Kila kiongozi unayemwona yuko vizuri basi kuna eneo moja ambalo analisimamia vizuri sana.

Kiongozi kuwa bora kuna gharama yake, na kila gharama unapaswa kuilipia. Huwezi kuwa bora kama kila siku ni mtu yule yule, huchukui hatua ya kujifunza.

Akili iliyosababisha tatizo haiwezi kutumika kutatua tatizo jipya, maana yake hapa unaalikwa kuwa na maarifa mengi kila siku.

Mzizi wa uongozi ni nidhamu. Maisha ya kiongozi yoyote yanajengwa kwa nidhamu, bila nidhamu binafsi uongozi unakuwa mzigo ambao haubebeki.

Nidhamu inazaa uaminifu. Kiongozi yoyote akiwa ana nidhamu wale anaowaongoza watamuamini na kutokuwa na mashaka naye.
Na kama unavyojua uaminifu unajengwa mahali penye uhakika.

Hakuna umaarufu bila kuwa na nidhamu. Ukitaka kuwa maarufu lazima uwe na nidhamu ya kufanya kile ulichochagua kufanya bila kusimamiwa.
Bila nidhamu huwezi kuwa mtu unayejulikana kupitia kile unachofanya.

Watu wanakubalika kwa sababu ya kuuza nidhamu. Kuna viongozi wana nidhamu ya hali ya juu, ambayo wanaitumia nidhamu yao kujiuza kokote kule.

Kila mtu anafurahishwa kufanya kazi na mtu mwenye nidhamu. Kwa sababu watu wanapenda kuona mtu aliyesimama na ataweza kuwaongoza.
Kuwa mtu wa nidhamu kupitia kile unachofanya na utajiuza vizuri.

Tunawatamani watu jinsi walivyo jinsi kwa sababu ya nidhamu zao. Ukiona mtu ana nidhamu ya kufanya kazi, muda, fedha nk unavutiwa na hata kumtamani kufanya naye kazi. Ndiyo maana nilisema nidhamu inakusaidia kuuza kile unachofanya uwe kiongozi au la.

Nidhamu za viongozi ndiyo zinatufanya sisi tuwapende na kufanya nao kazi.

Hakuna mtu ambaye anavutiwa na mtu mzembe, hivyo jitahidi kuwa mtu anayewajibika na utakua rafiki wa watu makini.

Hatua ya kuchukua leo; Nidhamu ndiyo mzizi wa uongozi, nenda kaishi kwa nidhamu kwenye kila eneo la maisha yako.

Kwahiyo, kipimo cha uongozi kinaanzia katika nidhamu binafsi, kama wewe umekosa ushawishi wa kuwaonesha watu kuwa inawezekana watu hawatoweza kujituma na kuchukua hatua.

Kila la heri rafiki yangu.

Makala hii imeandikwa na

Mwl. Deogratius Kessy
ambaye ni mwalimu, mwandishi na mjasiriamali.

Unaweza kuwasiliana naye kwa namba zifuatazo 0717101505/0767101505
deokessy.dk@gmail.com

Pia, mwandishi anakualika kuweza kujifunza zaidi kupitia mtandao wake wa Kessy Deo, unaweza kuingia kwa kutumia link hii hapa http://kessydeo.home.blog

Asante sana na karibu sana.