Ili kuwa na maisha bora na yenye mafanikio unahitaji kuwa na uhuru. Lakini uhuru siyo kitu kimoja, kuna uhuru chanya na uhuru hasi.
Uhuru hasi ni pale ambapo unapata nafasi ya kuondoka kwenye hali ambayo ni kandamizi kwako. Kupata uhuru wa kuondoka chini ya wengine, kuwa huru kupanga mambo yako bila ya kuzuiliwa na wengine. Huu ni uhuru mzuri ambao unakuwezesha kuondoka kwenye ukandamizi na kuyasimamia maisha yako mwenyewe.
Uhuru chanya ni pale ambapo unachagua kufanya kile ambacho unataka kufanya. Ni uwezo wako wa kutumia fursa zinazokuzunguka katika kupata kile ambacho unakitaka. Kwa uhuru chanya unachukua hatua kwa sababu ndiyo kitu unataka na siyo kwa sababu unaepuka hali fulani. Huu ni uhuru bora zaidi kwa sababu ndiyo unaokufikisha kwenye mafanikio makubwa.
SOMA; FALSAFA MPYA YA MAISHA; Changamoto Za Kuondoka Kwenye Vifungo Vya Maisha Na Kupata Uhuru Wa Maisha.
Aina zote za uhuru ni nzuri, lakini unahitaji kuwa na uhuru chanya zaidi ili uweze kufanikiwa. Kwa sababu uhuru hasi unakuondoa kwenye utumwa wa wengine, lakini uhuru chanya ndiyo unaokufikisha mbali zaidi.
Haitoshi tu wewe kuondoka kwenye utumwa wa wengine, haitoshi tu kusema umeondoka kwenye ajira kwa sababu inakunyima uhuru, bali unahitaji kuanzisha mpango wa maisha yako, unahitaji kufanya kile ambacho unapenda kufanya. Kuondoka kwenye kazi usiyoipenda unaweza kuwa umejipa uhuru, lakini kama utaenda kuifanya kitu usichopenda tena utakuwa umejiingiza kwenye utumwa mwingine.
Uhuru hasi ni hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye maisha huru, uhuru chanya ni kuwa na uhuru kamili wa maisha yako, ambapo unachofanya kinatoka ndani yako kweli na hakuna msukumo chanya au hasi wa wengine.
TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)