Rafiki yangu mpendwa,

Kitu kimoja kikubwa ninachoshukuru sana ni uwepo wako wewe kwenye maisha yangu. Wewe ndiye ambaye umekuwa unanisukuma kuandaa maarifa bora sana yanayokuwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Bila ya uwepo wako kazi zangu zisingekuwa na maana, ndiyo maana kila wakati huwa nakushukuru kwa namna ambavyo umeendelea kuwa pamoja na mimi. Nina imani kuna kitu kikubwa unachokipata ndiyo maana tunaendelea kuwa pamoja.

Katika jitihada hizi za kukushirikisha maarifa bora yatakayokuwezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako, kila mwaka nimekuwa naandaa semina moja kubwa ya kukutana ana kwa ana.

semina 2017 4

Semina hii ni kubwa kwa sababu inawakusanya watu kutoka nchi nzima ya Tanzania, watu wanasafiri kutoka maeneo mbalimbali na kuja kushiriki mafunzo haya ambayo yanatokea mara moja tu kwa mwaka.

Semina hii pia ina nguvu kubwa sana ya kujifunza na kupata hamasa kutokana na mafunzo bora pamoja na shuhuda mbalimbali ambazo watu wanashirikisha. Unaposhiriki semina hizi unaona jinsi ambavyo wengine wameweza kupiga hatua kubwa kwa kuanzia chini kabisa, hivyo wewe unakuwa huna cha kukuzuia.

Kwa mwaka huu 2019, semina yetu hii ya mwaka itafanyika jumapili ya tarehe 03/11/2019 jijini Dar Es Salaam. Itakuwa ni semina ya siku nzima, kuanzia saa moja kamili asubuhi mpaka saa moja kamili usiku. Yatakuwa ni masaa 12 ya kupata dozi zote unazohitaji ili kuondoka na maarifa na hamasa ya kukusukuma kwa mwaka mzima

Ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii kubwa, unapaswa kutoa taarifa ya kuthibitisha ushiriki wako na pia kulipa ada kabla ya tarehe 31/10/2019.

Taarifa ya kuthibitisha unaituma kwa ujumbe wenye majina yako kamili na namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki semina. Ujumbe huo unatumwa kwenda namba 0717396253.

Ada ya kushiriki semina hii ni tsh laki moja (100,000/=) ambayo itagharamia kila kitu kwenye semina hii, kuanzia chai ya asubuhi, chakula cha mchana, chai ya jioni, vinywaji, vijitabu vya kuandikia, kalamu na vingine vinavyohusika kwenye semina. Ada hii inapaswa kulipwa mpaka kufikia tarehe 31/10/2019. Ada inalipwa kwa Mpesa 0755 953 887 au tigo pesa/airtel money/mobile bank kwenda namba 0717 396 253. Ukituma ada ya kushiriki tuma ujumbe wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia semina.

Rafiki, zimebaki wiki mbili pekee kwako wewe kupata nafasi ya kushiriki semina hii kubwa sana kwa mwaka huu 2019, semina ambayo haitajirudia tena kwenye mwaka huu, semina ambayo utajifunza na kuhamasika sana na kuondoka na nguvu ya kwenda kufanya makubwa zaidi kwenye maisha yako. Usipange kabisa kukosa semina hii, kwa sababu ni kitu cha mara moja pekee.

Hatua ya kuchukua leo; kama bado hujathibitisha kushiriki semina, fanya hivyo leo, tuma ujumbe kwenye majina yako na maelezo kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253.

Pia kamilisha malipo ya ada ya kushiriki semina hii, ili uwe na uhakika wa kujumuika pamoja na sisi kwenye semina hii kubwa ya mwaka, tujifunze, kuhamasika na kuondoka na nguvu za kwenda kuchukua hatua kubwa.

Naamini tarehe 03/11/2019 tutakuwa pamoja rafiki yangu, chukua hatua sasa ili usiikose nafasi hii adimu.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,