Mwaka 1968 kwenye mashindani ya Olympic yaliyofanyika nchini Mexico, Tanzania iliwakilishwa na mwanariadha John Stephen Akhwari.

Kitu kimoja kikubwa ambacho watu hawajui kuhusu mashindano hayo ni kwamba japokuwa Akhwari hakushinda, lakini aliweka rekodi ya kipekee.

Muda mfupi baada ya mbio kuanza, Akhwari alianguka vibaya, kitu kilichopelekea kutenguka mguu na kuumia bega. Alipatiwa huduma ya kwanza na kushauriwa kutokuendelea na mbio, lakini yeye aliendelea.

Pamoja na maumivu makali aliyokuwa nayo, Akhwari aliendelea na mbio mpaka kukamilisha maili alizopaswa kukimbia. Alikamilisha mbio zake saa moja zaidi baada ya washindani wengine kuwa wamemaliza. Umati wa watu ulimsubiri na kushangilia licha ya muda kuwa umeenda sana.

Kwenye mbio alizoshiriki Akhwari, kulikuwa na washiriki 75 na kati yao, 18 waliishia njiani kwa sababu mbalimbali, ambapo hakuna aliyekuwa na sababu kubwa kama ya Akhwari. Lakini yeye alipambana mpaka akamaliza mbio, licha ya kuwa na maumivu makali.

Alipoulizwa kwa nini aliendelea kukimbia licha ya kuwa na maumivu, Akhwari alijibu; “Nchi yangu haijanituma maili 5,000 kuja kuanza mbio, bali imenituma kuja kumaliza mbio.”

Hebu soma tena jibu hilo na utafakari, na uone ni kauli ya kishujaa kiasi gani, uone jinsi mtu anapokuwa amedhamiria jambo, hakuna kinachoweza kumzuia asilifanye au asipate anachotaka.

Ninachotaka kukuambia leo rafiki yangu ni nguvu aliyoitumia Akhwari kuweza kukamilisha mbio licha ya maumivu makali, hata wewe unayo na unaweza kuitumia kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.

Mara ngapi umepanga kufanya kitu fulani, ila unajikuta umechoka na kushindwa kuendelea?
mara ngapi umekuwa unatamani uendelee kufanya kitu lakini usingizi unakubana na unashindwa kuendelea?

Yote hayo yanatokea kwa sababu hujaua siri kubwa ya mwili wako.

Iko hivi, mwili wako una nguvu kubwa ya ziada ambayo huwa inalinda usiitumie, hiyo ni nguvu inayohifadhiwa kama kutatokea dharura kubwa. Ndiyo maana hata kama umechoka kiasi gani, ukijikuta kwenye hatari kubwa, mfano unafukuzwa na mbwa mkali, unapata nguvu ya kukimbia na kujiokoa.

Pale unapojiona umechoka na huwezi kuendelea tena, unakuwa umetumia asilimia 40 tu ya nguvu na uwezo wa mwili wako. Kuna asilimia 60 bado hujaigusa kabisa. Hiyo ndiyo Akhwari aliweza kuitumia kwa sehemu na ndiyo ambayo wewe ukiijua na kuitumia, utaweza kufanya makubwa.

Kwenye kitabu kipya nilichotoa kinachoitwa UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, sura ya sita inaitwa USIKUBALI KUUMIZWA. Kwenye sura hii unajifunza siri moja kubwa ya kuweza kuvuka maumivu ya mwili na kuweza kufanya makubwa.

Kwenye sura hiyo unapata ufafanuzi wa kina kuhusu kanuni ya asilimia 40 na jinsi ya kuiongeza kidogo kidogo mpaka kuweza kufanya makubwa sana.

Rafiki, nisikucheleweshe kuijua siri hii, jipatie leo nakala yako ya kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA na uweze kujua nguvu na uwezo mkubwa wa akili na mwili wako na jinsi unavyoweza kutumia nguvu hizo kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.

Kitabu hiki kimechapwa (hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Kwa maisha yako yote, umekuwa unafichwa siri ambayo iko mbele ya macho yako, ni wakati sasa wa kufichua siri hiyo ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako na upate mafanikio makubwa.

ZAWADI NYINGINE YA KITABU.

Rafiki, kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kimeambatana na kitabu kingine kipya nilichotoa kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Kwa hali inavyoenda, kwa ukosefu wa ajira uliopo na unaoendelea kukua, biashara ndiyo mkombozi pekee kwa kila mtu kuweza kuingiza kipato sahihi kwake.

Lakini wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara kwa kubahatisha, nasema hivyo kwa sababu watu hawaanzi na mawazo sahihi ya biashara, hawajui taratibu mbalimbali za kufuata na pia hawana mikakati ya kuiwezesha biashara kukua na kutokuwategemea.

Kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kimekuja na jawabu, kinakupa yale maarifa ya msingi kabisa ambayo kila mtu aliye kwenye biashara au anayepanga kuingia basi anapaswa kuyajua na kuyafanyia kazi.

Hivyo kama tayari upo kwenye biashara au unapanga kuingia kwenye biashara, pata nakala yako leo ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA ili uweze kujenga biashara yako kwenye misingi sahihi na ufanikiwe.

Kitabu hiki kimechapwa (hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini leo ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 pekee. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania