Pita kwenye haya maisha kwa amani kadiri uwezavyo. Enenda na wengine kwa mapatano na jitahidi kadiri uwezavyo kutokuingia kwenye migogoro na wengine.
Mara zote fanya kile kilicho sahihi na simama kwenye ukweli na haki.
Kuna watu watachukizwa na wewe kuishi kwenye misingi hiyo, watajenga uadui na wewe, usijisumbue nao wala usilipe chochote kibaya wanachofanya.
Wewe waache wafanye yao, na wewe fanya yako ambayo ni kuishi kwa misingi yako.
Ishi maisha ya misingi hiyo na ambayo yatakuwa ya viwango vya juu, na hilo litakuwa maumivu tosha kwa wale wasiopendezwa na jinsi ulivyochagua kuishi.
Kwa yule anayekukosea au kukufanyia ubaya, usijisumbue, wacha asili impe majibu, maana asili huwa haikopeshi, inalipa kadiri ya mtu anavyofanya.
Epuka kujenga uadui na mtu yeyote, maana utaacha kuyaishi maisha yako na kuanza kuhangaika na maadui. Hata adui mmoja anatosha kukusumbua na kukuondoa kwenye misingi yako.
Lakini kwa wale wanaochagua kuwa na uadui na wewe, kwa sababu umechagua kuyaishi maisha yako, hilo lisikusumbue, watajitesa wao wenyewe na asili itawalipa kwa kiwango chao.
Una mengi tayari ya kukusumbua kwenye maisha yako, usiongeze uadui ambao utakusumbua zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ni kweli kocha,Nina mengi yanayonisumbua kwenye maisha yangu,kuongeza uadui na wengine Ni kuzidisha usumbufu zaidi.
Asante sana kwa makala nzuri.
LikeLike
Karibu Datius.
LikeLike