“The improvement of man can be measured by the level of his inner freedom. The more a person becomes free from his personality, the more freedom he has.” – Leo Tolstoy

Mafanikio yako yanapimwa kwa uhuru uliopo ndani yako.
Uko huru kiasi gani na maisha yako ndiyo inaonesha umefanikiwa kiasi gani.
Na uhuru binafsi unatifautiana baina ya watu, hivyo pia mafanikio yanatofautiana baina ya watu.

Muhimu kabisa ni kujua unapaswa kufika wapi ili kuwa huru,
Unapaswa kuwa na fedha kiasi gani ili usiwe tegemezi kwa njia za kuingiza kipato zinazotaka uwepo wako.

Ukishaujua uhuru wako na kuufanyia kazi, ni rahisi kwako kufanikiwa, kwa viwango vyako na siyo vya mtu mwingine.

Unapoimaliza siku hii, jiambie kesho ni uhuru gani unaoenda kutengeneza kwenye maisha yako.
Chagua eneo utakalofanyia kazi na chukua hatua.

Uwe na wakati mwema.
Kocha.