Rafiki yangu mpendwa,
Leo nina ujumbe mfupi sana kwako wa kukukumbusha kuhusu tukio letu kubwa la SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019. Hii ni semina inayofanyika mara moja kila mwaka na kuwakusanya pamoja wanamafanikio kutoka kila kona ya Tanzania. Ni semina ambayo ukishiriki unaondoka na mikakati, mbinu na hamasa za kwenda kuchukua hatua zaidi ili kufanikiwa.
Kwa mwaka huu 2019, semina hii itafanyika jumapili ya wiki hii, tarehe 03/11/2019, jijini Dar Es Salaam. Lakini ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kuwa umelipa ada yako ya ushiriki mpaka kufikia tarehe 31/10/2019, ambayo ni kesho. Hivyo una siku moja pekee ya kukamilisha ulipaji wa ada na uweze kujumuika nasi kwenye tukio hili kubwa na la kipekee.
Ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 ni tsh laki moja (100,000/=) na inalipwa kwa namba zifuatazo; 0717 396 253 au 0755 953 887 majina ya namba zote ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma ada ya kushiriki, tuma ujumbe wenye majina yako na namba ya simu na kwamba umelipia semina ya KISIMA CHA MAARIFA.
Mwisho wa kulipia ili upate nafasi ni kesho tarehe 31/10/2019.
Nikushirikishe siri moja muhimu rafiki yangu, siku nzuri kwako kufanya malipo ili usikose nafasi hii ni leo tarehe 30/10/2019. Hii ndiyo siku unayoweza kulipa bila ya usumbufu wowote. Watu wengi huwa wanasubiri mpaka siku ya mwisho kufanya malipo, sasa inapotokea watu wengi wanalipia kwa pamoja, au siku hiyo mtandao ukasumbua, basi wanasumbuka sana.
Jiepushe na usumbufu huu kwa kufanya malipo yako leo, siku moja kabla ya tarehe ya mwisho ya kulipia semina hii.
Kama hukupata taarifa kamili za semina hii, ni kwamba semina ya mwaka huu itakuwa ya tofauti na ya miaka ya nyuma.
Mwaka huu utasikia zaidi kutoka kwa wafanyaji na hatua walizopiga, hivyo utajifunza na kupata hamasa ya kupiga hatua na wewe pia. Tutajifunza kutoka kwa mwenzetu aliyeweza kuongeza wateja na mauzo kwenye biashara yake mara tano zaidi. Tutajifunza jinsi wenzetu wanaweza kuendesha biashara na ajira kwa wakati mmoja na jinsi wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali. Tutajifunza kuhusu mahusiano, maisha ya mafanikio na namba muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.
Muhimu zaidi, kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, utajiwekea lengo moja ambalo utawashirikisha wengine na kulifanyia kazi kwa mwaka mzima huku ukishirikisha maendeleo yako kila mwezi.
Nakazana sana upate thamani kubwa kwenye semina hizi, kwa sababu najua unawekeza fedha na muda mwingi kushiriki semina hii, napenda mwaka kesho tunapokutana tena, utuoneshe alama ya jinsi semina ya 2019 imeleta mabadiliko kwenye maisha yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, kamilisha malipo yako leo tarehe 30/10/2019 ili uepukane na changamoto zinazoweza kujitokeza siku ya mwisho ya kulipia.
Nina imani tutakuwa pamoja kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, nakusubiri kwa hamu ili tuweze kushirikishana yale muhimu na uende ukachukue hatua na maisha yako yawe bora zaidi.
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr. Makirita Amani,