Kwenye moja ya mahojiano yake na watu mbalimbali waliofanikiwa, mwandishi James Altucher alikuwa anamhoji mchekeshaji na mfanyabiashara Bryon Allen ambaye alianza ujasiriamali akiwa na umri wa miaka 12.
Alipokutana na wachekeshaji maarufu, aliona hicho ndiyo kitu anachotaka kufanya kwenye maisha yake na hapo alijipa kauli ya kishujaa na iliyompa msukumo mkubwa wa kufanyia kazi ndoto yake.
Alisema; “Hiki ndiyo kitu nitakachokwenda kukifanya kwa maisha yangu yote, sitajali iwapo nitalipwa au la. Nipo tayari kufanya bure, nipo tayari kulala nje na nipo tayari kula nyasi, ila hiki ndiyo nitakachofanya maisha yangu yote.”
Habari njema ni kwamba Bryon hakulala nje, wala hakula nyasi, bali alikuwa bilionea, kwa sababu kauli hiyo ilimfanya aache kuhangaika na mambo mengine na kuweka nguvu zake kwenye kile alichochagua.
Swali kwako rafiki yangu, ni kitu gani ambacho umekichagua kufanya maisha yako yote, ni kipi unaweza kutumia kauli hiyo ya kishujaa?
Shirikisha kwenye maoni hapo chini, kile ambacho umechagua kukifanya maisha yako yote, na kisha weka nguvu zako na umakini wako kwenye kitu hicho.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante sana kwa thread hii
Nimechagua kufanya kazi ya udaktari wa binadamu maisha yangu yote kutoa huduma hii bila kuangalia ni kipi kitakachonizuia kuhudumu nitakavyo kwa ubora na sitafanya kwa kuangalia kipato
LikeLike
Hongera Hendry.
LikeLike
Napenda sana ufugaji hasa ufugaji wa kuku,najua una changamoto nyingi lakini nipo tayari kuzikabili,pia najua nyuma ya ushindi kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa,hivyo katu sitakubali kukata tamaa.
LikeLike
Hongera Beatus.
LikeLike
Nimechagua kuelimisha watu juu ya malezi bora na fedha.Naamini kabisa nitaweza Kugusa wengi na kuleta mabadiliko kwa wengine.
LikeLike
Hongera Innocent.
LikeLike
Mimi na kichina,nimechagua kuwa mchina wa mwanza katika maisha yangu.
LikeLike
Hongera Alex
LikeLike
Shukrani Sana koacha kwa makala hii.Kauli yangu ya kishujaaa ni kutoa kwa wengine maisha yangu yote kadri Mwenyezi Mungu atakavyonijalia.
Asante.
LikeLike
Hongera Datius
LikeLike
Asante sana kocha.
Na mie kauli yangu ya kishujaa ni kuwa mwalimu wa mafanikio maisha yangu yote nikijua ukitoa unapata zaidi
LikeLike
Hongera Stephano.
LikeLike
Ahsante kocha nimechagua kuwa mfantabiashara wa wakala wa kifedha maisha yangu yote.
LikeLike
Vizuri Deo.
LikeLike
Nimechagua kujifunza kuhusu biashara na kufundisha na nitafanya hivyo maisha yangu yote,nijiona mkamilifu nikifundisha wengine, nikiona wengine wanaondoka kwenye changamoto zinazowakabili.
LikeLike
Hongera Kelvin.
LikeLike
Mie nimeamua kuwa mfanyabiashara wa bidhaa za chakula ili kukidhi mahitaji ya watu huku nikipata kipato, Hivyo nitaendelea kujifunza kuhusu mbinu mbali mbali za biashara kwa lengo hilo.
LikeLike
Hongera.
LikeLike
Nimechagua kuwa mkulima mkubwa, na ndio kitu nakifanyia kazi, nitang’ang’ana na sitaruhusu sababu yeyote inikwamishe.
LikeLike
Kila la kheri Yusuph.
LikeLike