Rafiki yangu mpendwa,
Ni imani yangu kwamba unaendelea vyema na mapambano ya kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora na unafanikiwa zaidi. Hongera sana kwa hilo.
Kama ambavyo nimekuwa nakupa taarifa, toleo la pili la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA limeshatoka.
Hiki ni kitabu ambacho kinakupa mwongozo sahihi wa kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa.
Kitabu hiki kina mafunzo yote muhimu kuhusu kuanzisha na kukuza biashara, ambayo yanamfaa kila anayepanga kuingia au ambaye tayari yupo kwenye biashara.
MAELEZO ZAIDI KUHUSU KITABU HIKI SOMA HAPA; KITABU; Biashara Ndani Ya Ajira Toleo La Pili Oktoba 2019.
KARIBU KWENYE UZINDUZI WA KITABU.
Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye uzinduzi wa kitabu hiki cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili.
Uzinduzi utafanyika siku ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, ambayo ni jumapili ya tarehe 03/11/2019. Semina itafanyika jijini Dar es salaam.
Pamoja na uzinduzi wa kitabu hicho, ndani ya semina hii utapata mafunzo na hamasa kubwa sana itakayokuwezesha kupiga hatua na kufanikiwa zaidi. Semina hii ni ya siku nzima, kuanzia saa 1 asubuhi mpaka saa 1 usiku. Utapata mafunzo ya mafanikio, na shuhuda mbalimbali kutoka kwa wale waliochukua hatua na kupata mafanikio.
Ili kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 pamoja na kupata uzinduzi wa kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, unapaswa kulipa ada ya kushiriki ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Ada inalipwa kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 ukishalipa ada yako tuma majina yako kamili na maelezo kwamba umelipia SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019. Mwisho wa kufanya malipo ili kupata nafasi ya kushiriki semina na uzinduzi ni tarehe 31/10/2019.
Karibu sana rafiki yangu tujumuike pamoja kwenye siku hiyo muhimu sana kwa mafanikio yetu. Chukua hatua leo ili usikose semina hii na uzinduzi wa kitabu.
KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU SEMINA FUNGUA HAPA; Karibu Kwenye Semina Ya Kisima Cha Maarifa 2019; Afya, Utajiri Na Hekima.
WANAONIDAI ZAWADI YA KITABU.
Rafiki, wakati naandaa toleo la pili la kitabu cha biashara ndani ya ajira, niliomba wale ambao walisoma toleo la kwanza na kufanyia kazi wanipe shuhuda zao jinsi ambavyo kimewasaidia. Nashukuru sana kwa mrejesho wenu marafiki, wengi walichukua hatua ya kuandika mrejesho.
Lakini pia kuna wanamafanikio mbalimbali ambao nimekuwa nawapa huduma ya ukocha ya kuziwezesha biashara zao kukua zaidi. Nao niliwaomba washirikishe mchanganuo wa biashara wanazofanya na jinsi ambavyo mtu mwingine anaweza kuanza biashara za aina hiyo. Nao pia walifanya hivyo na ninawashukuru sana.
Kutoka makundi hayo mawili, hapa kuna marafiki 16 ambao watapata zawadi ya kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA Toleo la pili, bure kabisa.
Watakaopata zawadi hiyo ni kama ifuatavyo;
- Tumaini A. Jonas,
- Sebastian Kalugulu Mbilizi,
- Godfrey M Mbise,
- Godius Rweyongeza,
- Kelvini Kinyaga,
- Priscilla Isabelle Tayari,
- Annamary Ottaru,
- Godfrey Chacha,
- Peter Vincent Balele,
- Mary Charles Kunena,
- Elia Jacob Hassani,
- Ali Khamis,
- Patrick Edgar James,
- Leonard Amo,
- Remod Kibona,
- Sebastian Moshi.
Utaratibu wa kupata zawadi hii ni zawadi itatolewa siku ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, tarehe 03/11/2019 ambapo pia ndiyo utakuwa uzinduzi wa kitabu hicho. Karibuni sana wote mjipatie zawadi hii nzuri ya kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili. Tutapata pia nafasi ya kupiga picha ya pamoja kwa sababu watu hawa 16 majina yao yapo kwenye kitabu kwenye shuhuda zao na michanganuo waliyoshirikisha.
Karibuni sana wote kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 itakayoambata na uzinduzi wa kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili. Chukua hatua mapema ili usikose nafasi hii ya kipekee inayotokea mara moja tu kwa mwaka.
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,