Rafiki yangu mpendwa,

Kwa wasomaji wa AMKA MTANZANIA kumekuwa na utaratibu wa kupokea mafunzo moja kwa moja kwenye email yako.

Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri, utagundua kwa siku kadhaa hujaweza kupokea makala za AMKA MTANZANIA moja kwa moja kwenye email yako kama ambavyo umekuwa unazoea kupokea.

Hiyo yote ni kwa sababu mfumo wa email tuliokuwa tunatumia umepata changamoto ambayo imepelekea nishindwe kukutumia email kama ambavyo nimekuwa nafanya.

Changamoto hii imetokana na kuwepo kwa watu wengi waliojiandikisha kupokea email za makala, lakini email zinatumwa na hawafungui kusoma.

Na pia wapo wengine ambao wanafungua na kusema kwamba email hizi siyo nzuri kwao.

vitabu softcopy

Hivyo nimetengeneza mfumo mpya wa kutuma email na zitakwenda kwa wale wanaotaka kupokea email hizo pekee.

Kama unataka kuendelea kupokea mafunzo ya Kocha Dr Makirita Amani moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA HAPA NA JAZA FOMU ITAKAYOFUNGUKA kisha bonyeza kujiunga.

Kwa wale watakaojiunga ili kupokea mafunzo kwa email tegemea yafuatayo;

Nitakuwa nakutumia email mara mbili kwa wiki, alhamisi na jumapili.

Email nitakazokuwa nakutumia zitakuwa na makala ambazo hazipo kabisa kwenye AMKA MTANZANIA, lakini pia nitaambatanisha viungo vya makala zilizopo kwenye AMKA MTANZANIA ambazo huenda bado hujazisoma kama ukumbusho.

Kwenye kipindi ambacho natoa huduma fulani kama semina, tarehe ya mwisho inapofika nitakutumia email nyingi zaidi kukukumbusha ili usikose nafasi nzuri ya kujifunza.

Ni hayo tu rafiki yangu, kama utapenda tuendelee kuwa pamoja karibu.

MUHIMU; Mfumo wa sasa wa email una gharama mara tatu ya mfumo wa mwanzo. Lakini haitakugharimu chochote kupokea email hizi. Gharama ninayoomba kwako ni moja tu, fungua na usome email. Kama umejiunga na kwa mwezi mzima hujafungua email yoyote, utaondolewa kwenye mfumo huu na hutaweza tena kupokea mafunzo ninayotuma kwa email.

Karibu sana rafiki yangu tuendelee kuwa pamoja.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha