
Kila mtu unayekutana naye, kuna kitu cha kujifunza kutoka kwake. Inaweza kuwa kitu cha kuanza kufanya au kuacha kufanya.
Kuwa tayari kujifunza na utajifunza mengi mno. Unaweza kwenda mahali kupata huduma fulani na kisha ukapata huduma ambayo ni mbovu mno. Badala tu ya kulalamikia huduma mbovu uliyopata, jifunze kutokufanya hivyo kwenye shughuli zako, umeyapata maumivu, hakikisha husababishi maumivu kama hayo kwa wengine.
Ukiwa mnyenyekevu kuna mengi mno ya kujifunza kutoka kwa wengine, ambayo ukiyazingatia, utaweza kupiga hatua kubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Asante sana kocha kwa tafakari hii,usipojifunza inamaana utakuwa ni upotevu wa muda,
LikeLike
Kabisa.
LikeLike