Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari SIYO MUDA UNAOFANYA, BALI KIASI UNACHOFANYA…
Kwenye eneo la kazi, watu wamekuwa wanajidanganya sana.
Utawasikia watu wanasema nipo bize kweli, nafanya kazi masaa mengi sana kwa siku.
Lakini unapochukua hatua ya kuiangalia siku yake kwa umakini, unagundua muda mwingi hatumii kufanya kazi, bali anautumia kutoroka kazi.
Anatoroka kazi kwa kufanya vitu ambavyo havina matokeo yoyote kwenye kazi yake.
Wakati mwingine anachofanya siyo kazi, bali maandalizi ya kazi.
Na wanaoongoza kwa kujidanganya kwenye kazi ni wale walioajiriwa, ambayo kwenye masaa nane ya siku ya kazi, ukiangalia kwa kina, utagundua masaa hasa aliyofanya jazi hayazidi masaa mawili.
Muda mwingine unakuta ameupotezea kwenye vikao, kujiandaa kwenda kwenye chai, kupata chai, kurudi kwenye chai, kujiandaa kwenda kwenye chakula, kula na kupiga soga na wengine, kurudi kwenye kazi na hatimaye kujiandaa kumaliza kazi.
Mtu anachoka kweli, lakini ukipima alichozalisha, ni kidogo mno.
Rafiki, usipime kazi yako kwa muda uliofanya kazi, bali kwa thamani uliyozalisha, kwa kiasi ulichofanya.
Na nikupe kipimo rahisi kwako kutumia.
Unapokuwa kwenye kazi, kabla hujafanya chochote jiulize je hichi kinaingiza fedha kwenye kazi ninayofanya? Kama jibu ni hapana usikifanye.
Ni hivyo tu, unapopanga muda wako wa kazi, fanya vile vinavyoingiza fedha tu.
Vingine vyote achana navyo, ni usumbufu, ni kutoroka kazi, ni kujidanganya.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kufanya kazi kweli na siyo kutoroka kazi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha
asante sana Kocha kwa Tafakari ya leo!!! hakika naendelea kujifunza na kubadili fikra katika maisha yangu……
naomba unisaidie katika hili..
mm ni mwanafunzi nko level ya elimu ya juu(degree ya pili)
katika kazi zangu najitahidi sana kuweka juhudi, kuendana na mda ila naona kama sitimizi kwa wakati.. je kuna sehemu nakosea au ndo uwezo wangu huo???????
LikeLike
Inawezekana kwa namna unavyitumia muda wako na vipaumbele vyako hauko sawa.
Soma kitabu nilichoandika cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA na utajifunza njia bora za kutumia muda wako.
LikeLike
asante sana Dr.
LikeLike
Karibu Kabyazi,
Inawezekana kuna eneo unakosea, hebu fanya tathmini ya juhudi zote unazochukua, je zote ni muhimu kufika kule unakotaka kufika?
Kwa sababu inawezekana unaweka juhudi kubwa kwenye maeneo ambayo siyo muhimu.
Jikumbushe sheria ya Pareto, yaani 80/20 rules, kwamba asilimia 20 ya juhudi unazoweka ndiyo zinazalisha asilimia 80 ya matokeo.
Jua yale maeneo muhimu na kazana na hayo, utaona matokeo bora zaidi.
LikeLike
asante sana Kocha..
LikeLike