Siku za nyuma biashara zilikuwa zinatangazwa kwa sifa za biashara hizo, lakini sasa hivi mambo yamebadilika, badala ya kutangaza biashara kwa ubora wake, sasa hivi biashara zinatangazwa kwa kile zinachofanya.

Mteja hataki kusikia biashara yako inatumia teknolojia gani ya tofauti, mteja hataki kusikia biashara yako imemshinda nani na nani.

Anachotaka kusikia mteja ni jinsi gani biashara yako inamsaidia yeye kutatua matatizo yake. Na hivyo mara zote unapopata nafasi ya kuongea na mteja au mtu yeyote kuhusu biashara yako, gusia zaidi yale matatizo ya wateja ambayo biashara yako inayatatua.

Mteja ana maumivu yake na anachotaka ni yatatuliwe na awe kwenye hali bora zaidi.

Kwa mfano kama una maumivu ya jino, huhitaji kusikia sijui ni kifaa gani kipya kimegunduliwa cha kutoa meno, unachotaka kusikia ni kwamba maumivu hayo yanaweza kuondolewa au jino hilo kung’olewa.

Yajua maumivu ya wateja wako na izungumzie biashara yako kwa maumivu hayo.

Mteja hataki kusikia biashara yako ina nguvu kiasi gani, anachotaka kusikia ni tatizo lake linaweza kutatuliwa kupitia biashara yako.

MUHIMU; Kama una swali, maoni au changamoto yoyote ya kibiashara, weka kwenye maoni hapo chini na tutajadiliana zaidi na kama itahitajika nitaandaa makala ya kuhusu jambo hilo kwenye makala zijazo.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz