Nimekuwa nasema, moja ya vitu tunavyopaswa kujifunza kutoka kwenye hadithi za waliofanikiwa ni mchakato waliopitia na siyo kile ambacho wamefanya.
Wale waliofanikiwa, kama wangeanza tena kufanya walichofanya, wasingeweza kupata matokeo waliyopata sasa, lakini bado wangefanikiwa kwa kupata matokeo tofauti kwa sababu wana mchakato wanaoutumia.
Unaposikia kwamba Thomas Edison alishindwa mara elfu 10 kabla hajafanikiwa kutengeneza taa ya umeme, unachopaswa kujifunza hapo ni mchakato wa ung’ang’anizi na kuweka kazi ili kupata matokeo ambayo unayataka.
Karibu kila mtu anajua hadithi za baadhi ya waliofanikiwa, ambao walianzia chini, wakapambana na kufanikiwa.
Lakini cha kushangaza, inapokuja kwenye kuyaishi maisha yake, mtu hawezi kutumia yale aliyojifunza kutoka kwa waliofanikiwa. Mtu anajaribu kitu mara moja na kushindwa kisha anakata tamaa na kuona hawezi.
Ninachotaka kukukumbusha leo ni kitu kimoja, jipe muda wa kuweka kazi, muda ambao hutaangalia matokeo gani umepata, bali juhudi zipi umeweka. Isiwe chini ya miaka kumi na potea kabisa na uende ukaweke kazi.
Na kwa njia hiyo, utapata matokeo mazuri.
Changamoto ya zama zetu, kila mtu anataka kufanya huku akitangaza kila anachofanya kwenye mitandao ya kijamii, hivyo anaposhindwa anapata maumivu kwa sababu kila mtu anaona.
Kama ukijichimbia kwa muda, ukaweka kazi hasa, kimya kimya, baadaye matokeo yatakuja kujionesha yenyewe na hutakuwa na haja ya kupiga kelele watu waone unafanya nini.
Wewe kazana kuweka kazi, mengine yatajiweka sawa yenyewe.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Umeongea ukweli sana Dr Makirita zama hizi mtu anataka kuonekana na si kuweka ukimya kujishughulisha na mchakato wa kufanikiwa
Mtu ameanza biashara kidogo haina muda mrefu ni changa labda kabahatisha wateja wawili watatu mauzo kapata anapost mtandaoni kuonyesha kwa watu
Biashara changa ushapost karibu tukuhudumie….japo s vibaya kutangaza ila unaacha mchakato thabiti na kupoteza muda kuonyesha wengine unachofanya ngoma ni pale inapoporo nmoka sasa naushaanza kujionyesha
Mchakato unahitaji ukimya sana unahitaji kutotambulikana mapema
LikeLike
Hakika Hendry,
Mtu mmoja amewahi kunilalamikia kwamba kila akianza kitu hafiki mbali, nilipomfatilia, nikagundua anaweka kazi kubwa kwenye aonesho kuliko kwenye kile anachofanya.
Huu ni mtego ambao wengi wanatumbukia.
LikeLike
Najivunia kuwa mmoja wa familia ya kisima cha maarifa,nimelisha chakula ubongo wangu kwamba natakiwa kufanya kazi kwa bidii bila ya kuwaonyesha mimi ni nani
LikeLike
Vizuri sana Mary,
Weka kazi.
LikeLike