari wa kujifunza kila siku na kufanyia kazi yale tunayojifunza.
Asanteni sana
Tukutane wiki ijayo
Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

One thought on “Mambo 20 Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha The 360 Degree Leader.

  1. Kingi Kigongo December 2, 2015 / 10:05 am

    Kwa kweli ni makala nzuri inayohamasisha jamii. Shukrani sana.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s