“The only person you are destined to become is the person you decide to be.” Ralph Waldo Emerson
Watu huwa wanaamini kwamba kila mtu anazaliwa na hatima ya maisha yake.
Kwamba mtu anazaliwa akiwa ameshapangiwa kabisa atakuwa na maisha ya aina gani.
Wale wanaoamini hivi ndiyo ambao huwa hawaweki juhudi kuboresha maisha yao.
Huamini kama ipo ipo tu.
Kwamba hata kama watajitahidi kiasi gani, kama hawakuandikiwa, kama siyo hatima yao basi haitatokea.
Huu siyo ukweli,
Huu ni uongo ambao umewapoteza wengi.
Kila mmoja wetu anazaliwa akiwa na uwezo mkubwa sana ndani yake,
Kila mmoja anaweza kuwa na hatima yoyote ile,
Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa, ni maamuzi ambayo watu wanafanya na hatua ambazo wanachukua.
Ukiamua kwamba unataka kuwa mtu wa aina fulani, unataka kufanya kitu fulani, ukaweka mipango ya namna ya kufikia maamuzi hayo na kisha kufanyia kazi mipango hiyo hila kuacha, lazima utapata kile unachotaka.
Hakuna anayezaliwa na hatima, bali kila mtu anaitengeneza hatima yake mwenyewe kwa maamuzi anayofanya na hatua anazochukua.
Asubuhi ya leo tafakari ni namna gani unayaendesha maisha yako,
Anza kwa kujiuliza ni mtazamo upi ulionao, je unaona hatima yako imeshatengenezwa au unaweza kuitengeneza mwenyewe?
Pia tafakari ni maamuzi yapi uliyofanya kwenye maisha yako na hatua unazochukua kila siku ili kuyafikia.
Kuanzia leo jua kila maamuzi unayofanya na kila hatua unayochukua ndiyo unatengeneza hatima yako mwenyewe, hivyo kuwa makini sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kujikinga na mihemko ya wengine, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/21/2021
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante Sana kocha kwa tafakari,hatima ya maisha yangu ipo mikononi mwangu, sitakubali kukata tamaa wala kurudi nyuma pamoja na kujua safari ya mafanikio sio rahisi nitajisukuma kila Siku kupambana bila kuchoka wala kuacha.ubarikiwe Sana kocha.
LikeLike
Vizuri kwa maamuzi hayo.
Kila la kheri.
LikeLike