Rafiki yangu mpendwa,

Mwaka 2017 nilishirikisha makala ya uchambuzi wa kitabu kilichoitwa HANDBOOK OF EPICTETUS ambacho kinatokana na mafundisho ya mwanafalsafa wa Ustoa aliyeitwa Epictetus. Kitabu hicho kinatupa mwongozo wa maisha bora, yenye furaha na mafanikio kutoka kupitia falsafa ya Ustoa.

ustoa 1

Uchambuzi ule ulipendwa na watu wengi sana, huku wengi wakishirikisha mafunzo yale kwa wengine na kuonesha nia ya kupenda kujifunza zaidi kuhusu falsafa hii, ambayo moja ya faida zake ni kumwezesha mtu kudhibiti hisia zake na kufanya maamuzi sahihi kwa kufikiri.

Kwa kuona utayari huo wa watu kujifunza, nilianzisha kundi maalumu la wasap la wale wanaopenda kujifunza falsafa hii, lakini sharti la kujiunga na kundi hilo ilikuwa ni usome kwanza kitabu cha ustoa, ushirikishe yale uliyojifunza na hapo unapata nafasi ya kujiunga. Wengi walionesha nia ya kupenda kujifunza, lakini wachache ndiyo walisoma kitabu, kushirikisha na kupata nafasi ya kujiunga.

Lakini kadiri siku zinavyokwenda, bado watu wengi wanakutana na makala ile na kuomba nafasi ya kujifunza falsafa ya Ustoa, ambayo ni moja ya falsafa bora sana inayoweza kumsaidia mtu kwenye changamoto za maisha ya zama hizi.

Baada ya kufikiri kwa kina tunawezaje kuwasaidia wengi kujifunza falsafa hii, nilipata wazo la kuwakusanya pamoja watu ambao tumekuwa tunajifunza falsafa hii kwa muda, na ambao tunaweza kuandaa makala za mafunzo ya falsafa hii ambazo zitaeleweka na wengi wanaopenda kujifunza falsafa hii.

Na hapo ndipo umezaliwa mtandao wa FALSAFA YA USTOA TANZANIA.

Huu ni mtandao ambapo utapata nafasi ya kujifunza kuhusu falsafa ya Ustoa na jinsi ambavyo unaweza kuitumia kwenye maisha yako ya kila siku, ukawa na maisha tulivu na yenye mafanikio makubwa.

Falsafa ya ustoa inalenga kutufundisha kuishi kwa kanuni za asili na kufanya maamuzi kwa fikra zetu na siyo hisia zetu. Kwa zama tunazoishi sasa, ambapo hisia zimekuwa zinawatawala wengi, ni muhimu sana kuwa na falsafa inayokuongoza. Na falsafa bora ambayo naona inawafaa wengi ni Ustoa.

Tumeanzisha mtandao utakaokuwa unatoa mafunzo haya ya falsafa ya ustoa, mtandao huo unapatikana kwa anwani www.ustoa.or.tz

Tembelea mtandao huo kila siku na utaweza kujifunza kuhusu falsafa hii ya Ustoa na jinsi ya kuitumia kuzivuka changamoto mbalimbali za maisha.

Mtandao huu unaendeshwa na waandishi watatu, ambao ni Dr Makirita Amani, Dr. Raymond Mgeni na Mwl. Deo Kessy. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu waandishi hao na safari yao kwenye falsafa ya ustoa kwa kufungua viungo hivi; www.ustoa.or.tz/makirita , www.ustoa.or.tz/mgeni na www.ustoa.or.tz/kessy

Kujifunza kuhusu falsafa ya ustoa, misingi yake, wanafalsafa ambao wameifundisha na kuikuza fungua; https://ustoa.or.tz/kuhusu-mtandao-huu/kuhusu-falsafa-ya-ustoa/ na https://ustoa.or.tz/kuhusu-mtandao-huu/wanafalsafa-wa-ustoa/

Kujifunza jinsi unavyoweza kuitumia falsafa ya ustoa kwenye maisha yako ya kila siku na kukabiliana na changamoto mbalimbali, fungua https://ustoa.or.tz/misingi-minne-ya-ustoa/ na https://ustoa.or.tz/maisha-ya-kistoa/

Kupakua bure kabisa vitabu vya msingi vya falsafa hii, fungua; https://ustoa.or.tz/maktaba-ya-ustoa/

Kujiunga na kundi la telegram la mtandao huu wa falsafa ya ustoa, ambapo utaweza kupata vitabu, kuuliza maswali na kupata majibu, fungua; https://t.me/ustoatz

Kupokea moja kwa moja mafunzo ya ustoa kwenye email yako, unaweza kujiunga na mfumo wetu wa email kwa kufungua; http://eepurl.com/gETVMf

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye mtandao huu wa FALSAFA YA USTOA TANZANIA.

Waandishi wote watatu tumejitoa kuhakikisha zile faida ambazo sisi tumezipata kwa kujifunza na kuishi falsafa hii, na wewe pia unazipata.

Mtandao huu unaendeshwa kwa kuegemea kwenye kazi za wanafalsafa wa tatu, na kila mwandishi atabobea kwa mwanafalsafa mmoja wa ustoa, hivyo kuwa na wigo mpana wa kufundisha.

Dr. Makirita Amani ataandika na kufundisha kutokana na mafundisho ya mwanafalsafa Seneca.

Dr. Raymond Mgeni ataandika na kufundisha kutokana na mafundisho ya mwanafalsafa Marcus Aurelius.

Mwl. Deo Kessy ataandika na kufundisha kutokana na mafundisho ya mwanafalsafa Epictetus.

Kwa pamoja, timu hii ya watu watatu, tutahakikisha kila anayetembelea mtandao huu anaondoka na maarifa sahihi na hatua za kwenda kuchukua ili kuyafanya maisha yake kuwa bora zaidi.

Nikutakie kila la kheri katika kujifunza na kuiishi falsafa hii ya Ustoa ili kuwa na maisha tulivu na bora.

Rafiki na kocha wako,

Dr Makirita Amani,

www.ustoa.or.tz/makirita

makirita@ustoa.or.tz