Even after a bad harvest there must be sowing. – Lucius Annaeus Seneca

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KINACHOFUATA BAADA YA MAVUNO MABAYA…
Ni kupanda.
Haijalishi mavuno yamekuwa mabaya kiasi gani, mkulima lazima apande tena.
Na hii ndiyo inamfanya aitwe mkulima, kwa sababu analima, bila ya kujali nini kinatokea.

Iwapo baada ya mavuno mabaya mkulima atasema sipandi tena kwa kuwa mazao niliyopata siyo mazuri, unafikiri ataendelea kuwa mkulima?

Kadhalika kwenye chochote tunachofanya, hata baada ya vikwazo na changamoto, tunapaswa kuendelea kufanya yale tunayofanya.
Endelea kufanya kazi yako, endelea kufanya biashara yako, changamoto na vikwazo visiwe mwisho wako wa kufanya.

Ukawe na siku bora sana leo, siku ya kufanya licha ya changamoto na vikwazo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha