“A man is wise who does three things: first, he does by himself those things which he advises others to do; secondly, he does not do anything that contravenes the truth; and thirdly, he is patient with the weaknesses of those who surround him.” – Leo Tolstoy
Moja ya jukumu lako kubwa kwenye maisha ni kuwa na hekima,
Hivyo kila siku unapaswa kujifunza na kuweka kwenye matendo yale unayojifunza ili kuwa na hekima.
Na njia rahisi ya kujifunza hekima, ni kupitia wale wenye hekima.
Watu wenye hekima huwa wanafanya mambo haya matatu.
Moja; huwa wanafanya kile ambacho wanawashauri wengine wafanye.
Hekima siyo fanya kama ninavyokuambia, bali fanya kama ninavyofanya.
Kwa sababu hakuna njia bora ya kushauri au kufundisha kama wewe mwenyewe kuwa mfanyaji.
Mbili; hawafanyi chochote kinachokwenda kinyume na ukweli.
Hekima na ukweli ni vitu pacha, huwezi kuvitenganisha kwa namna yoyote ile.
Hata kwa jambo dogo na unalojiambia halina umuhimu.
Ni lazima usimamie ukweli mara zote, hata pale unapokuumiza wewe au wengine.
Na pale ukweli unapoumiza, ndiyo kipimo hasa cha hekima, kama utausimamia ukweli huo au utakwenda kinyume na ukweli.
Tatu; wanavumilia madhaifu ya wengine.
Pamoja na wao kujiwekea viwango vya juu na kujisukuma kuvifikia, wanajua wengine hawawezi kujiwekea viwango vya aina hiyo.
Hivyo wanavumilia madhaifu ya wengine, hawawategemei wawe kama wao, hawawaadhibu kama wanavyojiadhibu wenyewe.
Kuwa mvumilivu kwa wanaokuzunguka, hasa pale unapojua mtu ana nia kweli na ana kazana kadiri ya uwezo wake, lakini udhaifu wake unamkwamisha.
Lakini usivumilie wazembe, wanaojikwamisha kwa makusudi.
Fanya mambo haya matatu kwenye kila siku ya maisha yako na utajijengea hekima kwenye maisha yako.
Mambo haya siyo magumu, hayahitaji uwe na chochote cha ziada,
Bali ni wewe kufanya maamuzi na kuyasimamia, ambacho ndiyo kipimo sahihi cha hekima.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa Maneno mazito, hakika naendelea kujifunza vitu adimu Sana ndani ya Kisima cha Maarifa.
LikeLike