Tunapoona wengine wamepiga hatua kuliko sisi kwenye baadhi ya maeneo, huwa tunawaonea wivu, huwa tunatamani na sisi tungekuwa tumepiga hatua ambazo wao wamepiga.
Tunafika hatua ya kutamani tungekuwa wao, na kuona sisi hakuna kikubwa tunachofanya.
Labda ni mtu mliyesoma pamoja, na labda ufaulu wako ulikuwa mkubwa kuliko wewe. Lakini yeye amepata kazi inayomlipa mshahara mara mbili wa ule ambao wewe unalipwa kwenye kazi yako.
Kitu ambacho unakosea ni unaangalia eneo moja la maisha ya mtu, huangalii maisha yao kwa ujumla.
Kwenye maisha kuna kitu kinaitwa TRADE OFF, yaani toa ili upate. Ili kupata chochote, lazima kuna kitu unapaswa kutoa, lazima kuna kitu utapoteza. Hivyo wale ambao wamepiga hatua kubwa kwenye maisha yao, kuna vitu vikubwa wametoa.
Kabla hujajiambia ungependa kuwa kama mtu fulani, jiulize kwanza ni nini amepoteza, kisha jiulize je upo tayari kupoteza kama alivyopoteza wewe.
Tukirudi kwenye mfano wa kazi, huenda rafiki yako anayelipwa mara mbili ya unacholipwa wewe, anafanya kazi muda mrefu kuliko unavyofanya wewe, hivyo analipwa zaidi, lakini hana muda wa kuishi maisha yake, hana muda wa kufanya vitu vingine vya pembeni. Lakini wewe una muda mwingi, ambao unaweza kuutumia kufanya mambo mengine nje ya kazi yako.
Rafiki, hujiambii hili ili kujiridhisha pale unaposhindwa kufanya makubwa bali unajipa picha kubwa, kwamba licha ya kwamba hujapata kile ambacho wengine wamepata, una nafasi ya kufanya kingine kikubwa zaidi, kutokana na kile ambacho wengine wamepoteza lakini wewe unacho.
Kabla hujatamani kuwa kama wengine, jiulize kwanza wamepoteza nini ambacho wewe unacho, kisha kitumie hicho kufanya makubwa zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Daa bonge la makala huu ujumbe mzito umeandika ushaur mzuri sana ahsante kocha umeniongezea kitu nakwenda kuweka ktk matendo
Ili kuku aanguliwe lazima yai liharibike
LikeLike
Karibu Hendry.
LikeLike
Asante sana kocha, nimejifunza kitu kazi kwangu
LikeLike