Habari za wakati huu mwanamafanikio?
Napenda kutoa taarifa kwamba kipengele cha BIASHARA LEO ambacho kinatoa makala fupi kuhusu mambo ya biashara kinarudi tena. Baada ya muda wa kutokuwepo kwa kipengele hiki, sasa kinarudi tena hewani.
Kila siku kutakuwa na makala fupi kuhusu biashara kupitia kipengele hiki.
Katika makala hizi tutaangalizia kwenye maeneo yafuatayo;
1. Changamoto za kibiashara.
2. Mbinu za masoko na kitangaza biashara.
3. Kupata na kuboresha wazo la biashara.
4. Usimamizi mzuri wa muda na fedha kwenye biashara.
5. Makosa madogo madogo tunayofanya kwenye biashara zetu kila siku.
Makala hizi zitakuwa za kijifunza na kuchukua hatua.
Ili kuhakikisha tunajifunza kwa kina na tunapata maarifa bora ya kibiashara, tafadhali weka maoni, swali au changamoto ya kibiashara unayotaka tuigusie kwa kuweka maoni chini ya makala yoyote ya kipengele hiki utakayoisoma.
Karibu sana tujifunze kwa pamoja.
Changamoto kubwa kwangu ni kuhusu malengo ya kuongeza faida,kipato pamoja na Wateja
Hapo ndo najikuta naanguka sana
LikeLike
Sawa, tutajadili hili kwenye makala hizi za biashara leo.
LikeLike
Ahsante coach na nashauri tuanze na mada ya 4; kusimamia muda na fedha kwenye Biashara.
LikeLike
Sawa, tutajadili yote hayo kwenye makala hizi za BIASHARA LEO.
LikeLike