Sababu Tano Zinazokuzuia Kufikia Malengo Yako Ya Kila Mwaka Na Jinsi Ya Kuepuka Hilo 2016.

Kulingana na tafiti zilizofanyika kwenye eneo la kuweka malengo, watu wengi wamekuwa wanaweka malengo yale yale kwa kila mwaka na wamekuwa wanashindwa kuyafikia.
Yaani mwaka 2016 utakapoanza, utaweka malengo yale yale uliyoweka 2015 na ukashindwa kuyafikia. Na mbaya zaidi utayaweka kwa mtindo ule ule hivyo kufanya vigumu kwako kuweza kuyafikia.
Kuna sababu kuu tano ambazo zimekuwa zinawazuia watu wengi kushindwa kufikia malengo wanayoweka. Sababu hizi pia zimekuwa zinakuzuia wewe kufikia yale maisha ya ndoto zako. Kupitia makala hii ya leo utakwenda kuzijua sababu hizi na jinsi ya kuweza kuzishinda.
Je upo tayari kuzijua sababu tano ambazo zimekuwa zinakuzuia kufikia malengo yako? je upo tayari kuchukua hatua ya kuondokana na sababu hizi? Kama ndio karibu sana.
Sababu ya kwanza; kuweka malengo kwa kuendeshwa na hisia.
Mwaka mpya mambo mapya, hii ni kauli ambayo imekuwa inatumika sana kwenye kipindi cha mwaka mpya. Na kwa sababu kwenye kipindi hiki karibu kila mtu anakuwa anazungumzia malengo, basi na wewe unajikuta umebebwa kwenye hilo. Unajikuta unaweka malengo ambayo hujui kwa nini unayaweka, ila unaweka tu kwa sababu kila mtu anaweka malengo.
Tatizo la kuweka malengo kwa kuendeshwa na hisia ni kwamba zile hisia zinapoisha, na wewe unasahau malengo yale. Na ndio maana zile shamra shamra za mwaka mpya zinapoisha na yale maisha ya kawaida kurudi, watu wengi wamekuwa wakisahau malengo yao na kurudi kwenye maisha yao ya kawaida.
Sababu ya pili; unaweka malengo ambayo hujayachambua vizuri.
Malengo kwenye maisha yako ni kama ramani ya nyumba. Unapochukua ramani ya nyumba inakuwa imechambuliwa vizuri kuanzia msingi mpaka paa. Na kwa fundi yeyote anayeangalia ramani hiyo anaweza kuijenga vizuri sana. Lakini kama utamfuata fundi na kumwambia nijengee nyumba ya vyumba vitano na ukaondoka, fundi anaweza kujenga nyumba ya vyumba vitano vinavyofuatana kama madarasa ya shule.
Hili umekuwa unalifanya sana kwenye malengo yako, unasema mwaka huu mpya nataka nipate fedha zaidi! Vizuri, lakini hiyo zaidi ni kiasi gani? Kama ulikuwa unapata elfu kumi na sasa ukaanza kupata elfu kumi na mia moja ni fedha zaidi. Hivyo mwisho wa mwaka unaweza kuona hujafikia malengo, lakini ukweli ni kwamba hukuwa na malengo yoyote, kwa sababu hukuchambua vizuri.
Sababu ya tatu; kutokuandika malengo yako.
Kuna sababu kubwa sana kwa nini kwenye makubaliano mengi watu wanafanya kwa maandishi. Mnaingia mkataba ambao kila mtu anatakiwa kuufuata. Kwa nini msikubaliane tu kwa mdomo? Kwa sababu inajulikana kwamba jambo lolote ambalo halipo katika maandishi halipewi uzito mkubwa. Na pia akili zetu sio za kuamini sana katika uwekaji wa kumbukumbu. Tunakutana na mambo mengi sana kila siku ambayo yanatufanya tuweze kusahau yale ambayo ni muhimu zaidi kwetu.
Umekuwa unatamka tu malengo yako na kuishia hapo, hujawahi kukaa chini na kuandika malengo hayo. Kwa kuyaacha tu kwenye akili yako, yale maisha yako ya kawaida yanapoanza, na ukaanza kukutana na changamoto zako za kawaida ni rahisi sana kusahau malengo hayo.
Sababu ya nne; umekuwa unakata tamaa mapema.
Watu wengi wamekuwa wakifikiri kwamba ukishaweka malengo tu, basi njia ni nyeupe kwa wewe kuweza kuyafikia. Lakini huu sio ukweli, kuweka malengo sio uhakika kwamba utayafikia kirahisi, bado utakutana na changamoto nyingi kwenye safari yako hiyo.
Kama utakosa uvumilivu na kukata tamaa, itakuwa vigumu sana kwako kufikia malengo hayo. Na watu wengi wamekuwa wakifanya hivi, wanayafanyia kazi malengo yao kwa kipindi cha mwanzo, baadaye wanaona mambo ni magumu na kuacha malengo hayo. Na hasa inapokuwa imekaribia mwisho wa mwaka, wengi hupunguza kabisa kasi na kusema wanajipanga kw amwaka ujao. Kwa bahati mbaya hata mwaka huo ujao wanaendelea kurudia yale yale.
Sababu ya tano; kuweka malengo madogo ambayo hayakusukumi zaidi.
Hii pia ni changamoto kubwa sana katika uwekaji malengo. Watu wengi wamekuwa wanaweka malengo ambayo hayawasukumi kutoka pale walipo sasa, au kufanya kazi zaidi ya wanavyofanya sasa. Wamekuwa wanaweka malengo madogo yanayoendana na kile wanachofanya kwa sasa.
Ni rahisi kuona kwamba kuweka malengo madogo ni kuzuri kwako, lakini hili linakuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa ambayo yapo ndani ya uwezo wako. Kwa kuweka malengo ambayo hayakusukumi ufanye zaidi ya unavyofanya sasa, malengo yoyote unayoweka huwezi kuyafikia, na hata ukiyafikia hayatakuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya maisha yako.
Ufanye nini ili kuepuka mambo hayo matano na kuweza kuweka malengo makubwa na utakayoyafikia?
Kuna mambo mengi muhimu ambayo unahitaji kuyajua kuhusu uwekaji wa malengo. Na kuna hatua ambazo ni lazima uzipitie katika uwekaji wa malengo kama unataka kufikia malengo hayo.
Tarehe 04/01/2016 tutaanza semina yetu ya 2016 NI MWAKA WANGU. Katika semina hii tutajifunza malengo matano muhimu kwa kila mmoja wetu kuyaweka, na pia hatua za kuweka malengo hayo ili kila mmoja wetu aweze kuyafikia.
Utaweka malengo hayo bila ya kuwa na hisia na utayaweka baada ya kujijua wewe vizuri, kujua unaweza nini na kujua unataka nini. Pia utayachambua malengo yako vizuri kiasi kwamba utakachohitaji ni kuanza kuchukua hatua tu. Kitu kingine muhimu ni kwamba utayaandika malengo yako kwa usahihi ili uweze kuwa unayapitia kila siku.
Yote hayo utayafanya wewe mwenyewe kwa msaada wa karibu kutoka kwa mimi kocha wako. Hii ni semina ambayo itafanyika kwa njia ya mtandao na mafunzo yanatumwa kwa njia ya email, na pia kutakuwa na kundi la wasap ambapo tutakuwa tukijadiliana mambo muhimu kuhusu semina hii.
Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii muhimu sana kwako, unahitaji kulipa ada ya semina ambayo ni tsh elfu 20. Malipo yanafanyika kwa namba zifuatazo; MPESA 0755 953 887 na TIGO PESA au AIRTEL MONEY 0717 396 253. Ukishafanya malipo ya semina fungua maandishi haya na jaza taarifa zako na tayari unakuwa umejiandikisha kwenye semina hii muhimu. Na kama tayari ulishajiunga, fanya malipo yako sasa ili ujihakikishie kushiriki mafunzo haya.
Mwisho wa kujiunga na semina hii ni jumamosi ya wiki hii tarehe 02/01/2016, baada ya hapo hutaweza tena kujiunga na utakuwa umepoteza nafasi hii nzuri sana kwako kujifunza. Kama unapenda kuweka malengo ambayo utayafikia kwa mwaka 2016 basi hakikisha unajiandikisha kwenye semina hiyo leo ili ujihakikishie nafasi ya ushiriki.
Nakutakia kila la kheri kwenye mwaka 2016, ukawe mwaka wako wa kufanya mapinduzi makubwa kwenye maisha yako. Na usichelewe kujiunga na semina hii ambayo itakuwezesha wewe kufikia hilo.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

One thought on “Sababu Tano Zinazokuzuia Kufikia Malengo Yako Ya Kila Mwaka Na Jinsi Ya Kuepuka Hilo 2016.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: