“People aren’t in awe of your sharp mind? So be it. But you have many other qualities you can’t claim to have been deprived of at birth. Display then those qualities in your own power: honesty, dignity, endurance, chastity, contentment, frugality, kindness, freedom, persistence, avoiding gossip, and magnanimity.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.5
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii mpya tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari ONESHA UBORA ULIONAO…
Hakuna binadamu aliyekamilika,
Kila mmoja wetu kuna udhaifu fulani anao, kuna kitu fulani amekikosa, ambacho kama angekuwa nacho maisha yake yangekuwa vizuri.
Lakini kinachokuzuia wewe kupiga hatua siyo ulichokosa, bali kushindwa kutumia vizuri kile ulichonacho.
Licha ya kukosa vitu fulani ulivyotamani sana kuwa navyo, bado una tabia nyingine bora kabisa unazoweza kujijengea na maisha yako yakawa bora sana.
Huenda umezaliwa ukiwa mfupi sana au mrefu sana au una kigugumizi au mweusi sana au mweupe sana. Hizo zote ni hali ambazo zinaweza kuwa na kikwazo kwako kwa namna moja au nyingine, na huna namna ya kuzibadili.
Lakini vitu hivyo ulivyokosa, havikuzuii wewe kujijengea tabia bora kabisa na zitakazokuwa na msaada kwako na kukuwezesha kupiga hatua.
Unaweza kuchagua kuwa mkweli,
Unaweza kuchagua kuwa mwaminifu,
Unaweza kuchagua kuwa mwema,
Unaweza kuchagua kuwa mvumilivu,
Unaweza kuchagua kuwa na furaha,
Unaweza kuchagua kuwa mtu wa kujali,
Unaweza kuchagua kuepuka majungu,
Unaweza kuchagua kuwa huru.
Zote hizi ni tabia bora kabisa unazoweza kujijengea na ukawa mtu bora kabisa bila ya kuhali ni udhaifu gani ambao umezaliwa nao.
Chagua leo kuwa mtu bora na kuonesha tabia zilizo bora na ulichokosa hakiwezi kuwa kikwazo kwako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya leo kujijengea tabia bora ambazo zitakufanya wewe kuwa bora kabisa licha ya mapungufu unayoweza kuwa nayo.
#HakunaAliyekamilika #JijengeeTabiaBora #TumiaVizuriUlichoNacho
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1
Asante sana kwa ujumbe mzuri.
LikeLike
Karibu.
LikeLike