Rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa nimekuwa nakupa taarifa kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 ambayo inakwenda kufanyika jumapili hii ya tarehe 03/11/2019. Hii ni semina ya kipekee ambayo inawakusanya pamoja wapenda mafanikio wote kutoka kila kona ya Tanzania.

Leo napenda nikukumbushe kwamba tumefika siku ya mwisho kupata nafasi ya kushiriki semina hii. Leo tarehe 31/10/2019 ndiyo siku ya mwisho kwako kupata nafasi ya kushiriki semina hii. Hivyo kama bado hujachukua hatua, fanya hivyo sasa ili uweze kujumuika nasi na kujifunza pamoja na kuhamasika ili kwenda kuchukua hatua kubwa na kufanikiwa zaidi kwenye mwaka wa mafanikio 2019/2020.

SEMINA KISIMA CHA MAARIFA 2018 029.JPG

Ili kupata nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, unapaswa kulipa ada ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Malipo yanafanywa kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishafanya malipo, tuma ujumbe wenye majina yako kamili na namba ya simu na maelezo kwamba umelipia semina.

Ukishafanya malipo ya kushiriki semina, utaunganishwa kwenye kundi maalumu la wasap la semina hii ambapo utapata taarifa zote kamili kuhusu semina.

Rafiki, kila mara nimekuwa nakusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua kama kweli unataka kufanikiwa zaidi. Hivyo ni wakati wa kuchukua hatua sasa, ili usikose nafasi hii ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.

DSC_0093.JPG

Kama leo utachagua kuikosa semina hii, maana yake umechagua kukosa vitu hivi kumi vyenye manufaa makubwa kwako.

  1. Utakuwa umekosa nafasi ya kujifunza UTATU WA MAISHA YA MAFANIKIO, dhana muhimu sana kwako itakayokuwezesha kuishi maisha ya mafanikio na yasiyotetereka. Lakini pia utakosa nafasi ya kuongeza kipato chako zaidi kwa mwaka 2020 maana moja ya masoko nitakayofundisha kwenye semina hii linaitwa KIPATO ZAIDI 2020, hapa utapata nafasi ya kujiwekea lengo la kipato na kulifanyia kazi kila mwezi huku ukishirikisha maendeleo yako kila mwezi. Kwa hatua hiyo tu, utasukumwa kuchukua hatua zaidi.
  2. Utakosa nafasi ya kujifunza kuhusu CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO na jinsi ya kuzitatua. Kama tunavyojua, mahusiano yetu yana mchango sana kwenye mafanikio yetu. Hamisi Msumi ametuandalia somo zuri mno kwa upande huu wa mahusiano.
  3. Utakosa nafsi ya kujifunza kuhusu NAMBA MUHIMU ZA KIBIASHARA na jinsi ya kuzitumia kwa ukuaji wa biashara yako. Hafidhi Ali, atatushirikisha somo hili muhimu, na kutuonesha jinsi ya kuzitumia namba za biashara vizuri.
  4. Utakosa nafasi ya kujifunza jinsi Isaack Zake alivyokuwa ameandika vitabu na kushindwa kuvichapa kwa miaka miwili, lakini akapata msukumo na nguvu ya kuchapa vitabu viwili ndani ya siku 30, pamoja na kuwafikia wateja wapya 191 ndani ya siku 30, kitu ambacho alishindwa kukifanya kwa karibu mwaka mzima. Hapa utajifunza jinsi na wewe unavyoweza kuacha kuahirisha mambo na kuchukua hatua mara moja.
  5. Utakosa nafasi ya kujifunza jinsi ambavyo Donard Msanga alivyoweza kukuza biashara yake kwa kuongeza wateja kutoka 10 mpaka 50 na mauzo kutoka tsh 400,000/= mpaka tsh 1,600,000 ndani ya mwaka mmoja, ukuaji mkubwa mno kwenye biashara. Hapa utajifunza jinsi na wewe unavyoweza kukuza biashara yako kwa kiwango kikubwa.
  6. Utakosa nafasi ya kujifunza jinsi Sebastian Kalugulu anavyoweza kuendesha miradi mbalimbali huku akiwa bado ni mwajiriwa. Anaweza kuendesha miradi ya ufugaji wa kuku, nguruwe na hata samaki, huku akiwa na biashara ya gari la mizigo na ajira yake akiwa anaendelea nayo. Hapa utajifunza jinsi unavyoweza kufanya miradi tofauti kwa pamoja.
  7. Utakosa nafasi ya kujifunza jinsi Leonard Amo alivyokuwa akisumbuka na hasara kwenye biashara yake pamoja na kuahirisha mpango wa ukuaji, lakini ndani ya siku 30 akaweza kupunguza sana hasara na kuikuza biashara yake kwa kufungua ofisi mpya na kuongeza wafanyakazi, huku kipato kikiongezeka kwa kiwango kikubwa. Hapa utajifunza jinsi unavyoweza kupiga hatua kubwa na kutoka pale ulipokwama sasa.
  8. Utakosa nafasi ya kujifunza jinsi Godius Rweyongeza alivyoweza kuanza ujasiriamali pamoja na uandishi wakati akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu, na sasa amehitimu akiwa na mtazamo tofauti kabisa na wahitimu wengine. Hapa utajifunza huna sababu ya kusema huwezi kupiga hatua.
  9. Utakosa nafasi ya kujifunza jinsi Mary Kunena alivyoweza kuanzisha biashara yake na anavyoweza kuiendesha licha ya ajira yake kumbana kwa kuchukua muda wake mwingi. Hapa utajifunza hata kama ajira inakubana, bado unaweza kuwa na biashara ya pembeni.
  10. Utakosa nafasi ya kujifunza jinsi Elia Hassan alivyoweza kuanza biashara ya kupika karanga kwa mtaji kidogo mno (elfu 5) na kuweza kuikuza mno kiasi cha kuweza kupata faida ya mpaka elfu 30 kwa siku. Kutoka kuuza karanga kilo mbili kwa siku mpaka kilo 12 kwa siku. Hapa utajifunza kwamba kama unasema huna mtaji wa kuanza, basi unajidanganya tu, maana hakuna anayekosa elfu 5, au elfu 50 na ukaweza kuanza biashara ndogo na kuikuza.

Rafiki, kama hujawahi kufanya kazi kwa karibu na mimi (kupitia huduma za ukocha), unaweza ukawa unajiambia baadhi ya mambo hapo juu hayawezekani. Lakini nakualika uje kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, usikie shuhuda halisi, kutoka kwa watu halisi na uweze kuwauliza maswali yoyote unayotaka wewe.

Chukua hatua leo, maana ndiyo siku ya mwisho kabisa kupata nafasi ya kushiriki semina.

Kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakiomba nafasi ya kushiriki baada ya siku ya mwisho kulipia kupitia. Kwa mwaka huu hutaweza kupata nafasi hiyo, kwa sababu maandalizi yanafanyika kulingana na idadi ya wale waliolipia mpaka kufikia leo tarehe 31/10/2019.

Kama nafsi yako inakuambia hii ni semina unayopaswa kushiriki, kama inakuambia hupaswi kukosa mambo hayo kumi niliyokushirikisha hapo, basi chukua hatua sasa hivi. Fanya malipo yako ya ada ya tsh 100,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253.

Naamini tutakuwa pamoja rafiki, naamini mwaka wa mafanikio 2019/2020 utakwenda kuacha alama ya tofauti kabisa kwenye maisha yako. Fanya maamuzi sahihi leo ili uweze kunufaika sana.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,

Kocha Dr. Makirita Amani.